Ujenzi wa Njia Nne Bukoba unasuasua, Mamlaka hazifahamu barabara hiyo ndio mlango wa uchumi wa Mji?

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Your browser is not able to display this video.
Oktoba 28, 2023, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akiwa Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera alielekeza Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) - Kagera kumsimamia Mkandarasi M/s Abemulo Contractors Ltd afanye kazi usiku na mchana ya ujenzi wa upanuzi wa njia nne wa Barabara ya Bukoba (Rwamishenye) - Bukoba Port (km 5.1), sehemu ya kwanza yenye urefu wa Kilometa 1.

Akikagua kuanza kwa kazi ya Ujenzi wa upanuzi wa Barabara hiyo ya njia nne sehemu ya kwanza inayoanzia Round about ya Rwamishenye hadi eneo la Mitaga lenye urefu wa Kilometa 1, alielekeza ujenzi ufanyike kwa mtindo huo hili kukamilika kwa wakati.

Bashungwa alisema Tsh. Bilioni 4.61 zilitolewa kwa ajili ujenzi wa upanuzi sehemu ya kwanza inayoanzia Roundabout ya Rwamishenye hadi Mitaga yenye urefu wa Kilometa 1.

Ambapo katika kuhakikisha ujenzi huo unafanyika kama ilivyokusudiwa tayari kiasi cha shilingi bilioni 1.8 ilielezwa zilitengwa kwa ajili ya kulipa fidia.

Kwa mujibu wa TANROADS - Kagera ilielezwa utekelezaji ambao unafanywa na Mkandarasi M/s Abemulo Contractors Ltd utakuwa wa miezi 12 ambapo kazi kuanzia Oktoba 9, 2023.

Mkandarasi alianza na kasi lakini kwa sasa zoezi linaonekana kusuasua tofauti na matarajio yaliyokuwepo awali kwamba kipande hicho kitakamilika kwa wakati ikizingatiwa ilielezwa wazi fedha kwa ajili ya utekelezaji zilikuwa tayari zimeshatolewa.

Kwa sasa ni Desemba 2024, takribani miezi miwili inapita tokea muda wa ujenzi uliotajwa kwamba kipande hicho kikamilike hatuoni hizo dalili na Mkandarasi ni kama ameenda likizo, tunajiuliza kuna changamoto gani ambayo imepelekea ujenzi huo kutokukamilika kwa wakati?

Ujenzi wa barabara hiyo umekuwa ukipelekea baadhi ya shughuli zinazofanyika katikati ya Mji wa Bukoba kutofanyika kama ilivyozoeleka awali, hilo linachngiwa na magari mengi hasa makubwa kushindwa kuingia eneo la Mjini, ikizingatiwa hiyo ndio njia kuu inayotegemewa zaidi kuingia Mjini hasa kwa magari makubwa.

Hata hivyo wasiwasi wangu kama kipande hicho kinakaa kwa muda mrefu hivyo bila kukamilika wakati tayari pesa ipo, je awamu nyingine za uendelezwaji wa ujenzi ambazo zimeshatangazwa zitakamilika lini, hili kurejesha Mji katika hali ya kawaida hususani shughuli za kiuchumi?


Siku Waziri Bashungwa alipotembelea ujenzi wa Barabara hiyo


Pia soma
~
Serikali Kuongeza Bilioni 4 Kukamilisha Upanuzi wa Njia 4 Bukoba Mjini
~ Shilingi Bilioni 45.6 kutumika kukamilisha Miradi ya Dharura Mkoani Kagera
 
Kwanza meneja wa TANROAD unajua ni nani na kwanini kawekwa hapo??
 
Hizo pesa sio za ndani ni za world Bank ndo inalazimisha njia nne kutoka bukoba mjini mpaka mtukula mpakani wa Uganda na Tanzania, ila suali ni kwamba ni njia nne kwa gari zipi uko bukoba au ni njia nne za bodaboda?.......hizo pesa zingeenda kutengeneza njia sita Mwanza ile njia ya kutoka Dar kuanzia Buhongwa mpaka Airport gari ni nyingi kupita maelezo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…