Ujio wa wageni Chato ulituletea majanga? Wana usalama hawakuona?

Ujio wa wageni Chato ulituletea majanga? Wana usalama hawakuona?

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Mwanzoni mwa mwaka huu tumeshuhudia ugeni mkubwa ukimilinika kuelekea Chato huku tukiona hakuna tahadhali juu ya ugonjwa wa Covid 19 ikichukuliwa. Tulishudia waziri wa mambo ya nje wa China, rais wa Mozambique, rais wa Zanzibar na aliyekuwa makamu wake.

Baada ya muda sio mrefu tukasikia maalim Seif anaumwa na baadae kufariki. Baada ya muda tena aliyekuwa Chief Secretary ndugu Kijazi alifariki. Huku akiacha waziri Mpango akiwa hoi kitandani.

Tukiunga dots tutakuja kuona kuwa kuna tatizo ambalo lililetwa na ugeni uliokuja Chato ila hakuna tahadhari zilizochukuliwa. Hapa kuna jambo la kujifunza. Tuache kuwa tunachukulia kila kitu kwa mazoea.
 
Acha upotoshaji usio na msingi, mwendazake alikuwa na jeuri na mzaha usio na tija kwenye huo ugonjwa. Yeye ndio alioongoza kejeli dhidi ya ugonjwa huo, na sasa umegeuka fedheha kwa taifa zima. Kama hao wageni ndio walileta huo ugonjwa mbona wao hawajafa?
 
Screenshot_20210318-024847.jpg

hii sio coincidence, kuna tatizo mahali. our statesmen are falling and our country is dividing.
 
Back
Top Bottom