hiii kesi ni ngumu, usiseme sio ngumu, ni kwamba tukio hili limemweka lulu katika hali ya kuharibiwa maisha, hata akitoka leo hii itamwathiri maisha yake yote, cha kuelewa ni kwamba, kuanzia sasaivi hadi siku upelelezi utakapokamilika na yeye kufungiwa PI (to be committed to the High court), itachukua muda kwa wapelelezi wa hapa tz, hata miaka miwili, muda wote huo atakuwa ndani. jalada likipelekwa kwa state attorney wakaangalia aina ya kosa la kumshitaki kulingana na maelezo ya mashahidi basi hapo ndo ataweza kupata dhamana kupitia high court kama itakuwa proposed kwamba ashitakiwe kwa manslaughter. baada ya hapo, atafungw amiaka michache tu, wkasababu kwa mazingira halisi, hii ilikuwa bahati mbaya na labda ilitokana na kupigana ambako kisheria huishia kwenye manslaughter. lakini kwa sasa, naweza sema uyu mtoto atatumikia jela si chini ya miaka minne kuanzia sasa, kusubiria upelelezi hadi kesi kusikilizwa. miaka hii kuishi jela si michache. akitoka future yote imeharibika. namwonea huruma sana.