Mtaka Haki
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 492
- 149
Nimesikitika sana kuona kuwa katika maadui wakuu wa tangu kale
1. Ujinga
2. Umaskini
3. Maradhi
Kwa WANASIASA wa leo hao ndio marafiki wao wakuu katika kutimiza agenda zao na uovu wao.
1. UJINGA
Tunawekeza kwenye ujinga wa watu wetu. Kama sio ujinga wa watu wetu VIONGOZI wetu wasingethubutu kufanya na kusema tunayoyaona na kuyasikia. Hofu ya uelewa wa watu ingewaogopesha na kuwanyenyekesha. Huwezi kuona mahali duniani penye demokrasia ya kweli wananchi wakilazimishwa kufuata matakwa na vitisho vya watu wachache au kikundi cha watu wachache wanaoweza kubadilisha hata maamuzi ya wananchi. Huwezi kuona mahali ambapo Chombo cha wawakilishi wa wananchi kinafanyika mahali pa mipasho umbeya matusi bila hofu ya kuwajibishwa na waliokutuma.
Kila mahali ambapo elimu haikupewa kipaumbele tumeona ni mahali pazuri pa kupata UONGOZI hata kwa watu wasiokuwa waadilifu hawaogopi kwa kuwa wamewekeza kwenye ujinga wa watu.
Heshima kwa utawala wa sheria na uaminifu kwa KATIBA, KANUNI na taratibu zinapokiukwa bila heshima wala hofu ni ishara ya ujinga wetu.
2. UMASIKINI
Watu kwa umaskini wao wanarubuniwa kuuza utu wao na heshima yao. Wanalazimishwa na nguvu ya PESA kuwa wanafiki na kutokufuata dhamiri zao juu ya nani bora. Wakati wenzetu wengi wa nchi zilizoshinda masuala ya rushwa hutafuta pesa za kujitangaza na kueneza sera ili wakubalike sisi bado tunatafuta fedha za kuhonga watu wasiojua tunachoamini au kupanga kufanya. Badala ya kuunga mkono hoja wanaunga mkono aliyetoa pesa au kiasi cha pesa walichopokea bila kujali msimamo, UADILIFU na MISINGI anayosimamia mtoaji.
3. MARADHI
Haya yamegeuka kuwa mitaji ya wanasiasa wengi. Hatuboreshi lolote tunatumia maradhi ya watu wetu kuombea misaada bila kuwa na mpango wa DHATI toka moyoni wa kuyatokomeza.
UJINGA NA UMASKINI NA MARADHI NI MTAJI MKUU WA VIONGOZI WA KISIASA. Ni wakati wanasiasa waitendee HAKI dhamiri yao hata kama wataanguka kisiasa wakumbukwe kama Gorbashev na Fredrick De Clark waliofanya ya HAKI hata kama walikosa cheo.
HATUA GANI ZICHUKULIWE HAPA TANZANIA KUBADILISHA HALI HII.