Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
- Thread starter
- #161
Kama nchi imeona njia ya kujikimu kiuchumi ni mikopo na kuleta wawekezaji wa nje ambao kwa kila namna wanaangalia namna ya kuingia mikataba itakayowafaidisha wao zaidi kuliko sisi .
TULISHAFELI KAMA TAIFA , yaani inashindikana vipi kujifunza kwa walioweza kukuza uchumi sa nchi zao bila kutegemea kubebwa bebwa? Gadaffi aliweza vipi kuinyanyua libya mpaka ilipofikia hatua ya kutokuwa na masikini hata mmoja nchini kwa kutegemea mafuta pekee? Najua kuna watu watasema oooo mafuta yana mzunguko mkubwa kuliko rasilimali tulizokuwa nazo haya "seretse khama" raisi wa kwanza wa botswana aliweza vipi kuinyanyua nchi yake bila kutegemea wawekezaji wa nje na mikopo na ukiangalia alipokea nchi kutoka kwa wakoloni ikiwa na 90% wasio na elimu ambao wengi ni wafugaji na wakulima? Tulifeli wapi?
N.b
Ndiyo maana sipendi kabisa kufuatilia siasa za bongo maa a ghadhabu niliyonayo basi tu.