Suala la ulinzi na usalama wa nchi yetu ni jukumu letu lakini pia kama nchi sisi siyo kisiwa tunao washirika wetu tunaosaidiana katika hilo.
Ujio wa Makamo wa Rais wa Marekani suala la ulinzi na usalama wake lipo mikononi mwa Serikali ya Tanzania lakini pia wakishirikiana na nchi mgeni siku hiyo,kila mahali patapohitajika ulinzi kwa ajili ya ugeni huo basi naamini Askari wetu shupavu kwa kushirikiana na wa Marekani watafanyakazi bega kwa bega na hii ni kama ilivyokuwa hata alipokuja Obama na Bush.
Haipo nchi yoyote ile Duniani itaacha Kiongozi wake anapokuwa ziarani nje ya nchi kumlinda,hata aje Rais wa Somalia hapa bado walinzi wake watamlinda kwa kuwa itifaki inaruhusu hilo pia.