Ujenzi wa SGR Mwanza-Isaka kuanza wakati wowote

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Kauli hii imetolewa na mkurugenzi wa TRC ndugu Masanja Kadogosa akiwa Malampaka mkoani Simiyu.

Kwa mujibu wa ndugu Kadogosa ni kuwa kutakuwa na kambi kubwa hapo Malampaka ambayo itachukua takribani watu 3000. Kipande hiki kina takribani KM 341 na kitagharimu tril tatu nukta sita za Kitanzania. Masanja Kadogosa amedai kuwa tayari wamefanya kikao na wadau ili kuweka utayari wa kuanza mradi huo.

Je, kwanini kandarasi ya kutoka Makutupora mpaka Isaka haikuanza kutangazwa? Maana mradi umeanzia Dar ukielekea Mwanza.
 
Mradi una awamu 5 na sasa awamu zilizoanza kutekelezwa ni 3. Nazo ni Dar kwenda Morogoro, Morogoro kwenda Makutopola Singida (maarufu kama Morogoro kwenda Dodoma japo imevuka Dodoma). Isaka mkoani Shinyanga kwenda Mwanza.

Awamu ambazo hazijaanza ni Isaka mkoani Shinyanga kupitia Kahama mjini kwenda Uvinza Kigoma hadi mpakani mwa Burundi na Rwanda. Makutupola mkoani Singida hadi Isaka mkoani Shinyanga.

Kwanini wameanza na awamu ya Isaka hadi Mwanza hilo wanalijua wao kimkakati zaidi yaweza kuwa ni pesa inatosha kipande hicho au pengine ni sababu za kiuchumi. Cha msingi awamu zote zikamilike
 
Kipande gani kimekamilika?
 
Lazima kitatoboa Shato maana Isaka- Mwanza haizidi 200km, sasahiyo 341 inatoka wapi kama siyo mpaka Shato?
Nikusaidie na ndio maana huwa mnakurupuka.

Kuanzia Dar hadi Morogoro ni kati ya klm 220 lakini zimejengwa klm 330 au zaidi vivyo hivyo kwa Dodoma, na Mwanza hivyo hivyo,
Katika hiyo reli kuna sehemu zinajengwa njia mbili kwa ajili ya kupishana, kwa hiyo hiyo njia ya pili pia inawekwa kwenye urefu wa hizo meter.

Nadhani umeelewa.
 
Awamu ambazo hazijaanza ni Isaka mkoani Shinyanga kupitia Kahama mjini kwenda Uvinza Kigoma hadi mpakani mwa Burundi na Rwanda. Makutupola mkoani Singida hadi Isaka mkoani Shinyanga.
Nadhani umekosea ni Rusumo mpaka wa Rwanda na Tanzania maana kama ni kwenda Uvinza lazima ipite Tabora hadi Kigoma.
 
Mradi una awamu 5 na sasa awamu zilizoanza kutekelezwa ni 3. Nazo ni Dar kwenda Morogoro, Morogoro kwenda Makutopola Singida (maarufu kama Morogoro kwenda Dodoma japo imevuka Dodoma). Isaka mkoani Shinyanga kwenda Mwanza.

Awamu ambazo hazijaanza ni Isaka mkoani Shinyanga kupitia Kahama mjini kwenda Uvinza Kigoma hadi mpakani mwa Burundi na Rwanda. Makutupola mkoani Singida hadi Isaka mkoani Shinyanga.

Kwanini wameanza na awamu ya Isaka hadi Mwanza hilo wanalijua wao kimkakati zaidi yaweza kuwa ni pesa inatosha kipande hicho au pengine ni sababu za kiuchumi. Cha msingi awamu zote zikamilike.
Njia ya DAR to MWANZA ina Lot 5.Ya kwanza Dar t- Morogoro, 2 Morogoro - Makutopora,3 Makutupora - Tabora,4 Tabora - Isaka,5 Isaka- Mwanza. Lot nyingine ndio hiyo Isaka- Kigali na Tabora- kigoma. Wanachotaka kuanza sasa ni lot 5.
 
Mwezi April Wamesema Kutoka Dar Es Salaam ~Morogoro Ni Treni Tu
 
Kauli hii imetolewa na mkurugenzi wa TRC ndugu Masanja Kadogosa akiwa Malampaka mkoani Simiyu.

Kwa mujibu wa ndugu Kadogosa ni kuwa kutakuwa na kambi kubwa hapo Malampaka ambayo itachukua takribani watu 3000 . Kipande hiki kina takribani KM 341 na kitagharimu tril tatu nukta sita za kitanzania. Masanja Kadogosa amedai kuwa tayari wamefanya kikao na wadau ili kuweka utayari wa kuanza mradi huo.

Je,kwa nini kandarasi ya kutoka Makutupora mpaka Isaka haikuanza kutangazwa ? Maana mradi umeanzia Dar ukielekea Mwanza.
Naskia inaenda mpka Chato kubeba fisi wala watu
 
Back
Top Bottom