Mkuu Mshana, hii haijakaa vizuri kwasababu kwenye shambulio la Lissu, ukiondoa uzushi wa mitaani na ramli chonganishi, hakuna mtuhumiwa yoyote rasmi, kufuatia shambulio hilo kufanywa na watu wasiojulikana, hivyo kitendo cha wewe kusema kuna mtuhumiwa, huku sheria zetu ziko wazi kabisa, kukitokea tukio lolote la jinai, kama kuna mtu yoyote mwenye taarifa zozote za mhusika au wahusika wa tukio hilo, anapaswa kuripoti kunakohusika na sio kutegenea uzushi wa mitaani na mitandaoni, vinginevyo na mada yako hii ni ramli chonganishi!
P. Mayala nakuheshimu sana ila katika hili umepotoka wa kati mwingine si lazima uchangie waweza kaa kimya kwani nayo ni busara, kama ingekuwa ni wewe umepigwa risasi, ukanyimwa haki ya kutibiwa, ukaporwa ubunge, uchunguzi haujafanyika na mbaya zaidi jalada la uchunguzi likafungwa, ukiwa huko nje ya nchi unataka kurudi nyumbani vitisho kibao hakika usingekuja na hoja ya kumpinga MSHANA.
Tundu Lissu kanyanyaswa sana na hii serikali, kateswa na hakuishi kwa raha hata kabla ya kupigwa risasi, kwa matukio yote haya hata kama wewe ni muunga juhudi za kununuliwa kwa Bombardier huna haja ya kupelekwa shule kuona madhila aliyotendewa Lissu.
Watu kama nyie akina Mayala, Lumumba & Co. ndiyo mnaowapa nguvu baadhi ya manyang'au mafedhuli hapa nchini kuendelea kufanya upumbavu wa kiwango cha Lami kwakuwa wanaona wanatetewa tena na watu Credible kama wewe Mayala.
Mayala wewe ni msomi na ninahakika kwa ninvyokufahamu unafahamu kila kitu kwamba serikali haimtaki Lissu na unajua hila anazofanyiwa kwa namna nyingi ila aidha unaogopa au umeamua kuungana na wenye nguvu ili kum-suppress asiye na nguvu sasa nakuomba unapokuta hoja za watu walio huru ki fikra kama alivyo MSHANA, so please don't try to block them for provoking against or going against those confiscating other's right to life.
Hata US embassy waliwahi mtuhumu bwana BASHITE kwamba anahusika na kupora watu haki ya kuishi na walisema wana credible information kuanzia mawasiliano na kila kitu na muda umefika wa hili genge la uhalifu lililojipa madaraka ya IZRAIL MTOA ROHO kufumuliwa kama ambavyo ilivyosambaratishwa KGB na kuunda FSB huko Russia.
Kuna watu huku kitaa tuliokoka bila kupenda ili tuweze kumuombea Lissu apone, wengine tulikuwa watenda dhambi ikiwamo kwa kuwaza na kwa kunena na kwa kutenda lakini dakika chache baada ya Lissu kupigwa tuliacha haya yote na kujikita katika maombi, sisi wengine hatujawahi funga kula kama daktari hajasema lakini tulilazimika kufunga ili mpendwa wetu apone kupitia maombi.
Tulijinyenyekeza kwa Mwenyezi Mungu ili Lissu apate kupona Mtanzania asiye na hatia aliyepigwa risasi mithili ya Simba aliyevamia makaazi ya watu na huku majangili wakubwa wakiachwa wakijivinjari, kwa bahati Mungu asiye na makuu akajibu na hisi sasa LISSU yu bukheri wa afya.
Sasa LISSU anataka kurudi home tunaona mizengwe ikiandaliwa na wauaji wake tunaweka mambo sawa watu kama akina Mayala mnataka kutetea upupu chunga sana tupo karne nyingine sasa hivi.