Ujinga niliowahi kuufanya kulilia penzi la mchepuko

Ujinga niliowahi kuufanya kulilia penzi la mchepuko

Jack Daniel

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
2,912
Reaction score
12,904
Habari wanabodi ni matumaini yangu mu wazima

Kama ada wana MMU, vipo visa vingi tunafanyiana wanandoa hasa mtu kuumizwa na mapenzi na mtu mwingine ilhali mtu una mke/mume.

Iko hivi Kuna kipindi niliwahi kuteseka Sana na mchepuko Tena naamini hakunipenda ila alipenda pochi yangu tu.

Basi kuna siku ilikuwa ni ijumaa yaani weekend inaingia, nikampanga mapema kwamba leo lazima tutoke,naam tulikubaliana freshi wapi tutapata dinner na lodge itakuwa wapi.

Kumbuka Mimi nina mke, akiwa na mtoto wa miezi minne,

Basi muda Kama saa kumi na Moja jioni yule manzi alinipigia simu kwamba tuahirishe mpango wetu kwakuwa ana dharula,eti mama yake kapata ajali.

Nikamwambia basi anielekeze wapi walipo Kama ni hospital yoyote nifike nichangie hats matibabu, alikataa katakata akidai si jambo zuri mimi kwenda sehemu ambayo sijatambulishwa.

Akimaanisha Kama ni msaada basi nimfanyie muamala tu, bila hiyana nikampa laki na nusu ili mama yake atibiwe.

Kilichoniuma sasa,wakati natafuta kiwanja kingine ambacho huwa nawajoin washikaji zangu nikiwa Sina vyangu au Sina demu huwa na sizi pale,

Cha ajabu nilimkuta yule mwanamke kajaa tele yupo na kivulana fulani kikiwa kimemshikia mkoba huku wakipigana mabusu Kama mvua.

Hasira zililijaa,nikagonganisga meno kwa hasira, shukrani ziende kwa mchizi wangu James a .k.a Wiz khalifa kwa kunitoa ,nje na kunilazimisha nipande gari lako mpaka home

Wakati nafika home,sikuwa vizuri kichwani nikawa mkali Hadi kwa wife

Nakumbuka waifu alihoji nipatwa na nini mbona sipo sawa nilimjibu nyodo lakini pongezi ziende kwa Mdogo wangu James a.k.a Wizzy khalifa kwa kutunga uongo wa papo kwa papo Hadi wife akalainika

Kumbe wavuta bangi muda mwingine wana busara Sana[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Basi usiku kucha nililala na mawazo sana kuhusu yule manzi ila kilichoniuma zaidi na kunipa ujasiri ni haya maswali

1.hapa naumia kwa vitu vya kijinga, lakini si Nina mke?

2.halafu mke wangu hajajua nini kinaniumiza, he akijua kuwa ni masuala ya kijinga si nitahatarisha ndoa yangu na kuzidisha matatizo?

Nikajiona ni mjinga...

Nilimwangalia wife kwa huruma akiwa ananipa maneno yenye ushauri mzuri akinibembeleza kwamba Kama ni masuala ya wewe kuhofia kusimamishwa kazi utapata sehemu nyingine

Niliumia Sana,hasa kwakuwa kinachoninyima Raha ni kitu Cha kijinga

Basi Hali yangu ikawa shwari my wife akafurahi zaidi akijiona mshindi si anajua busara zake zimezaa matunda[emoji23][emoji23][emoji23]

Basi weekend ile nilitulia home tu nikipewa mapenzi Moto Moto na my wife

Nikamsahau kabisa nyang'au yule,halafu akanipigia simu nilichomjibu hatosahau,akaja mpaka ofisini lakini nilimuonesha ukatili hatosahau.

Ujumbe

Tuwapende wake zetu.
 
Sijui mwenzangu, ila mimi huwa sipendi tu mtu akiisaliti ndoa yake
Haya mambo ni magumu sana

2795695_images_2.jpeg
 
"Kuna wakati michepuko inazingua hadi unatamani kumsimulia mke/mume ili akufariji"

Nimeukumbuka tu huo msemo.
 
Back
Top Bottom