KERO Ujio wa DP World mbona haujatupunguzia kero ndogondogo Wafanyakazi wa Bandarini?

KERO Ujio wa DP World mbona haujatupunguzia kero ndogondogo Wafanyakazi wa Bandarini?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Huku Bandarini tangu DP World wamekuja mambo yamekuwa magumu kwa Wafanyakazi, hatuna over time.

Pia wafanyakazi wengi wamehamishwa, yaani tafrani tupu, kubwa zaidi ni kuwa hatulipwi kwa wakati, mfano sasa hivi tulipaswa kupewa pesa zetu za rent tangu June mpaka leo tunaitafuta August 2025 bado hatujalipwa, hali hiyo inasababisha wafanyakazi wengi tumekopa mpaka basi.

Hata wale Askari na Wajeda nao hawajalipwa posho zao tangu mwezi wa tano 2025 mpaka leo. Naomba Serikali Kuu isikie hoja yetu ili tulipwe, mtaani kugumu tumekopa saana.
 
Huu dp world Kuna mtanzania mmoja amejitengenezea mrija wa pesa unadanganywa kuwa ni muwekezaji kumbe ni geresha tu
 
Hivi hizi nafasi walizotoa mwishoni mwa mwezi wa sita hazita husisha watu kupangiwa bandari ya dar es salaam ? maana siinamilikiwa na dp world , naona watapelekwa ports nyingine au
 
Back
Top Bottom