Mtaka Haki
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 492
- 149
- Thread starter
- #81
Ugonjwa wa kupenda tiba yake lazima utendwe vibaya sana ndio waweza kushituka, wakati mwingine mapenzi hayo hutia ganzi kiasi kwamba usione wala usisikie. Naipenda TZ lakini siupendi utawala uliopo kwa upendo ulionao FaizaFoxy. Wewe umeamua kuweka pamba masikioni mwako na kuvaa miwani ya mbao. Kwamba huuoni uongonzi mbaya wa serikali yetu mpaka sasa. Just to name a few
1. Wizi wa fedha za uma (EPA, ESCROW, RADA n.k.) unazorotesha maendeleo.
2. Maamuzi hafifu yanapoteza rasilimali za nchi. Leo nimemsikia mh. Kafulila akielezea uamuzi wa serikali kujenga bandari ya kisasa Bagamoyo bila kufanya economic analysis yenye kuleta tija
3. Kushindwa kushughulikia uhalifu, waTZ wanauawawa kama kunguni
4. Mikataba yenye kunufaisha watu wachache (au wewe umo katika kundi hili) bila kujali maslahi ya wananchi
Hao mitume sio sehemu yao katika mjadala huu. Kubali kiungwana tubadilishe uongozi safari hii (hata kama atakaye ondoka ni mjomba wako), achana na mambo ya zimwi likujualo.
Nadhani ameajiriwa kwa ajili ya kupinga tu chochote.