Mkuu hii sio habari ya kufumbiwa macho kabisa na watu wetu wa Usalama,leo hii sisi ambao tunanufaika kwa kuwa karibu na wachina huku tukijiona tumefanikiwa kuliko wanaotuzunguka kwenye jamii zetu muda sio mrefu hata sisi wanufaikaji wa vi misaada hivi tutaona uhalisia na matokeo ya huu Upumbavu tunaofaunya,
Sekta ya Madini imevamiwa kwa Kasi na hawa Wachina,kwa sasa wananunua Leseni za utafiti na Leseni ndogo za wachimbaji wadogo kwa Kasi ya kutisha, sio Kahama,Morogoro,Chunya, Geita mpaka Mpanda kote wanahodhi maeneo na wenyeji tukiendelea kutunishiana misuli kwa nani anayemiliki Gari zuri baada ya kupata mgao kutoka kwa wachina hao.
Watanzania tumelala sana kama raia wa kawaida lakini viongozi ndio tuseme pengine hawajui hata kwanini wapo hapo,
Utajiri wetu upo katika Ardhi,huu Upumbavu wa kuhonga Ardhi kwa Wachina hautoishia tu katika Ardhi bali utagusa mpaka katika maamuzi ya Chama na Serikali siku Maslahi ya hawa wanaopewa Ardhi hii kwa kisingizio cha uwekezaji watakapoguswa Maslahi yao.
Kwa kuwa wenye mamlaka wameona njia ya kuiokomboa nchi hii kiuchumi ni kuzitoa Fursa za hii nchi kwa Waarabu,Wachina na mataifa mengine ya nje na sisi wazawa hatuna Akili ya kufanya lolote zaidi ya kuimba muziki na kubishana kuhusu nani Bora kati ya Simba na Yanga basi wacha wenye Akili wachukue Fursa zote ila mwisho wa haya ni mbaya kuliko hata hizo zama za Ukoloni,
Mwenye masikio na asikie,kama una Akili ya kuona mbali huu ndio wakati wa Kuhodhi maeneo ya Ardhi yenye Madini na Rotuba nzuri kwa ajili ya kilimo(ufugaji) sio kwa ajili yako bali kwa vizazi vyako miaka 50 inayokuja,bila hivyo siku moja mtaona wajukuu zetu wakiwa Manamba ndani ya nchi yao kwa ujila wa Chakula tu.
Fikra Za Mwalimu Zidumu....