matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,968
- 19,368
Isaya 65:24
Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu;
Sio kila kitu unatakiwa kuomba. Vingi unatakiwa kuamini unavyo, hivyo unaanza kutenda kwa msingi kuwa kabla hujaviomba Mungu ameshakujibu tayari.
Kwa hiyo, mfano ukitaka nyumba, badala ya kukesha na kufunga anza kuhulizia bei ya materials, fanya windowshopping, anza kuangalia gari linafikaje site bila kujali unahela au huna. Kimsingi anza mitachakato ya ujenzi sio kuomba. Anza vitendo vingi kwa kidogo ulichonacho ukiamini kabla hujaviomba umeshapewa. Mungu ataunga mkono jihudi zako kwa imani hii.
Hii itakufanya upunguze maombi ya kuombaomba vitu, huo muda uutumie kutenda, kufanya michakato, kukutana na watu sahihi, ili umpe nafasi Mungu kutekeleza kauli yake hii ya isaya.
Mtu mwenye uelewa huu maombi yake hata kama ni siku nzima ni kama kupiga story na Mungu, kufanya ushirika na Mwenyezi sio kulialia, kupiga misamba na kugaragara kama mwehu.
Mungu qkupe neema ya maisha ya mtu ambaye anaamini kabla hajaomba ameshajibiwa, hivyo utatenda kisha utashukuru. Maisha yako yajae na kuzungukwa na vitendo zaidi nq mqombi ya kushukuru pamojq na dua za ushirika na Mungu wako.
Hautakuwa mtu wa kawaida.
Barikiwa
Mtumishi Matunduizi