Ujerumani kuanza mgao wa mafuta

Ujerumani kuanza mgao wa mafuta

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Ujerumani imetangaza rasmi kuanza kutoa gesi kwa watu wake kwa mgao, huku kukiwepo wasiwasi ya kuacha kuagiza mafuta kutoka Russia.

Hatua hiyo imechukuliwa wakati kuna hali ya kutoelewana kuhusu malipo kwa kutumia sarafu ya Russia.

Hatua ya umoja wa ulaya kuanza kutekeleza onyo la mapema la uwezekano wa kutokea uhaba wa gesi, ni ishara ya moja kwa moja ya kutokea uhaba wa mafuta kutokana na uvamizi wa Russia nchini Ukraine.

Waziri wa uchumi wa Ujerumani Robert Habeck, ameambia waandishi wa habari kwamba chumba cha dharura kitaundwa ndani ya wizara hiyo, akiongezea kwamba timu itakayosimamia swala hilo itahusisha wanachama kutoka kwa wizara hiyo, wasimamizi wa mafuta nchini humo na wadau kutoka sekta binafsi.

Katika hatua inayoonekana kama juhudi za kuimarisha sarafu yake ambayo inaendelea kupoteza thamani, Russia imesema kwamba itaweka mikakati ifikapo March 31, ambapo nchi ambazo zimetajwa kwamba sio rafiki, zile ambazo zimeiwekea vikwazo, zitalipia gesi yake kwa kutumia sarafu ya Russia na wala sio Euri wala dola ya Marekani.

Moscow inatarajiwa kuzindua kanuni mpya kuhusu malipo ya gesi kesho alhamisi.

Kremlin imesisitiza kuhusu mfumo kwa malipo ya gesi kwa umoja wa ulaya, baada ya mawaziri kutoka nchi 7 tajiri duniani kutaja mpangilio huo kuwa usiokubalika.

Uvamizi wa Ukraine imepelekea Russia kuwekewa vikwazo kadhaa na kupelekea sarafu yake kushuka kwa thamani huku Ulaya ikisitisha uagizaji wa mafuta na gesi kutoka Russia.

VOA Swahili
 
Ndo shida ya kuingilia ugomvi usiokuhusu.

Hivi ujerumani alkua na ugomvi gan na RUSSIA mpk nae ashiriki kumpiga SANCTIONS.

Angalia Sasa wajerumani wanaishi kwa tabu kwasababu ya viongzi wao kua vibaraka wa USA na kupelekeshwa ovyo.

Pongezi kwa TANZANIA kutokufungamana upande wowote, japo kias chake tunaathirika[emoji4][emoji106]
 
Ndo shida ya kuingilia ugomvi usiokuhusu.

Hivi ujerumani alkua na ugomvi gan na RUSSIA mpk nae ashiriki kumpiga SANCTIONS...
Hii ni fundisho kuwa ugomvi usio kuhusu usiuvalie kibwebwe.

Na mbaya zaidi ujerumani kuna military base ya marekani na CIA sub station kubwa tu kwa Europe.

Ujerumani wana tabu sana
 
(Kremlin imesisitiza kuhusu mfumo kwa malipo ya gesi kwa umoja wa ulaya, baada ya mawaziri kutoka nchi 7 tajiri duniani kutaja mpangilio huo kuwa usiokubalika.)
 
Urusi ndio taifa la kwanza kuwaumiza Wamagharibi kwa vikwazo vyao wenyewe.
Hongera Putin.
Kwani Russia inawapa ulaya gesi na mafuta bure inauwauzia, ulaya kugoma kununua gesi na mafuta itawaumiza wananchi wake na pia urussi atapata hasara sababu mapato yake mengi yanatokana na gesi na mafuta tuacheni ushabiki wa kitoto
 
Kivip yaani Kwan Russia inawapa ulaya gesi na mafuta bure sababu umecomment as if anawapaga ulaya gesi na mafuta bure
Logic hapa
-ulaya na us wanaiwekea vikwazo Urusi including vya kifedha ikiwemo Ruble
-Urusi anasema anauza Gesi yake kwa ruble tu

Hii ina maana ili ulaya wapate Gesi inabidi wale matapishi yao.

Angalia thamani ya Ruble ilivyopanda Sasa hivi inacheza around 80 vs usd zamani ilikua 140 baada ya vikwazo.

Putin alijipanga sana, ulaya walikurupuka.
 
Lengo la vikwazo ni kuiumiza Urusi, siyo wao.

Kwahiyo wanapoumia na wao maana yake lengo halijafanikiwa - ime-backfire.
 
Kivip yaani Kwan Russia inawapa ulaya gesi na mafuta bure sababu umecomment as if anawapaga ulaya gesi na mafuta bure
Shida sio kuwapa bure, shida ni vikwazo walidhani yeye ndiye atapata tabu peke yake, sasa kawakomesha either wanunue kwa kutumia pesa yake au hauzi. Wamelianzisha sasa wanacheza ngoma yake
 
Kwani Russia inawapa ulaya gesi na mafuta bure inauwauzia, ulaya kugoma kununua gesi na mafuta itawaumiza wananchi wake na pia urussi atapata hasara sababu mapato yake mengi yanatokana na gesi na mafuta tuacheni ushabiki wa kitoto
Wanajifanya hawajui hili,wewe waache hawajui kwamba hii issue itawaumiza Ulaya in short-term but in long-term inakula mazima kwa Urusi.
 
Logic hapa
-ulaya na us wanaiwekea vikwazo Urusi including vya kifedha ikiwemo Ruble
-Urusi anasema anauza Gesi yake kwa ruble tu

Hii ina maana ili ulaya wapate Gesi inabidi wale matapishi yao.

Angalia thamani ya Ruble ilivyopanda Sasa hivi inacheza around 80 vs usd zamani ilikua 140 baada ya vikwazo.

Putin alijipanga sana, ulaya walikurupuka.
Putin alijipangaje? Hujui kwamba hili swala litawaumiza Ulaya in short-term but in long-term Urusi ndio atakiona cha moto maana wataacha kununua gas yake mazima.
Screenshot_20220331-114836.jpg
 
Ndo shida ya kuingilia ugomvi usiokuhusu.

Hivi ujerumani alkua na ugomvi gan na RUSSIA mpk nae ashiriki kumpiga SANCTIONS.

Angalia Sasa wajerumani wanaishi kwa tabu kwasababu ya viongzi wao kua vibaraka wa USA na kupelekeshwa ovyo.

Pongezi kwa TANZANIA kutokufungamana upande wowote, japo kias chake tunaathirika[emoji4][emoji106]
Sisi hatujaweka vikwazo na hatuna uwezo huo ila sasa hivi lita moja mafuta ya kula ni 8000. Kufikia juma lijalo yatakua 9000 au 10,000.

Hili joto litakufanya vita ikuguse utake usitake.
 
Lengo la vikwazo ni kuiumiza Urusi, siyo wao.

Kwahiyo wanapoumia na wao maana yake lengo halijafanikiwa - ime-backfire.
Wewe unadhani Ulaya hawakujua hili la Gas na mafuta kuwa litawapa shida kwa muda fulani but in long run watakuwa wamejiondoa kwenye utumwa wa Gas ya Russia? Kwanza hata leo wakiamua kupata mbadala wanao ambao ni Makaa ya Mawe halafu tuone hiyo Gas Urusi atamuuzia nani.
 
Back
Top Bottom