Kwa sisi vijana tuliozaliwa miaka ya 1980+ nadhani kwenye siasa za nchi hii tutakuwa tumezifahidi sana kwa kujioneea na kuziishi pamoja na kuzisikiliza kwa makini na ukaribu zaidi ni siasa za wakati wa Rais Kikwete anawania nafasi ya kuingia IKULU.
Hapo tulipewa matumaini mengi sana hasa kwa sisi tunaoishi kwenye huu umasikini, kwani kwa mara ya kwanza swala la kila mtanzania kuwa na maisha bora tena kwa kasi na hali mpya liliongelewa sana na kuelezea mikakati na mipango ya jinsi tutakavyo jivua JOHO la umasikini.
Kufufua na kuanzisha ya viwanda, kuacha kuudha mazao ghafi, mikataba mibovu, rushwa, maji, afya (wazazi kujifungulia chini), ajira (hasa vijana) , michezo (hadi kushiriki kombe la dunia kwenye soka) yote haya tuliambiwa na kuaminishwa yanawezekana tuwape nafasi, na watanzania wakawapa.
Baada ya miaka kumi kupita nilitegemea leo watangaza nia wote kupitia CCM wangekuja na habari mpya ambazo nilitegemea nyingi zitakuwa zinaelezea watanzania tukiwa tayari kwenye maisha bora na sasa tunaelekea kwenye maisha ya juu zaidi.
Matokea yake kila kila mtu anakuja na lake, mara huyu anauchukia umasikini mwingine umasiki sijausoma nimeuishi na mwingine yeye ni mtoto wa masikini na wote wakiahadi kuotokomeza umasiki ambao wote hawataki kueleza kuwa kama chama kwanini wameshindwa swala hilo kwa miaka zaidi ya 35 ya CCM.
Zaidi, wote ukiwasikiliza kwa makini wanakiri kuwa nchi ipo kwenye hali tete kiuchumi ila wenyewe watakuja kutupeleka nchi ya ahadi huku wakisema kwa sasa Rushwa imezidii na watapambana nayo kwa vitendo, mikataba mibovu nitatizo, elimu mbovu, umasikini umezidiii, Ajira ni BOMUU, afya ni tatizo, hakuna uwajibikaji kwa watendaji na mengine mengi.
Sasa nadhani huu ndio wakati wa vijana wa leo tujiulize na CCM watueleze ni kipi kimewafanya 35 hadi sasa hawaongelei swala la watanzania kuwa kwenye hali bora na matokeo yake UMASIKI wetu umeendelea kuwa ndio mtoko kwa mara nyingine tena.
Au tuamni kuwa UMASIKINI wetu ndio mtaji wenu?