Ujerumani kusitisha uuzaji wa silaha kwa Israel zinazoweza kutumika Gaza, Merz asema

Ritz

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Posts
57,035
Reaction score
46,479
Wanaukumbi.

Ujerumani itasitisha uuzaji wa silaha zake kwa Israel ambazo zinaweza kutumika katika Ukanda wa Gaza, Kansela Friedrich Merz anasema kutokana na mipango ya Israel ya kuuteka mji wa Gaza.

Akizungumza muda mchache uliopita, Merz amesema serikali yake haitaidhinisha usafirishaji wowote wa zana za kijeshi kwa Israel ambazo zinaweza kutumika Gaza hadi ilani nyingine itakapotolewa.

Merz anasema ilikuwa "inazidi kuwa vigumu kuelewa" jinsi mpango wa kijeshi wa Israel ungesaidia kufikia malengo halali, akiongeza: "Katika mazingira haya, serikali ya Ujerumani haitaidhinisha mauzo yoyote ya zana za kijeshi ambazo zinaweza kutumika katika Ukanda wa Gaza hadi ilani nyingine."

Kihistoria, Ujerumani imekuwa mojawapo ya wauzaji wakubwa wa silaha kwa Israeli.

Kulingana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm (Sipri),-Taasisi ya utafiti ambayo inaangalia migogoro na silaha, Marekani ilikuwa muagizaji mkuu wa silaha za Israel na zana za kijeshi kijeshi katika kipindi cha kati ya 2020-2024, na Ujerumani ikiwa ya pili.

Usiwaamin wazungu linapokuja swala la israel ni kama mbwa kwa chatu . Amesema hivyo ili kupunguza pressure tu ya watu wake
 
Baada ya Ujerumani kusema haya nawaona wayahudi weusi kutoka maeneo mbali mbali Tukuyu, Kwimba, Mwabuki, Nyasho, Makete, Uyole, Nyambiti kila moja anakuja na tamko lake😂
 
Baada ya kuuliwa watu laki 5 gaza ndo wanasitisha shenz kbs hawa
 
Washajua uko mbole kitawakuta tu Damu za Binadamu wasiokuwa na hatia uwa chungu kwa kila muhusika. Lazima watalipia tu hata iwe miaka 30 mbele. Pesa za silaha zitawadidiza Ujerumani.
 
Usiwaamin wazungu linapokuja swala la israel ni kama mbwa kwa chatu . Amesema hivyo ili kupunguza pressure tu ya watu wake
ni kwamba hawawataki hao waisrael kwenye nchi zao kwa hivyo wanaona bora wabakie huko huko walikowapeleka
 
Back
Top Bottom