Ujue usanii wa bondia Floyd Mayweather katika pambano lake na Connor McGregory

Ujue usanii wa bondia Floyd Mayweather katika pambano lake na Connor McGregory

Bondia maarufu duniani floyd mayweather,ambaye amepigana mara 49 bila kupigwa anategemea kuingia ulingoni na mc gregory ambaye sio proffesional boxer na hana rekodi yoyote katika boxing,yeye ni proffesional katika mchezo unaitwa mixed martial artist,(ni mchezo ambao unachanganya ngumi,mateke,kukabana,kudondoshana na vitu kama hivyo. kwanini nasema floyd ni mjanja.Ni wazi kabisa floyd atashinda hilo pambano kwa uhakika wa asilimia 90. kwa sababu zifuatazo

Mayweather ni proffesional katika boxer lakini anacheza na mtu ambaye sio proffesional katika boxer,yaani ameingia kwenye boxer halafu anakutana na mtu ambaye ndo kazi yake kwa mda wa kama miaka 30.

May weather kapigana mara 49 bila kupoteza wakati gregory kashapoteza huko kwenye mchezo wake sina hakika mara ngapi.

Kwenye boxing kuna roundi 12 wakati kwa gregory huwa kunakuwa na roundi 4
Mayweather kakutana na proffesional boxers hatari zaidi lakini hawakumpiga ndo anapigwaje na mtu anayecheza mchezo tofauti akampiga ,mfano man pacgiao ndo alikuwa wa kumpiga mayweather lakini ilishindikana.

May weather mjanja sana yaani amewaaminisha watu kama anawewza kupigwa ili pambano livutie mashabiki ili apige mpunga mwingi,sababu kama watu wangekuwa na uhakika kuwa mayweather atashinda toka mwanzo pambano lisingevutia mashabiki,lazima iwe haijulikani ni nani atapigwa ndo watu wanavutiwa.

Na mbaya zaidi mayweather mwenyewe ndo promoter kupitia mayweather promotion,kwahiyo lazima amsifie jamaa lakini ukweli ni kwamba jamaa atakaa mapema tu.ni mtazamo wangu wapenzi wa ngumi mnaweza mkaongeza vitu hapa​
wanatafuta kutengeneza hela tu, hakuna ndondi



Sent using Jamii Forums mobile app
 
hahaahaaa....we ndo inaonekana ata kurusha ngumi hujui....may jr anauwezo mkubwa wa kushinda...ILA MIAKA 800 hawez thubuti kupambana kwenye cage ya UFC(ultimamate fighting championship)

Sent using Jamii Forums mobile app
Aende huko MMA kufanya nin,ili iweje,yeye sio mchezo wake,..ila mcgregor ndo kashoboka kumtaka may jr.
 
Kama ndo hivo basi Mimi sitakaa nifuatilie tena hilo pambano. May weather mwenyewe msanii msanii yule, na sina hakika kama ni kweli alimpiga Pacquiao ktk lile pambano.

Sent using Jamii Forums mobile app
haujui mchezo wa ngumi fuatilia michezo mingine tu inatosha.


Yaani katika ma boxers ambao hawakumpa changamoto Floyd, Pacquiao ni miongoni mwao.
 
hawa watu kma Floyd Mayweather ndio wamefanya boxing idharaulike nlipoteza mda wangu bure kwenda kuangalia fight yake na Mann Pacyao nika ambulia kuona upuuzi tu in short Floyd Mayweather ni msanii tu kma mrisho mpoto
sio lazima ufatilie ngumi, hauzielewi, fuatilia michezo mingine tu inatosha.
 
Kwa watu wasiojua prof boxing kama wewe unasema Mayweather si mpiganaji lakini uzuri ni kwamba hakuna anayehitaji mawazo ya mtu kama wewe maana zaidi ya mapenzi yako huna ujuzi wowote wa ngumi. Msikilize mtu kama Sugar Ray Leonard kuhusu Mayweather anayeijua game vizuri. Msikilize Mike Tyson anamzungumzaje Mayweather siyo wachambuzi mbuzi wa bongo wanaojiita nao wachambuzi.
mkuu, hivi vitoto vimeanza kumjua Floyd alipocheza na Pacquiao, ndio maana references zao zipo hapo tu.


Huyo Manny Pacquiao ni bondia mdogo sana kwa Floyd hata warudiane mara mia Floyd bado atashinda tu.


Bondia wa kumpiga Floyd alikuwa Miguel Cotto au yule El Chino (Marcus Maidana)


Katika maisha ya boxing Floyd hajawahi kupigwa idadi kubwa ya ngumi kama alizopigwa na Maidana.


Na Cotto, ingawa Floyd alishinda bila ubishi ila alipokea ushindani mkubwa sana na alivuja damu kwa siku kadhaa baada ya pambano.
 
All.in all haya mapambano ya uzeeni ya maywether ni ya kupangwa ....mshindi anajulikana

Sent using Jamii Forums mobile app
Floyd mapambano yake ya mwisho yalikuwa

1)na Marcus Maidana (2014)

2)Manny Pacquiao (2015)

3)Andre Berto (2016)

4)CONOR McGregor (2017)

haya taja mapambano yapi unayozungumzia wewe halafu kawangalie hao wapinzani wake kama wa kawaida ukimtoa huyu ngedere Conor McGregor.
 
Mayweather ni mpigadili kwa tunaofaham kiundani asilimia 90% ya mechi za mayweather hua matakeo yanapangwa yan huwa ni maigizo km WWE.Anakula mikataba ya siri pamoja na makampuni mbalimbali zikiwepo kampuni za kubet pamoja na upande wa mtu anayechezanae match yan yote tunafanyiwa maigizo watu wanapiga pesa.Reference nzuri ni km ulivosema mwnyw kwamba yeye ni mpiganaji na promota ni kampuni yake mwenyewe na ndivo ilivokua hata ktk pambano lake na paq wa philipine.Hio ndio sabab anaingiza pesa nyingi sana na mara kadhaa alikua celebrity wa kwanza kwa pesa duniani had alipokuja kuzidiwa na akina ronaldo na messi...Ktk hela hashindwi kufanya chochote usishangae ht akashindwa ili achane mikeka ya dunia nzima ili apige pesa ambayo haijashikwa na celebrity yoyote duniani..
huna unachokijua kuhusu boxing.
 
hahaahaaa....we ndo inaonekana ata kurusha ngumi hujui....may jr anauwezo mkubwa wa kushinda...ILA MIAKA 800 hawez thubuti kupambana kwenye cage ya UFC(ultimamate fighting championship)

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajua tofauti ya boxing na hyo UFC?
Mayweather ana fanya maonyesho ya ngumi.na ndo maana kamchagua mpinzani ambaye hachezi boxing.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua tofauti ya boxing na hyo UFC?
Mayweather ana fanya maonyesho ya ngumi.na ndo maana kamchagua mpinzani ambaye hachezi boxing.

Sent using Jamii Forums mobile app
WEE CIWEZI TAJA NCICHOKIJUA...ila kwa kua may jr ni mpiga pesa....amejitaftia mpinzani asiekua proffessional wa boxing...na kwa personalty ya macgregor...ya trash talking..imevuta attention kubwa ITS ALL ABOUT MAKING MONEY JOH

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngumi zilikua enzi ya wakina Tyson sio hawa warembo ngumi gani za kisenge zinaenda raundi kumi na mbili?

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani watu msio jua ngumi mnajulikana tu lazima mumtaje Tyson au Pacquiao.


Na kwa taarifa yako Tyson angekuwa na uzito sawa na Floyd halafu wazipige, nakuhakikishia hata ngumi 50 asingefikisha usoni mwa Floyd.
 
Nikweli kabsa,boxing ni mchezo namba moja wa real fight dunian,..mcgregor anacheza round4 halaf anatumia had mateke,kukabana,kupigana makofi ndo aje akutane na mtu anaye aim kichwan tuu na ndo mkali wa hizo kaz,mcgregor atakufa ulingon..kama ni mfatiliaj wa boxing utakumbuka jins kaseba alivochapwa na cheka had alitaka poteza maisha,
Jana kuna kipindi cha sport nimeangalia jana tv1. Mambo ya boxing ya jumuiya ya nchi za Africa. Mtanzania amepigwa kiboya sana mpaka sikukaa nikaamini. Raundi ya kwanza dkk.1: 58s. Mwanaume mzima kaangushwa kwa K.O kama kiroba cha MO sembe.
 
Yaani watu msio jua ngumi mnajulikana tu lazima mumtaje Tyson au Pacquiao.


Na kwa taarifa yako Tyson angekuwa na uzito sawa na Floyd halafu wazipige, nakuhakikishia hata ngumi 50 asingefikisha usoni mwa Floyd.
Wewe naona bado utoto unakusumbua kwanza nenda kapekue historia ya Tyson au Mohamed Ali alafu urudi hapa tuzungumze

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata pambano lake na PAC alikua promota vilevile

sent from my iPhone 7 nimeinunua SAPNA pale Posta mtaa SAMORA
 
Tatizo lako umeandika kiushabiki sana, ni kweli Mayweather ni undefeated but hakupata misuko suko kama ya kina tyson, Mapambano yake mengi ya Myweather alikuwa anapigana na watu ambao ni aged au ambao washapoteza zile nguvu mfano Pacquiao alikataa kupigana nae mara ya kwanza 2010 kwa sababu alimuhofia atampiga kaweka vikwazo viiingi kipindi hicho Pacman yupo on fire akaja kukubali baadae pacman kashaanza kupigwa na madogo hvyo hvyo kwa Dela hoya na wengineo,
halafu chengine usiende kupigana na Unknown enemy hicho mmarekani anakijua sana hapigani vita na nchi asiyojua atashindaje sasa mayweather anaenda kupigana na mtu ambaye hajui game plan yake aiset vipi, maana kama ingekuwa ni boxer mwengine angetumia tu video kuangalia weakness za enemy wake lakn kwa huyu Macgregor ni ngumu kwakwe kujua atatokeaje ulingoni, cha msingi nacho kiona kwa Mayweather atatumia experience tu na sometimes experience haitoshi kumaliza kazi.

for your info tu labda nikusaidie Professionally katika MMA Macgregor amepigana 24, 21 wins (18 times by knockout) 3 loses and he's just 29 yrs old.

Halafu round 4 za MMA usifananishe na boxing kijana vitu viwili tofauti wataalamu watakwambia so usimdharau Macgregor ukaona wa kawaida ila tukutane tu august 26 tushuhudie May weather akipewa kichapo kitakatifu
Wewe kweli zwazwa, yaani una mfananisha Floyd wa 2010 na Pacquiao wa 2010???


Floyd wa 2010 Pacquiao asingefikisha hata round tano, Floyd alikuwa na kasi balaaa, anarusha makonde ya maana.


Embu tafuta mapambano ya Floyd ya miaka hiyo halafu angalia ya Pacquiao halafu leta mrejesho.


Halafu unataka kudanganya watu kwamba Floyd hajapigana na boxers hatari, nahisi akili yako haipo sawa,

Asilimia kubwa ya Boxers waliopigana na Pacquiao Floyd pia amepigana nao, na hata bondia awe moto kiasi gani akipigana na Floyd anaonekana ni dhaifu sana.

Muangalie bondia kama Canelo Alvarez amepambana mapambano 51 kashinda 49 katoa sare moja na amepigwa moja na Floyd Mayweather.


Alipopigana na Mayweather alionekana bondia dhaifu sana, alipigwa kirahisi sana lakini akikutana na wengine anaonekana moto wa kuotea mbali.
 
WEE CIWEZI TAJA NCICHOKIJUA...ila kwa kua may jr ni mpiga pesa....amejitaftia mpinzani asiekua proffessional wa boxing...na kwa personalty ya macgregor...ya trash talking..imevuta attention kubwa ITS ALL ABOUT MAKING MONEY JOH

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo sawa may weather ana ganga njaa.amekuwa kama lipumba.anatuambia anajiuzulu alaf anarud

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom