Ujio wa Aziz Ki una maana gani kwa Fei Toto?

Ujio wa Aziz Ki una maana gani kwa Fei Toto?

Kiungonguli

Member
Joined
Jul 26, 2015
Posts
60
Reaction score
100
Stephane Aziz Ki ni jina lililotamkwa mara nyingi mno midomoni mwa mashabiki wa SIMBA na YANGA kwa takribani wiki nane sasa huku kila shabiki wa timu hizi akitamani huyu bwa mdogo acheze kwenye timu yake pendwa.
Hatimaye sasa ni rasmi AZIZ KI ni mali ya wananchi na ameshatambuliswa kwa mbwembwe zote anazostahili mchezaji mkubwa.Lakini ujio wake ni furaha kwa washabiki wa Yanga popote walipo lakini sidhani kama baadhi ya wachezaji wanocheza katika eneo ambalo huyu mwamba anacheza wamepokeaje ujio wake.
Aziz KI anacheza vizuri akiwa kama namba 10 au akitokea pembeni upande wa kulia,pia anaweza kucheza kama FALSE 9 pia,lakini mwalimu NABI bila shaka atataka kumtumia huyu mwamba kama namba 10 nyuma ya MAYELE eneo ambalo limemn'garisha sana kiungo fundi mzawa FEISAL SALUM..
Fei toto amekuwa na msimu mzuri hivi karibuni akitumika kama namba 10 nafasi ambayo Mwalimu Nabi alimpangua SAIDO ntibanzokisa na kumpeleka pembeni na kumwachia ZANZIBAR FINEST ajidai.
Wakati wa PAPA MWINYI ZAHERA eneo hilo alipewa IBRAHIM AJIB MIGOMBA na alin'gara sana huku FEI akicheza kama kiungo wa chini eneo ambalo mashabiki wake tunaona kama linamfifisha sana maana anakuwa mbali na lango.
Kwa sasa kuna ujio wa BIRIGIMANA na uwepo wa BABU KAJU katika eneo hilo sambamba na fundi AUCHO,nadhani BANGALA atacheza kama beki zaidi msimu ujao.
Je FEI TOTO atarudishwa kucheza chini abanane na akina SURE BOY,Bigirimana na Aucho?Au AZIZI KI atachezeshwa pembeni abanane na akina MOLOKO,MORISSON,YACOUBA,NKANE na KAMBOLE huku FEI akibaki kwenye eneo lake la kujidai?
Tusubiri tuone mwalimu NABI atafanyaje...
 
Fei mie namuona ni namba 8 zaidi kuliko 10, kama mwalimu akiamua kucheza 4 1 2 3, akiwa na double CM hapo atang'ara zaidi wakati babu kaju anasambaza upendo, yeye anawamaliza wapinzani kwa zile movements zake, dribbling na zile skills zake.

Huu ndio wakati sahihi fei aende nje nae akaimbwe huko, mpira anaujua, sijui shida ni nini haswa.
 
Nikiweka Usimba wangu pembeni naamini Feitoto ni panga pangua kwa Yanga huwezi kumtoa kwenye first eleven.

Naamini pia Feitoto ni mchezaji mzuri zaidi hata ya Ki Aziz na Kambole. Ukiniambia nikutajie wachezaji bora Yanga msimu ulioisha.

3.Mayele
2. Feitoto
1. Bangala
 
Fei mie namuona ni namba 8 zaidi kuliko 10, kama mwalimu akiamua kucheza 4 1 2 3, akiwa na double CM hapo atang'ara zaidi wakati babu kaju anasambaza upendo, yeye anawamaliza wapinzani kwa zile movements zake, dribbling na zile skills zake.

Huu ndio wakati sahihi fei aende nje nae akaimbwe huko, mpira anaujua, sijui shida ni nini haswa.
Fei huyu huyu? Hata Tp Mazembe hawawezi kumchukua, labda arudi kwao KMKM. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Aziz Ki asubiri tu kupigwa misumari na wachezaji wazawa wa utopwinyo
 
Hapo ndo patamu sasa, alieko nje ntu, alieko ndani ntu. Anatoka ntu anaingia ntu. Ile kumtegemea mtu mmoja sasa basi. Maana ilkua akiumia homa inaibuka. Na kulr yulr jamaa akienda kwao harudi mpaka apigiwe magoti sasa namba yake wahuni wanakiwasha.
 
Nabi atakuwa ana switch mifumo kwa kuingiza wachezaji wawili au mmoja anaweza akacheza na back 3 .5.2 au 3:6:1 hapa anacheza bila winga maana yake anaingiza viungo 6 akimtoa kiungo mmoja anaingiza winga mfumo unabadirika kbs . Au anaingiza striker anatoka kiungo

Anaweza cheza na 4:1:3:1 au 4:1:2:2 au 4:2:2:1

Anasoma TU mchezo ndiyo maana kaleta kocha wa kusoma wapinzani .

Na mtaalam wa lishe

Tuiunge Yanga gonna be giant over the world
 
Fei toto zaidi ya mashuti yake hana kipya,mashuti hata mi naweza kupiga,mpira ni zaidi ya mashuti ,fei toto na ndemla ni walewale
Huwezi mlinganisha fei na ndemla. Ujue TU fei mpka Sasa akienda Simba anaingia Moja kwa Moja kwenye 1st eleven utofuti wa fei ni kuwa multi-purpose anakaba, anaposess , dribbling, holding, anapiga mashuti , ndemla anaposess mpira na kupiga mashuti

Fei Yuko kiwango cha juu Sana
 
Huwezi mlinganisha fei na ndemla. Ujue TU fei mpka Sasa akienda Simba anaingia Moja kwa Moja kwenye 1st eleven utofuti wa fei ni kuwa multi-purpose anakaba, anaposess , dribbling, holding, anapiga mashuti , ndemla anaposess mpira na kupiga mashuti

Fei Yuko kiwango cha juu Sana
Simba hachezi yule atacheza namba ya nani?hana akili anatumia nguvu tu,kuna mechi huwa anapotea mpaka anatia huruma,hana consistence
 
Niliwahi kuomba nabi afukuzwe tupate kocha ambaye atakuwa jasiri kumuweka feitoto benchi ili namba 10 acheze saido, kiukweli feitoto ni chanzo cha yanga kukosa mabao, hawezi kabisa kucheza kama namba 10. Sehem ya kushoot anapasia sehemu ya kupasia anashoot. Angekuwa mchezaji mzuri angeshaonwa na kuhitajika nje.
 
Back
Top Bottom