Red black
JF-Expert Member
- Nov 29, 2019
- 18,719
- 60,636
hii inabidi pia tz ipewe
==========
Rwanda imejumuishwa miongoni mwa Mataifa 12 mapya yatakayofaidika na ufadhili wa Serikali ya Marekani unaolenga kuongeza upatikanaji wa dawa ya sindano ya kuzuia maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU), dawa inayojulikana kama Lenacapavir.
Ufadhili huo unatekelezwa kupitia ushirikiano kati ya Marekani na Global Fund, ambapo zaidi ya Watu milioni moja duniani wanatarajiwa kunufaika na upatikanaji wa dawa hiyo katika hatua hii mpya.
Katika mpango wa awali, Marekani tayari ilikuwa imewezesha utoaji wa dawa hiyo kwa zaidi ya Watu milioni mbili katika Mataifa tisa, huku ufadhili mpya ukiongeza Nchi nyingine 12 zikiwemo Rwanda, Morocco, Thailand, Fiji na Jamhuri ya Dominica, hatua inayolenga kupanua wigo wa mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya VVU.
Hata hivyo, Wataalamu wa afya wanasema Lenacapavir, inayotolewa kwa njia ya sindano mara mbili kwa mwaka, imeonesha ufanisi mkubwa kwa uwezo wa kuzuia maambukizi ya VVU kwa kiwango cha hadi asilimia 99.9, jambo linaloipa matumaini makubwa dunia katika juhudi za kudhibiti ugonjwa huo
Hatua hiyo inaonekana kuwa sehemu ya mkakati mpana wa kimataifa wa kupunguza kasi ya maambukizi mapya ya VVU, huku Nchi zinazonufaika zikitarajiwa kuanza utekelezaji wa mpango huo katika kipindi kijacho kwa lengo la kuimarisha afya za jamii zao kwa muda mrefu.