Ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Arusha utakaotumika kwenye Fainali za AFCON 2027 wafikia 11%

Ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Arusha utakaotumika kwenye Fainali za AFCON 2027 wafikia 11%

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
UJENZI WA UWANJA WA AFCON ARUSHA WAFIKIA 11%

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa amesema anaridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Arusha unaotarajiwa kutumika kwa ajili ya Fainali za AFCON 2027 ambao hadi sasa umefikia 11% za ujenzi.

Msigwa amesema hayo wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya Mradi wa ujenzi wa uwanja huo unaojengwa katika kata ya Olmoti jijini Arusha kwa saa 24 usiku na mchana.

Aidha, Msigwa mesema pamoja na kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo, hata hivyo amemtahadharisha mkandarasi huyo kuwa siku atakapochelewesha kazi ya ujenzi wa uwanja huo ndipo ugomvi wake na mkandarasi huyo utakapo kuja hata kabla Waziri wa Wizara yake Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro hajaja.

Msigwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa Uwanja huo wa Michezo wa Arusha unaotarajiwa kutumika kwa ajili ya Fainali za AFCON 2027 ambapo fedha za ujenzi wa Uwanja huo zimekuwa zikija kwa wakati kutoka Wizara ya Fedha.
IMG-20241130-WA0017.jpg
IMG-20241130-WA0009.jpg
IMG-20241130-WA0016.jpg
IMG-20241130-WA0015.jpg
IMG-20241130-WA0014.jpg
IMG-20241130-WA0013.jpg
IMG-20241130-WA0010.jpg
IMG-20241130-WA0012.jpg
IMG-20241130-WA0011.jpg
 
Hivi kuuboresha ule uwanja wa Sheikh Amri Abeid, halafu ukajengwa uwanja mwingine mpya Dodoma! Si ingependeza sana.
Kwa hiyo kwa uelewa wako Dodoma ina more spending capacity na facilities za ku-host event kuliko Arusha?

Kiukweli kuna baadhi ya mikoa mnabebwa! Ila kama ni suala la business sense hamna mtu binafsi anaweza kujenga uwanja Dodoma akaacha Arusha kwa sasa! Naamini hata huo utakaojengwa Dodoma sijui kama utajaa kipindi cha AfCON 2027!

BTW Sheikh Abeid Karume hamna nafasi ya kutosha pale! Kwanza hata hiyo Idadi ya 30,000 naona ni ndogo wangefanya 40,000 kwa Jiji la Arusha!
 
Fedha za kujenga uwanja zimetoka wapi wakati Tarura na Tanroads, walalalia makande!
 
Kikarabati chama cha mboga mboga maana sio waserikali mkuu. Mgongano wa kimaslahi baadae utasumbua
hapana ni chama cha uma ndugu..mali na vyote ndani ya jamuhuri ni mali ya chama siona tatizo kwenye hilo
 
Back
Top Bottom