Ujinga, Umaskini na Maradhi ni mtaji mkuu wa wanasiasa wa Tanzania

Ujinga, Umaskini na Maradhi ni mtaji mkuu wa wanasiasa wa Tanzania

Kama mwanasiasa mkubwa kabisa anapanda jukwaani na kuwauliza Wananchi "Hivi katiba itawajengea barabara?". Wananchi wanajibu "Hapana". Yeye badala ya kusikitika, anafurahi; unadhani kuna kazi tena hapo. Ujinga wetu ndiyo mtaji wao.

Wanatubagua na kutukebehi na sisi hatujitambui. Sasa tunaingia katika mtego, vijana sasa tunawaza "ukipata deal usiliache", piga pesa utoke. Tunasahau kuwa utapiga deal, utakuwa "Rich" lakini sio "Wealthy". Utapiga pesa lakini tutakaa wote foleni, ndugu zako wataendelea kupata elimu duni, na mbaya zaidi utachanganyiwa madawa hospitali (kwa maana wafamasia hawapiti mawodini) na hizo hospitali zitaendelea kukosa vifaa nk.

Tumeingia mwaka wa uchaguzi, vijana huwa tunakosea hapa. Tunaumia mno tunapoona mambo hayaendi sawa, lakini ushiriki wetu katika uchaguzi umekuwa janga tupu. Tuna mengi ya kufanya hasa kipindi hiki kujinasua hapa tulipo. [Akili kukichwa]
 
Iko hivi.. Mlinzi tuliyempa dhamana ya kulinda mali zetu anashirikiana na wezi kutuibia.. CCM ndiyo impewa dhamana ya kulinda rasilimali zetu na kukusanya kodi na kutuletea maendeleo.. Sasa kwa kuwa iko dhahiri shahiri Mlinzi huyu anashikiriana na wezi kutuibia dawa ni moja tu.. Kumfukuza kazi na kumpeleka mahakamani..

TOA CCM MADARAKANI TANZANIA IPONE

Mkuu naunga Hoja! Mijizi mikubwa halafu inajisifu mchan kweupe bila aibu wala woga
 
Iko hivi.. Mlinzi tuliyempa dhamana ya kulinda mali zetu anashirikiana na wezi kutuibia.. CCM ndiyo impewa dhamana ya kulinda rasilimali zetu na kukusanya kodi na kutuletea maendeleo.. Sasa kwa kuwa iko dhahiri shahiri Mlinzi huyu anashikiriana na wezi kutuibia dawa ni moja tu.. Kumfukuza kazi na kumpeleka mahakamani..

TOA CCM MADARAKANI TANZANIA IPONE

Ulishawahi kuona Mchagga anapewa kazi ya ulinzi?
 
Vipi kuhusu maazimio ya kamati kuu ya ccm.

Nakubaliana na FAIZA FOXY juu ya umuhimu ya juhudi binafsi. Lakini kama juhudi binafsi zinatosha viongozi wanachaguliwa kwa kazi gani? Siamini kuwa tunashabikia kuendelea kwa ujinga na umaskini na maradhi. Tatizo ni kubwa sana kama hata wanaowekeza kwenye ujinga na umaskini wetu tunawashabikia.
 
Hatua zinahusu nini?

Fanya bidii yako binafsi kushindana na yote hayo yatakuondokea. Unangoja mtu akuchukulie hatua kwa ujinga wako?

Nyie ndiyo mnawaponza wasiojuwa Kiswahili vizuri, wanaanza kupiga hatua kutoa Geita sijui wapi huko wanajuwa wakifika Ikulu kila kitu safi, wakaishia rumande.

Nakubaliana na wewe FAIZA FOXY juu ya umuhimu ya juhudi binafsi. Lakini kama juhudi binafsi zinatosha viongozi wanachaguliwa kwa kazi gani? Siamini kuwa tunashabikia kuendelea kwa ujinga na umaskini na maradhi. Tatizo ni kubwa sana kama hata wanaowekeza kwenye ujinga na umaskini wetu tunawashabikia.
 
Mtaji wa ccm, nape aliwauliza watu tanga eti mnataka maji au katiba, wale watu wakajibu majiiiiii....! Mnataka barabara au katiba, wakajibu barabaraaa..! Umeme au katiba, umemeeee! Katiba itawasaidia nini nyie watu hakunaaaa.....! Kama si uenda wazimu ni nini?
so sad!!!
Nini kifanyike?
 
Nakubaliana na wewe FAIZA FOXY juu ya umuhimu ya juhudi binafsi. Lakini kama juhudi binafsi zinatosha viongozi wanachaguliwa kwa kazi gani? Siamini kuwa tunashabikia kuendelea kwa ujinga na umaskini na maradhi. Tatizo ni kubwa sana kama hata wanaowekeza kwenye ujinga na umaskini wetu tunawashabikia.

Dunia hii haitaishiwa na matatizo hata uletewe mtume mwingine na si kiongozi tu wa kawaida, ikiwa wewe mwenyewe unashindwa kujiongoza usitegemee kuwa kiongozi atakuja kukushika mkono akuongoze.

Hivi, kiongozi yupi kakuongoza vibaya na kwa lipi? maana tunaweza kubishana pengine kiongozi wako alikuja akakuongoza vibaya na sisi hatujuwi, tuanzie hapo.
 
​Nimesikitika sana kuona kuwa katika maadui wakuu wa tangu kale 1. Ujinga
2. Umaskini
3. Maradhi
Kwa WANASIASA wa leo hao ndio marafiki wao wakuu katika kutimiza agenda zao na uovu wao.


1. UJINGA.
Tunawekeza kwenye ujinga wa watu wetu. Kama sio ujinga wa watu wetu VIONGOZI wetu wasingethubutu kufanya na kusema tunayoyaona na kuyasikia. Hofu ya uelewa wa watu ingewaogopesha na kuwanyenyekesha. Huwezi kuona mahali duniani penye demokrasia ya kweli wananchi wakilazimishwa kufuata matakwa na vitisho vya watu wachache au kikundi cha watu wachache wanaoweza kubadilisha hata maamuzi ya wananchi. Huwezi kuona mahali ambapo Chombo cha wawakilishi wa wananchi kinafanyika mahali pa mipasho umbeya matusi bila hofu ya kuwajibishwa na waliokutuma.
Kila mahali ambapo elimu haikupewa kipaumbele tumeona ni mahali pazuri pa kupata UONGOZI hata kwa watu wasiokuwa waadilifu hawaogopi kwa kuwa wamewekeza kwenye ujinga wa watu.


Heshima kwa utawala wa sheria na uaminifu kwa KATIBA, KANUNI na taratibu zinapokiukwa bila heshima wala hofu ni ishara ya ujinga wetu.


2. UMASIKINI
Watu kwa umaskini wao wanarubuniwa kuuza utu wao na heshima yao. Wanalazimishwa na nguvu ya PESA kuwa wanafiki na kutokufuata dhamiri zao juu ya nani bora. Wakati wenzetu wengi wa nchi zilizoshinda masuala ya rushwa hutafuta pesa za kujitangaza na kueneza sera ili wakubalike sisi bado tunatafuta fedha za kuhonga watu wasiojua tunachoamini au kupanga kufanya. Badala ya kuunga mkono hoja wanaunga mkono aliyetoa pesa au kiasi cha pesa walichopokea bila kujali msimamo, UADILIFU na MISINGI anayosimamia mtoaji.


3. MARADHI
Haya yamegeuka kuwa mitaji ya wanasiasa wengi. Hatuboreshi lolote tunatumia maradhi ya watu wetu kuombea misaada bila kuwa na mpango wa DHATI toka moyoni wa kuyatokomeza.


UJINGA NA UMASKINI NA MARADHI NI MTAJI MKUU WA VIONGOZI WA KISIASA. Ni wakati wanasiasa waitendee HAKI dhamiri yao hata kama wataanguka kisiasa wakumbukwe kama Gorbashev na Fredrick De Clark waliofanya ya HAKI hata kama walikosa cheo.


HATUA GANI ZICHUKULIWE HAPA TANZANIA KUBADILISHA HALI HII.

Nikweli Ujinga, Umasikini na Maradhi ni mitaji kwa wanasiasa hasa wanaCCM, ila kwanza ni lazima tu utokomeza Mfumo kipofu na wa kutofikiri uliopo ili kuodokana na majanga haya.

Just imagine kiongozi anawapa wananchi rushwa ya Ubwabwa, sukari, Buku 10 au 5, Kofia, Khanga n.k.,ili apate kura zawananchi nao wananchi pasipo kujua huduma waliyopewa ni muda mfupi tu.

Ndiyo maana ukitaka Kumtawala Mwanadamu yeyote yule Daima,Mpe Chakula na Umnyime Elimu. Na ndicho kinacho fanyika na Serikali yetu iliyopo madarakani kwa kuua Elimu Bora na sasa ni Bora Elimu.

Haiwezekani mtoto wa Darasa la 7 kufaulu pasipo kujua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu. Zaidi kuthibitisha hili ukiona mtoto aliye Felli Karne hii, uju hata Kuchunga mifugi hawezi.

Viongozi wetu waliopo madarakani hawana Hofu ya Mungu, hakika Ngamia atapita ktk tundu la sindano ila hawa CCM mwiko.
 
Ujinga, umasikini, na maradhi ndio mtaji wa wanasiasa,,,, ni kweli kabisa mama uko sahihi,,

Ujinga wawatanzania wengi umesababishwa na wengi kutoelimika, mfumo mzima haumfundishi mtu kujitambua, mfumo wa elimu unafundisha watu uoga na kutokujiamini kwa kifupi elimu ni duni na wengine hata hiyo duni hawajaipata sasa sijui uelevu hapa utatoka wapi... Wengi ambao ni waelevu na wanajitambua ni karama ambayo Mungu amewapa na wengine elimu yao hawakuipata hapa.... Elimu ahera na dunia zote humsaidia mtu kutokuwa mjinga, kama zote hukuzipata au hata moja huna au umezipata lakini sio sahihi kwa maana ya duni lazima uwe mjinga na mpumbavu,
NI NANI AMESABABISHA ASILIMIA 70%-90% YA WATZ KUWA WAJINGA JIBU NI WATAWALA AMBAO NI CCM WAMELETA UJINGA KWA KUTOWAPA WATU ELIMU SAHIHI NA KUWANYIMA KABISA ELIMU WENGINE mfano waisilamu/Muslim wamenyimwa elimu kwa kubaguliwa, nani muhusika jibu CCM. tunaona hata historia ya TZ imepotoshwa na hii ndio tunaita elimu duni je nani kapotosha??? Jibu ni CCM na JK NYERERE.

UMASIKINI: kwa umasikini duniani kote tanzania inajulikana ni masikini,, je nini maana ya umasikini??? na kwa nini sisi masikini?? Watanzania wengi ni masikini wa kipato na taifa lenyewe latanzania ni masikini kwa kipato,, lakini je umasikini wa kipato kwa taifa nani kauleta??? Umasikini wa mtu mmojammoja unaweza kwa kiasi fulani ukasababishwa na mtu mwenyewe au ukawa umesababishwa na watawala mfano walimu watanzania umasikini wao huletwa na watawala kwani malipo yao hayalingani na maisha halisi yalivyo na wakati mwingine hawalipwi kwa wakati... Kwa mji kama dar ili useme angalau familia imekula vizuri inabidi uache walau 10000 ambayo kwa mwezi ni 300000/= bado mambo mengine lakini watu hulipwa mishahara mpaka 200000/= kwa mwezi na wana familia... Mifumuko ya bei hailingani na vipato vya watu je nani ni mdhibiti wa haya??? Dada/mama ukifanya speacial research tanzania isiyokuwa na majungu au chuki utaona hali ya umasikini ni kubwa, naijua tanzania 85% physically nimefika maeneo mengi hali ya umasikini ni mbaya sana... Na sababu ya umasikini ni watawala ambao wako toka 1961, wameshindwa kupeleka maji,umeme na huduma muhimu kwa hawa watu je kwa nini wasiwe masikini??? Kama ulishawanyima elimu na ukawapa elimu duni watu wako kwa nini wengi wasiwe masikini??

MARADHI:: hospitali hazina dawa, huduma haziko sawa,madaktari hawalipwi stahiki kulinganana na risk ya kazi zao na mazingira ya kazi sio mazuri( vitendea kazi haba)... Miundo mbinu mibovu kiasi kwamba mazalia ya mbu ni mengi... Yale magonjwa ambayo tunaweza kuyadhibiti yasiwepo tumeshindwa mfano maleria, ukimwi, vichocho, kipindupindu,TB nk, kama Rais amepewa neti za mbu baada ya kuomba mbinu za kupambana na maleria na kuyatokomeza hapa sijui tumlaumu nani???
Gharama za matibabu na kujikinga na haya maradhi zimekuwa kubwa na kipato chenyewe ndio hicho cha mwalimu!!! Inawezekana kabisa zaidi ya 68% ya watanzania hawapati lishe bora sasa sijui maradhi watayaepuka vipi??? Akina mama wajawazito wanajifungua katika hali ngumu na mwisho wasiku wanaishia kupata maradhi ndani ya miili yao!! Vyakula visivyo na ubora vinaingia kiholela na mamlaka husika zinaangalia ( au hujui mafuta ya transfoma hukaangia chips TZ??) Elimu haitolewi kwa watu na mashuleni namna ya kupata na kula chakula bora kama Mungu alivyotuumba waafrika mwisho wasiku watu wameiga ya wazungu na vyakula vya kizungu ambavyo wao hula kama walivyoumbwa...

DADA/MAMA FAIZAFOX HAYO YOTE ULIYOYASEMA 98% YAMECHANGIWA NA WATAWALA KWA MAKUSUDI AU KUTOKUWA NA UWEZO WA UTAWALA,,, KAZI YA WATAWALA NI KUHAKIKISHA WATU WAKE WANAKUWA NA ELIMU BORA NA WAELIMIKE,, WATU WAKE WAWE NA KIPATO KIZURI KWA KUTENGENEZA MAZINGIRA YA WAO KUTAFUTA NA MAISHA NA KUFANYA KAZI, KAZI YA WATAWALA NI KULINDA AFYA ZA WATU WAKE ILI UWE NA WATU WALIO FITI KWA AJILI YA UZALISHAJI...

KAMA HAUPO TANZANIA BASI KINACHOENDELEA NI THE SIGN OF THE FAILED STATE, NATUNAHITAJI MKOMBOZI WAKWELI NA SI CCM,,, NAONGEA KAMA MLIPA KODI NA NALIPA 2000000/=
 
Dunia hii haitaishiwa na matatizo hata uletewe mtume mwingine na si kiongozi tu wa kawaida, ikiwa wewe mwenyewe unashindwa kujiongoza usitegemee kuwa kiongozi atakuja kukushika mkono akuongeze.

Hivi, kiongozi kakuongoza vibaya na kwa lipi? maana tunaweza kubishana pengine kiongozi wako alikuja akakuongoza vibaya na sisi hatujuwi, tuanzie hapo.

Matatizo ya kutengeneza na ya kujitakia LAZIMA YAKOMESHWE!
 
Hatua zinahusu nini?

Fanya bidii yako binafsi kushindana na yote hayo yatakuondokea. Unangoja mtu akuchukulie hatua kwa ujinga wako?

Nyie ndiyo mnawaponza wasiojuwa Kiswahili vizuri, wanaanza kupiga hatua kutoa Geita sijui wapi huko wanajuwa wakifika Ikulu kila kitu safi, wakaishia rumande.

Bidii ya mtu mmoja mmoja humaliza matatizo yake binafsi, tunamaanisha kuwapa lishe bora, kuwapa elimu na maradhi bora watu wa familia husika... Elimu bora ni shule na vyuo bora...... shule na vyuo bora sio mali ya muhusika ila ni mali ya Serikali na taasisi fulani..... na ukumbuke huyu mtu hulipa kodi nyingi sana ili apatiwe zile huduma ambazo ni public kwa gharama nafuu na kwa misingi ya taifa husika ili lijengwe na watu husika. Kama huyu mtu anatakiwa ajibidiishe na afanye kila kitu mwenyewe basi hakuna haja ya kuwa na serikali wala watu kukatwa kodi kwani hapa kila mtu atajibidiisha mwenyewe na kuwa na serikali yake ili ajilinde, aiishi kwenye nyumba bora akiwa na solar yake au generator yake full time, huyu mtu atachimba kisima chake mwenyewe na kutreate maji yake kwa sulphur/mawe/shabu, huyu mtu atanunua gari la 4*4 ili apite kwenye barabara mbovu ( wazungu watatuletea tu magari na meli zao za michangani kwani tutakuwa hatuna bandari)... kama wanachukua kodi zetu na wanaweka kodi kwenye bidhaa na tunalipa, wanakusanya kodi kwenye viwanda na wanataka tujibidiishe ili tumudu zile public service ambazo ni makukumu yao basi wasichukuwe kodi zetu, kila kitu kisiwe na kodi na tusiwe na serikali ili kila mtu ajiongoze mwenyewe...

Mwananchi anamajukumu yake na Serikali ina majukumu yake,,, kazi ya mwananchi ni kufanya kazi, kulipa kodi na kuangalia familia yake na yeye mwenyewe.. kazi ya Serikali ni kutawala watu wote, kukusanya kodi na kuzifanyia kazi stahiki kwa maendeleo ya nchi,,, sasa kama unataka mwananchi kufanya kazi ya serikali mfano kujenga maabara basi haina haja ya kuwa na serikali....

Mwananchi anaweza kujibidiisha akawa na hela/utajiri na akalipa kodi lakini akiugua hospitali hazina madawa, shule hazitoi elimu bora na maeneo mengine hazipo, umeme hauwaki, barabara hazipitiki na maji hakuna sasa hapo nani atakuwa ameshindwa kazi SERIKALI /MWANANCHI...

DADA FAIZAFOX HAMNA NAMNA YAKUITOA CCM KATIKA UMASIKINI WA TANZANIA NA WATANZANIA KWA UJUMLA MAANA WANAKUSANYA KODI NYINGI KILA MAHALI,, MISAADA KWA WAHISANI, KODI KWENYE MADINI HALAFU WANASEMA WATU WAJIBIDIISHE WAKATI 85% YA KODI INATOKA KWA WANANCHI.....SASA SIJUI WANGEKUWA HAWAJIBIDIISHI HIYO KODI INGETOKA WAPI???

HIVI DADA UPO TANZANIA KWELI HAPA NA UNAONA YANAYOTOKEA PHYSICALLY AU UNAONGEA TU NA HUIJUI HALI HALISI YA HUKO NAMANYELE, ENDASAKI, ENDAGAW, UJIJI, MASUMBWE, KATORO, NK??
 
Back
Top Bottom