Wakati Kampuni ya Mabasi ya Shabiby Line ikiwa kwenye maandalizi ya kuanza safari zake za Dar -Tanga, Tanga-Dar kila siku, tayari baadhi ya wamiliki wa mabasi wenyeji wameanza 'kukuna vichwa' wakipanga mikakati ya kuongeza mabasi ya kisasa ili kumudu ushindani.
Habari kutoka mtandao mmoja wa mabasi Tanzania, juzi uliandika habari ikiitaja kampuni moja ya mabasi inayotamba kwa sasa kwa njia Tanga kwamba imetia 'oda' kuingiza mabasi mapya YuTong- 14 na KingLong matoleo ya mapya ili kuyaingiza barabarani.
Mtandao huo ukaenda mbali zaidi kwa kutoa picha ya basi aina ya Yutong 14 likiwa bandarini Dar na kusema kuwa, ni mfano wa Shuttle Bus kwa ajili ya kuchukua abiria Tanga mjini kuwapeleka Stendi Kuu (Kange) kwa safari za Dar.
Katika kumalizia taarifa hiyo kutoka kwenye mtandao huo, ukaandika; Waliochokoza Tanga wenyweji siyo wanyonge!!!
Hata hivyo, vuguvugu la kuanzishwa kwa safari ya mabasi ya Shabiby Line limepamba moto jijini Tanga wangi wakisubiria kwa shauku kwa madai kuwa, huduma ya mabasi hayo ni ya uhakika.
Nje ya ofisi za Shabiby zinazokarabatiwa Barabara 13, Tanga watu wamekuwa wakifika kutaka kujua kama safari zimeanza.
Mfanyakazi mmoja wa kwenye mabasi hayo amesema safari rasmi zitaanza baada ya siku 11 zijazo huku maandalizi yote yakitamatika.
Amesema mabasi yote ya Shabiby Line yatakayoanza safari mpya kamwe hayajawahi kuwepo kwenye njia ya Dar-Tanga na Tanga-Dar kutokana na ubora na usasa wake kuanzia injini, mwonekano wa basi nje na ndani na wahudumu wenye mvuto.
Aliongeza kuwa, safari zitakapoanza mabasi yatakuwa yakipishana dakika 180 kutoka basi litakaloondoka na litakalofuata kuanzia asubuhi hadi usiku.
Mfanyakazi huyo alisema kwa wafanyabiashara wa Tanga ambao ratiba zao zitawataka kufika Dar na kurudi Tanga siku hiyohiyo basi Shabiby Line ndiyo usafiri sahihi.