Elitwege
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 5,294
- 10,970
Unajua China walichofanya ndani ya miaka 70 ya uhuru wao?Viongozi kutoka kanda ya ziwa tuwe na tahadhari nao kama taifa. Alichofanya jpm kinafanana na Alichofanya Mwl Nyerere mwaka 1978 alipotuingiza kwenye vita isiyo ya lazima na uganda na kutuaminisha kuwa uwezo wa kumpiga tunao, sababu na Nia ya kumpiga tunavyo pia. Lakini ona, kumbe ki uchumi hatukuwa na uwezo huo aliotuambia. Baada ya vita ile hali yetu ikawa mbaya hadi Leo. Jpm alitudanganya kuwa pesa za kujenga sgr, bwawa, Kuhamia dodoma, kujenga madarasa tunazo kumbe sio kweli.
Ni Heri kuwaambia watu ukweli ili wajiandae na hali kuliko kusema uongo. Sisi pesa tunazo kweli lakini ziko ardhini na baharini hatuwezi kuzitumia. Viongozi wetu walipuuza ushauri wa kuchimba chuma chetu kule liganga na mchuchuma, hivi sasa tungeijenga reli kwa kutumia chuma chetu wenyewe na kupunguza gharama za ujenzi.
Watanzania wenye uhuru wa miaka 60 washindwe kusimamia reli ya SGR?