Ujerumani ina watu milioni 82 ilhali baiskeli zipo mil. 81, Tanzania baiskeli ni alama ya umaskini

Ujerumani ina watu milioni 82 ilhali baiskeli zipo mil. 81, Tanzania baiskeli ni alama ya umaskini

Kuna dogo mmoja kahama makazi Dar, amehamia nje kidogo ya mji.

Akawa anasema anafikiria kutumia baiskeli kama usafiri.

Kutumia baiskeli kwa usafiri Dar kuna usalama kiasi gani?
Dar es Salaam na miji mikubwa ya Afrika kwa ujumla sio mahala salama kuendesha baiskeli. Hatuna barabara zilizotengwa kwa usafiri huo, mshauri aachane na hilo wazo. Mwambie huku sio Amsterdam hata njia za watembea kwa miguu tu unatembea ukiwa makini.
 
Awe makini tu mbona kuna wauza mayai wanatoka Tegeta hadi GMboto
Halafu mayai hayavunjiki wala hayapasuki, na vurugu zote zile za barabara za Dar.

Aisee hicho nacho ni kipaji.
 
Dar es Salaam na miji mikubwa ya Afrika kwa ujumla sio mahala salama kuendesha baiskeli. Hatuna barabara zilizotengwa kwa usafiri huo, mshauri aachane na hilo wazo. Mwambie huku sio Amsterdam hata njia za watembea kwa miguu tu unatembea ukiwa makini.
Na mimi huu ndio wasiwasi wangu mkubwa.
 
Halafu mayai hayavunjiki wala hayapasuki, na vurugu zote zile za barabara za Dar.

Aisee hicho nacho ni kipaji.
Kuna mmoja nilimshuhudia anawahi Kariakoo kununua Mayai alikua na mkono 1 ila anaendesha baiskeli
 
Nchi ya Ujerumani ina idadi ya watu milioni 82 huku watu hao wakimiliki jumla ya baiskeli milioni 81. Ujerumani inayo jumla ya magari milioni 48. Mtoto akifika miaka 11 anatakiwa kujifunza na kukata leseni ya baiskeli ili kuweza kuendesha baiskeli kwenye barabara za umma. Barabara husika nyingi zimetengwa sehemu ya waendesha baiskeli.

Jumla kulikuwa na ajali 85,000 za baiskeli nchini Ujerumani huku 372 kati yao wakipoteza maisha Cologne na Berlin zikiongoza kwa ajali! Wajerumani wameamua kujenga barabara za mwendokasi za baiskeli. Ulaya matumizi ya baiskeli ni maarufu huku Amsterdam ukiwa machampioni. Matumizi ya baiskeli yanaimarisha afya na kutochafua mazingira.

Tanzania kwa mijini wengi wanaoendesha baiskeli ni wale wasioweza kumudu gharama za nauli na kwa baadhi ya mikoa iliyokuwa na utamaduni wa kutumia baiskeli, utamaduni huo unakufa taratibu baada ya kutamalaki kwa ujio wa boda!

Taarifa kwa msaada wa DW

Baiskel kama usafiri pekee ni umaskini, hao watu wote wenye baiskeli wana magari, usifikiri wakitaka kwenda mji mwingine wanaenda na baiskeli, au wanapanda daladala, huku mtu anatoka mwanza mpaka shinyanga na baiskeli, nini huo kama sio umaskini?
 
Za ujerumani ni baiskel za Tz ni basikeli kunatofauti kubwa, Tz basikel ukimwagia mchuzi fisi wanaitafuna.
 
Ni sahihi ndio maana wasukuma wana watoto wengi
 
Wazungu walishaboresha barabara kila kona ya nchi, kumiliki magari sio ishu tena
Tanzania kufikia hatua hiyo labda mwaka 2999
 
Ndio ivyo, Tanzania ukikutwa unakula chungwa kutoka Chanika au Tanga wewe ni masikini lakini ukikutwa na box ya juice yenye picha ya chungwa wewe mambo yako safi
 
Ungekuja na idadi ya magari ili ujue kuwa hizo baiskeli nyingi ni za mazoezi tuu mtu unakuta ana Baiskeli, Gari, Boat na motorbike ya BMW 1200 huyo unamuweka kwenye kundi lipi harafu hao watu wana bara bara za kila chombo bila usumbufu...
 
Kuna mmoja nilimshuhudia anawahi Kariakoo kununua Mayai alikua na mkono 1 ila anaendesha baiskeli
Huyo na wenzake kama yeye inafaa tuwafanyie documentary ya "Tanzanian Profiles in Courage".
 
Miji ambayo inautamaduni wa muda mrefu wa kutumia Baiskeli kama Tanga inatakiwa kujenga bike lanes. Miji mingine kama ya nyanda za juu baiskeli si rafiki sana sababu ya milima.
 
Nchi ya Ujerumani ina idadi ya watu milioni 82 huku watu hao wakimiliki jumla ya baiskeli milioni 81. Ujerumani inayo jumla ya magari milioni 48. Mtoto akifika miaka 11 anatakiwa kujifunza na kukata leseni ya baiskeli ili kuweza kuendesha baiskeli kwenye barabara za umma. Barabara husika nyingi zimetengwa sehemu ya waendesha baiskeli.

Jumla kulikuwa na ajali 85,000 za baiskeli nchini Ujerumani huku 372 kati yao wakipoteza maisha Cologne na Berlin zikiongoza kwa ajali! Wajerumani wameamua kujenga barabara za mwendokasi za baiskeli. Ulaya matumizi ya baiskeli ni maarufu huku Amsterdam ukiwa machampioni. Matumizi ya baiskeli yanaimarisha afya na kutochafua mazingira.

Tanzania kwa mijini wengi wanaoendesha baiskeli ni wale wasioweza kumudu gharama za nauli na kwa baadhi ya mikoa iliyokuwa na utamaduni wa kutumia baiskeli, utamaduni huo unakufa taratibu baada ya kutamalaki kwa ujio wa boda!

Taarifa kwa msaada wa DW
Kuna sehemu labda ni typing error. Hakuna leseni ya kuendesha baiskeli hapo Ujeruman. Nina uhakika na Ninacho andika hapa kwani nimepanda sana baiskeli hapo nilipo kuwa mwanafunzi sehemu za Mannheim. Ilikuwa ni mkakati wa ku-serve pesa badala ya kupanda Tram au bus. Ila nchi ya ulaya yenye baiskeli zaidi ni Holland jirani yake. Germany inafuatia. I stand to be corrected
 
Duh! Hii kali, yaana ni mtu mmoja tu ndiye hana baiskeli! Mi hata niwe na gari na pikipiki sitaacha kuwa na baiskeli
 
Watu wa takwimu na sensa watuambie mkoa wa shinyanga una baiskeli ngapi? Nilifika moshi vijijini mwaka 2010 kule moshi chini TPC usafiri wa haraka ulikuwa ni wa baiskeli kama kule shinyanga lakini sasa vijiwe vya baiskeli vimegeuka na kuwa vya bodaboda, baiskeli hazipo
 
Back
Top Bottom