Ujinga alioufanya msanii Willy Paul jana dhidi ya wasanii wa Tanzania ukemewe vikali

Ujinga alioufanya msanii Willy Paul jana dhidi ya wasanii wa Tanzania ukemewe vikali

Kakutana na wakenya vichwa ngumu. Eti anazira afu mwanaume.
Lol
Hata kama chuki ila suo kihivyo coca. Kapanda mkenya na kuongea shit hukubanalia jukwaani then aje apande mondi? Usalama wake ungekuwaje?

Msilaumu na kubeza kwa kila kitu. Kiusalama hata mi nisingepanda na kuimba jukwaani mkuu.
 
tatizo media za kenya na waandaa matamasha wanadharau wasanii wao hawawapi kipaumbele. ana hoja lakini haikua platform sahihi.
Mzee heshima huwa haiombwi, unatakiwa uifanyie kazi uheshimike.

Mbona wakina Prezoo, Wahu, Jaguar, Jua Kali wametengeneza jina kubwa sana hapa Tanzania? Wafanye mziki mzuri tu sio kueneza chuki.
 
Mzee heshima huwa haiombwi, unatakiwa uifanyie kazi uheshimike.

Mbona wakina Prezoo, Wahu, Jaguar, Jua Kali wametengeneza jina kubwa sana hapa Tanzania? Wafanye mziki mzuri tu sio kueneza chuki.
Hii issue imenifikirisha sana, Wakenya wapo obsessed sana na mafanikio ya Watanzania sijui shida ni nini? Hawataki kuona tumewazidi kwa chochote, wakati huo huo ikitokea wao wamepiga hatua kwa chochote kutuzidi utawasikia wanatuponda na kutukandia kuwa sisi si chochote, sasa wanatakaje? Kwa Miaka kadhaa sasa entertainment industry ya Tanzania ipo juu sana hasa upande wa Muziki kuliko nchi yeyote ya Afrika Mashariki, hiki kitu wanamuziki wa Kenya huwa kinawaumiza sana kukubali na kujikuta hawana namna huku mioyo yao ikivuja chuki na matokeo yake ndo hayo ya Willy Paulo, hayo ni matokeo ya kile walichokitunza ndani mwao kwa muda mrefu sana ndiyo maana karibu kila mwanamziki na celeb wa kipande hicho anakubaliana na kile alichofanya mwenzao, wanasahau kuwa muziki wetu na tasnia nzima ya Bongo Flavour kufika hapa ilipo ni matokeo ya juhudi na maarifa mengi na kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa hasa Nigeria na South Africa.
 
mawazo ya kimasikini haya mkuu punguza jazba
Laaana za kupitiwa na pididi...yalianzia hukohuko bet na komasava yake chalii. ,,huku Kenya tena nako chalii na bado mwanzo huo laana inakuja kumuandama hadi huku bongo.........bora nile flava za khalighraph jones kuliko kusikiliza upuuzi wa wakina zuchu na mke wa pididi hehehe kumbe kwanza mambo yalianzia mbeya sinza pazuri Kazi iendeleee
 
Wakenya wana wivu na chuki sana willy ni msanii mzuri lakin hawezi kumfikia Diamond hao wote wajitape Diamond yupo juu mziki wa 𝑻𝒁 unaongoza watulie ,nimefurahi diamond kughairi na kuondoka
Shida nyingine wasanii wa Kenya ushoga unawatafuna sana aisee huyo wili poo mwnyw punga tu
 
Nimefatilia hii ishu wengi hata hamjaelewa, willy paul yupo sahihi maana ratiba ilionyesha atapanda yeye kwanza.... siku zote wasanii wadogo hupanda kwanza msanii mkubwa anakua wa mwisho hii hata kwenye boxing tunaona wanaanza wapiganaji wadogo main event inakua mwisho

Tatizo hawakwenda na ratiba vizuri muda ukawa unaenda diamond akawa analazimisha yeye apande amalize aondoke zake na zuchu wake ndo willy paul akataka ratiba ifuatwe kama kawaida


Diamond akalazimisha kupanda stejini kama kawa wakenya ni vichwa vigumu na hawapendi shobo wakamzomea akasepa zake... wakenya hawana ujinga... zuchu angejaribu kuwanyooshea dole la kati kama alivyofanya mbeya wangemkata masikio stejini
Hakuna kitu wewe. Kwani nani hajafuatilia?. Huyo dogo ndio alitaka awe wa mwisho kwa kusema yeye ni mkubwa kuliko Diamond. Diamond akaona isiwe kesi akakubali kabla ya huyo bwege wako unaemsapot. Sasa huyo kenge wako baada ya Diamond kushika stage vibe la kumwaga kwa wana ukumbini,akabadiri gear,akaanza kulazimisha ilikuwa zamu yake (Kumbuka hapo hao wasanii kenge wa Kenya walikuwa tayari wameshajipanga kushusha maneno mabovu kwa wasanii wa Tanzania. WIVU

MY TAKE. UKUBWA WAKO AU UMAARUFU WAKO HAUTOKANI NA WEWE KUULAZIMISHA. UKUBWA AU UMAARUFU WAKO UNATOKANA NA KAZI ZAKO KUBWA NA MATENDO YAKO. HIYO NI KUANZIA NGAZI YA FAMILIA,UKOO,KIONGOZI,MCHEZAJI NA MSANII. HIVYO WATU NDIO WANAOKUPA UMAARUFU KUTOKANA NA KAZI ZAKO AU MATENDO YAKO BORA KWA JAMII. KAMA ILIVYO KWA DIAMOND.
HAIWEZI KUTOKEA KAMA HAO KENGE WA KENYA WALIVYOJITANGAZA UKUBWA STAGINI. NEVER. DIOMOND BADO ATABAKI KUWA JUU SANA PAMOJA NA KWAMBA NYIE BAADHI YA VIJANA KSBB YA UVIVU WENU MNABAKI KUMDISS. WIVU WA KIJINGA
 
Hakuna kitu wewe. Kwani nani hajafuatilia?. Huyo dogo ndio alitaka awe wa mwisho kwa kusema yeye ni mkubwa kuliko Diamond. Diamond akaona isiwe kesi akakubali kabla ya huyo bwege wako unaemsapot. Sasa huyo kenge wako baada ya Diamond kushika stage vibe la kumwaga kwa wana ukumbini,akabadiri gear,akaanza kulazimisha ilikuwa zamu yake (Kumbuka hapo hao wasanii kenge wa Kenya walikuwa tayari wameshajipanga kushusha maneno mabovu kwa wasanii wa Tanzania. WIVU

MY TAKE. UKUBWA WAKO AU UMAARUFU WAKO HAUTOKANI NA WEWE KUULAZIMISHA. UKUBWA AU UMAARUFU WAKO UNATOKANA NA KAZI ZAKO KUBWA NA MATENDO YAKO. HIYO NI KUANZIA NGAZI YA FAMILIA,UKOO,KIONGOZI,MCHEZAJI NA MSANII. HIVYO WATU NDIO WANAOKUPA UMAARUFU KUTOKANA NA KAZI ZAKO AU MATENDO YAKO BORA KWA JAMII. KAMA ILIVYO KWA DIAMOND.
HAIWEZI KUTOKEA KAMA HAO KENGE WA KENYA WALIVYOJITANGAZA UKUBWA STAGINI. NEVER. DIOMOND BADO ATABAKI KUWA JUU SANA PAMOJA NA KWAMBA NYIE BAADHI YA VIJANA KSBB YA UVIVU WENU MNABAKI KUMDISS. WIVU WA KIJINGA

Kumbe alikubali kumpisha Diamond atumbuize, baadaye alipoona nyomi inamkubali kwa vibe la hatari, akabdili gia hewani, akaanza kung'ang'ania atumbuize yeye.
Huyu msanii ni jinga sana.
 
Jana usiku kulikuwa na Tamasha pale Nairobi ambalo moja ya Wasanii walioalikwa kutumbuiza ni Wasanii kutoka Tanzania, Diamond Platnumz akisindikizwa na Zuchu huku Msanii mwingine akiwa Rayvanny.

Vurugu zilianza baada ya muda wa Diamond Platinumz kupanda stejini kufika ambapo Msanii wa Kenya Willy Paul Msafi kulazimisha kupanda stejini eti kwa kuwa yeye ni msanii wa Kenya hivyo anapaswa kupanda mwanzo kabla ya Diamond Platnumz, na akadai yeye kuwekwa wa mwisho baada ya Diamond Platnumz ni kuwadharau Wasanii wa Kenya. Willy Paul anadai kuwa kwa mujibu wa ratiba yeye alipaswa kumtangulia Diamond, na pia anadai ratiba ilibadilishwa na yeye kupangwa baada ya Diamond Platnumz jambo ambalo hakulitaka na kupelekea kuleta vurugu ya kugombania kupanda stejini.

Baada ya vurugu hizi vyanzo vinasema Meneja wa Diamond ambae ni Sallam SK alipiga simu na kutaka Msanii wake "Diamond" ahairishe show hiyo. Diamond na timu yake waliondoka eneo hilo mara moja na kwenda kuendelea na ratiba nyingine pale jijini Nairobi.

Willy Paul alipanda stejini, lakini hakuishia hapo alizua taharuki baada ya Dj kupiga wimbo wake wa "Mmh" ambao alimshirikisha Rayvanny. Baada ya wimbo huo kupigwa Willy Paul akamwambia DJ kwa ukali "Naomba uondoe hiyo Takataka" akimaanisha aache kipiga wimbo huo. Hii kauli ilionesha ni dharau kiasi gani Willy Paul alikuwa nayo kwa wasanii wa Tanzania.

Bado Willy Paul aliongea na media na kudai wasanii wa kenya wanadharauliwa hawapewi kipaumbele na pia amelalamika kuwa jina lake na picha yake kwenye bango la matangazo vimewekwa kwa udogo ukilinganisha na jina na picha ya Diamond, huku wasanii wengine kama Eric Omondi wakikazia kupitia machapisho yao ya Instagram kuwa wasanii wa Kenya wamekuwa wakidharaulika.

Leo hii meneja wa Diamond Platinumz "Sallam SK" aliandika kwenye post ya Instagram:

"Nadhani ifike mahali wasanii muwekeze bidii kwenye kazi, kufeki story sababu ya fame ya kulazimisha bifu ili kutrend haisaidii, Msanii aitwae Willy aseme ukweli alikuwa anabishana na mtoto wa kike ( Zuchu ) aliblock njia Zuchu asipande kwenye steji akisema alikuwepo tokea mwanzo hivyo anataka apande yeye, ilhali wakati zamu yake aliitwa apande kwenye stage aligoma na kusema hawezi kupanda yeye ni Headliner anataka Afunge show Mwisho, baada ya kuona wenzake wanapata shangwe akawa anforce kupanda kwenye Muda wa Zuchu na wala sio Diamond. Regarding why Diamond hajapanda is between us and organizer has nothing to do na msanii yoyote. Bless Up 🙏🏽"

Tamasha la Furaha City Festival lilibadilika na kuwa tukio lenye drama nyingi, likitoa sio tu burudani za kuvutia bali pia ushindani mkali. Wakati mgongano kati ya Willy Paul na Diamond Platnumz ulikuwa tayari umeweka hali mbaya, msanii wa rap wa Kenya, Khaligraph Jones, alichukua mambo hadi kiwango kingine kwa matamshi yake ya kibaguzi.

Akiwa jukwaani, Khaligraph alitangaza sio tu kwamba yeye ndiye msanii bora wa rap barani Afrika, bali pia alijitawaza kuwa msanii bora nchini Tanzania—mbele ya Diamond Platnumz, ambaye kwa muda mrefu amehesabiwa kuwa mfalme wa muziki wa Tanzania. Kauli hiyo ya kishujaa iliwashangaza mashabiki, huku minong’ono ya kutokuamini ikitawala umati.

Kana kwamba hiyo haitoshi, Khaligraph aliendeleza hali hiyo kwa kuimba wimbo wake wa diss unaojulikana kama "Bongo Flavour" dhidi ya marapa wa Tanzania, wimbo ambao alitoa miezi kadhaa iliyopita akiwatuhumu kwa “kusinzia kazini.”


MY TAKE:
Katika ukumbi huo wa burudani hapo jijini Nairobi wanekuwa wakiharikwa wasanii wengi kutoka Jamaica na Nigeria lakini hakujawahi kutokea vurugu ya namna hii, lakini baada ya wasanii wa Tanzania kutokea jana zikatokea vurugu hizo, na mpaka sasa mitandaoni wakenya wamesapoti kwa ukubwa kitendo cha vurugu alichokileta Willy Pau.

Huwezi kusikia hata kwa bahati mbaya Msanii au Mtanzania yoyote yule kutoa lugha za kibaguzi kama hizi kwa Majirani zetu Wakenya.

Wenzetu ile dhana ya kubaguana ipo kwenye damu zao,
Wao Kwa wao kutwa kubaguana kwa misingi ya Ukabila na mahali unapotoka.
Sasa baadhi yao kama huyu Mpuuzi anachochea hasira za Wakenya waone sisi ni Maadui zao!!

Huku kwetu Tanzania always tunawaona nyinyi ni ndugu zetu na tunawapenda sana.
Wanasiasa wetu wa Afrika Mashar
iki siku zote wanafikiria kuunganisha Mataifa yetu,
Lakini kijana mmoja wa hovyo kwa chuki zake binafsi anatoa lugha za kishamba shamba.
wakenya wabugi
 
Back
Top Bottom