Pre GE2025 Ujio wa Rais Samia Suluhu Hassan: Hadi sasa sijaona dalili yoyote ya utashi wa kuwepo kwa maridhiano ya kisiasa nchini

Pre GE2025 Ujio wa Rais Samia Suluhu Hassan: Hadi sasa sijaona dalili yoyote ya utashi wa kuwepo kwa maridhiano ya kisiasa nchini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

M-mbabe

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2009
Posts
13,203
Reaction score
23,027
Chini ya Hayati Magufuli, tumeshuhudia jamii ya Watanzania ikiwa imegawanyika pasu-pasu kwa misingi ya itikadi kinzani za vyama vya siasa. Mgawanyiko wa jinsi hii haujawahi kutokea kwenye awamu yoyote ya urais huko miaka ya nyuma - ulikuwa mgawanyiko uliosheheni kuhasimiana kiasi cha kufikia watu kutamani kutoana roho, kupotezana, kutekana, kubambikiana kesi za uonevu, nk.

Katika kipindi hicho hicho tumeshuhudia sheria nyingi kandamizi zikitungwa zikiwa zimelenga kuudhoofisha upinzani wa aina yoyote dhidi ya serekali ya JPM.

Nchi imejikuta katika mtanziko huu mkubwa kufuatia mtazamo wa JPM alipokuwa anaingia madarakani mwaka 2015 alipoweka azma yake bayana kuwa lazima vyama vya upinzani viwe vimeshakufa kabisa ifikapo mwaka 2020. Katika kuhakikisha azma hii chini ya utawala wake inafikiwa, tulishuhudia kati ya 2015 hadi 2020 jinsi ambavyo vyama vya upinzani vilivyokumbwa na sulba ya kiama. Hakuna haja ya kurudia yaliyojiri kwani wote humu tunayajua.

Dhamira hiyo ovu hata hivyo haikufanikiwa kwani vyama vya upinzani vikaimarika zaidi ilipofikia mwaka 2020 kuliko hata vilivyokuwa mwaka 2015. Hivyo chama tawala kikabakiwa na silaha moja pekee - kufanya uovu mkubwa wa karne dhidi ya demokrasia October 2020!

Sisi tunaoamini tunajua Mungu ni Mungu wa haki, huwapatiliza wale wote wawafanyiao udhalimu waja wake. Mungu ni fundi. Hutenda kwa majira yake.

Sasa amekuja mama Samia. Wengi tukimtegemea kuwa ni a new hope of fresh air. Watanzania wanamuangalia yeye kama tumaini jipya pekee la kuleta matengenezo katika nchi yetu.

Hata hivyo, kwa maoni yangu naona hajaanza vizuri. Niliyoyaona na kuyasikia so far si dalili za mwisho mzuri kabisa.

1. Kwenye speech yake ya leo pale uwanja wa Jamhuri Dodoma, hajatambua uwepo wa vyama vya upinzani. Kama kuna mtu kasikia, nisahihisheni!

2. Sambamba na # 1 hapo juu, hakuna mwakilishi yoyote kutoka kambi ya upinzani aliyepewa nafasi ya kutoa salaam.

3. Kuna watu walikamatwa eti kwa kusema tu kuwa JPM ni mgonjwa. Mara tu baada ya kuapishwa, ilitarajiwa atoe decree ya kuachiliwa huru kwao mara moja lakini kimya hadi sasa.

4. Kuna watu wamekamatwa kwa vile eti hawaonyeshi kusikitika kifo cha JPM. Kama rais, alitarajiwa alikemee hili mara moja!

5. Kuna watu kadhaa wameripotiwa kupoteza maisha kwenye stampede iliyotokea jana kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Rais ni mfariji wa taifa, kupitia speech yake ya leo Dodoma alipaswa atamke neno la faraja kwa familia zilizokumbwa na msiba kutokana na tukio hilo.

Zipo dalili nyingine kadhaa lakini nimeorodhesha hizo hapo juu kwa uchache.

Rai na ombi langu kwa rais wetu mpya (mama Samia). Mama tutoe kwenye mtanziko huu ili maendeleo ya nchi yetu yawe jumuishi na wananchi wote tuyafurahie.

JK yupo hapo, nakushauri usisite kuomba ushauri kutoka kwake - mathalani ni jinsi gani aliweza ku co-exist na wapinzani in harmony.

Wakatabahu
Mwalimu M-Mbabe
22 March 2021

SOMA PIA
2022
2023
2024

2025
 
Pasu/Pasu Wilaya gani hiyo? Tumepata picha halisi mapekeo ya kifo cha Bwana mkubwa. Msiba huo umetueleza kinaga ubaga kuwa JPM anachukiwa sana na wananchi wa Jamhuri ya JF. Lakini wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walimkubali na walikuwa tayari kumfia.

Mama Samia shikilia hapo hapo, usisikilize wahamisha magoli ya lawama, hawana jema wala shukrani hao, utatukwaza sana kama utamkaribisha adui yeyote Ikulu. Long live the spirits of JPM.
 
Ngoja tuzike kwanza, Hizi ramli zenu ni mapema mno kuzitoa
 
Maridhiano ya nini mzee? Kwani tulikua na Vita. Rais Samia endeleza moto ule ule hakuna kumkaribisha mtu Ikulu kunywa Juice
Sisi ni watu wa kulalamika tu
Acha malalamishi yaendelee
Ila ni aibuu

Ova
 
Back
Top Bottom