Ujumbe kutoka kwa wanachama minority wa CHADEMA kwenda kwa mwenyekiti mpya Tundu Lissu

Ujumbe kutoka kwa wanachama minority wa CHADEMA kwenda kwa mwenyekiti mpya Tundu Lissu

Kwani watu wanachaguliwa kwa kanda au sifa? Muanze kuwa mnatumia akili wakati mwingine na kuepuka infiriority complex. Watanzania hawaangalii rangi ya paka. Wanaangalia paka atakayeshika panya
Sizungumzii authority nazungumzia legitimacy.

This is politics. And politics is science. Power Politics is how you can convince makundi ya kijamii kukuunga mkono. Iwapo akili ya vijana wa chadema bado inaamini watu wa pwani hawana weledi wa kuteuliwa chadema. Nimekula kwenu. It's to a matter of inferiority its about legitimacy Uhalali wa kuwashawishi watu baada kujua utamaduni wao
 
Huwezi nielewa kama si ktk think tank. Hatuhitaji Authority CHADEMA. Sisi watu wa pwani hatuamini ktk kugombea vyeo. Bali tunaamini ktk Ligitimacy (uhalali).

Legitimacy ni kukubalika na kupata mamlaka kutoka kwa watu wa kawaida wa jamii fulani wale wanaoongozwa.

Uhalali unahusisha masuala ya imani, na ridhaa ya watu, hata kama mamlaka hayo yanaungwa mkono na katiba za taasisi.

Uhalali ni bora kuliko Mamlaka na vyeo.

Uhalali ni wa muhimu kwa sababu hujenga uaminifu na mshikamano kati yako na wale wanaoongozwa.

Mwenyekiti ana mamlaka na Mamlaka isiyo na uhalali hupoteza imani ya watu na inaweza kusababisha kukataliwa.

Lissu atakataliwa ukanda wa pwani kwa sababu kaonyesha upendeleo ulio dhahiri. Upendeleo si kwa watu wa pwani tu bali kuna manung'uniko ya team FEM kutengwa.

Lissu anahitaji kura za watu wa pwani. Na chaguo lilobaki ni moja kuungana na ACT na kuwaachia kiti cha Urais.

Sisi kama wafuasi minority ndani ya chadema kwasasa tuko dilemma kwa kuwa hatuna nguvu tena ya kuwashawishi jamii yetu kwa kuwa mtazamo wa jamii yetu wanataka kuona uwakilishi wa watu wao.

Mimi ni mpenda mabadiliko nikiingia mkono sera ya majimbo yenye uhuru zaidi wa kujiamulia mambo yake wenye. Na naelewa vzr sana. Na kabla ya uchaguzi nilikuwa nafanya kampeni kwa viongozi wa kidini kuielewa dhana hii ili waweze kuinga mkono. Nikielewa tokea awamu wanaituhumu chadema na udini. Sasa kwa teuzi za mwenyekiti waliofanya nimebaki speachless
Kama siasa makini zingekuwa zinafuata udini na ukabila basi tungekuwa na taabu kubwa kama taifa, uhalali unaozungumzia wa kuteuliwa siyo merit za uongozi unatengeneza jamii inayoongozwa kiimla wala siyo kidemokrasia.

Katika kampeni za CHADEMA sikusikia kundi lolote lililokuwa linahubiri au kufanya kampeni kwa kufuata misingi ya udini na ukabila, hata tena mbili zilizokuwa zinachuana hazikujitanabaisha na udini wala ukanda. Tanzania inaenda mbele na si kurudi nyuma, tunatofautishwa na nchi kama kenya kwa sababu Tanzania licha ya kuwa na makabila zaidi ya 126 badi haijaadhiri umoja wa watanzania.

Hata wakati wa kugombea uhuru kulikuwa hakuna matabaka ya udini. Nikuulize swali ulitoka CUF sawa, katika uongozi wa CUF enzi za Ibrahim Lipumba na Maalim Seif kwenye safu ya uongozi kulikuwa na wakristo wangapi? Na ulisikia wenye akili wakilalamika?

Mimi nakushauri rudi ACT waislamu viongozi ni wengi hutaumia achana na CHADEMA hiki ni chama cha demokrasia kama ulivyoona kwenye uchaguzi. Hakuna kampeni za udini hapa
 
Si uende huko chauma shida ni nini?
Sawa. Hata chawa mmoja wa Mbowe aliwashauri chawa wa Lissu kama Mbowe hana ushawishi watafute vyama vingine.

Kama hizi ndio fikra za Lissu mtapiga ninyi wenyewe kura kama mtashinda.

Kam watu wa pwani wanapoona kauli hizi za Ego kutoka chadema, tunapata nguvu kuwa ccm na chadema wote ni wabaguzi na hawatoweza kushinda uchaguzi kama si kwa kuibiana kura.

Nani sasa atasimama juani kusubiri kuwapigia kwa chama wasichokuwa na wawakilishi wao
 
Kama siasa makini zingekuwa zinafuata udini na ukabila basi tungekuwa na taabu kubwa kama taifa, uhalali unaozungumzia wa kuteuliwa siyo merit za uongozi unatengeneza jamii inayoongozwa kiimla wala siyo kidemokrasia.

Katika kampeni za CHADEMA sikusikia kundi lolote lililokuwa linahubiri au kufanya kampeni kwa kufuata misingi ya udini na ukabila, hata tena mbili zilizokuwa zinachuana hazikujitanabaisha na udini wala ukanda. Tanzania inaenda mbele na si kurudi nyuma, tunatofautishwa na nchi kama kenya kwa sababu Tanzania licha ya kuwa na makabila zaidi ya 126 badi haijaadhiri umoja wa watanzania.

Hata wakati wa kugombea uhuru kulikuwa hakuna matabaka ya udini. Nikuulize swali ulitoka CUF sawa, katika uongozi wa CUF enzi za Ibrahim Lipumba na Maalim Seif kwenye safu ya uongozi kulikuwa na wakristo wangapi? Na ulisikia wenye akili wakilalamika?

Mimi nakushauri rudi ACT waislamu viongozi ni wengi hutaumia achana na CHADEMA hiki ni chama cha demokrasia kama ulivyoona kwenye uchaguzi. Hakuna kampeni za udini hapa
Ushauri mzuri. Na nina wasiwasi wewe ni Lissu na alichofanya ni mpango maalum.

Lkn hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa kujidanganya kuwa hayapo​

Ushauri mzuri. Na nina wasiwasi wewe ni Lissu na alichofanya ni mpango maalum.

Lkn hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa kujidanganya kuwa hayapo​

Hakuna tatizo bali tatizo liko kwenye mtazamo wako ambao unataka tatizo.

Hapa umeonyesha rangi rangi yako asili, chuki dhidi ya Lissu kwa sababu ni mkristu. Toka ameingia kwa kampeni za wazi wala hakufanya kwa siri, ila wewe ndio una mpengo maalumu: UDINI
 
Majitu yanayoendekeza udini na ukabila yanakiwa kukatwa vichwa.
PUMBAVU.
 
Hakuna tatizo bali tatizo liko kwenye mtazamo wako ambao unataka tatizo.

Hapa umeonyesha rangi rangi yako asili, chuki dhidi ya Lissu kwa sababu ni mkristu. Toka ameingia kwa kampeni za wazi wala hakufanya kwa siri, ila wewe ndio una mpengo maalumu: UDINI
Swali ni dogo tu. Unajua maana ya legitimacy. Kama hujui subiri dunia itakufundisha. Nasaha zangu ni za nia nzuri na muda bado tunao ikiwa tunataka kushika dola.

Legitimacy ndio roadmap ya kushika dola.
 
Sizungumzii authority nazungumzia legitimacy.

This is politics. And politics is science. Power Politics is how you can convince makundi ya kijamii kukuunga mkono. Iwapo akili ya vijana wa chadema bado inaamini watu wa pwani hawana weledi wa kuteuliwa chadema. Nimekula kwenu. It's to a matter of inferiority its about legitimacy Uhalali wa kuwashawishi watu baada kujua utamaduni wao
Kwani wamegombea wakaondolewa? Sijaona unacholalamika. Si waligombea waliomba kugombea na kura zimepigwa wazi? Ulitaka waseme sasa tuchague wa kutoka Pwani? Hiyo ni tabia ya kujishtukia. Mimi wa Pwani sikwenda kuomba kugombea wangenichaguaje?
 
Nazungumzia legitimacy na sio authority.

Kama hamuelewi kuhusu uongozi (leadership) na ushawishi subirini October.
 
Nilitaka Mwenyekiti na Chawa wale waweze kuona vinavyopaswa kuonwa sawa na lengo alilojipambanua halo Mwenyekti. Kuunganisha majukwaa ktk kuleta mabadiliko ya utawala.

Kwa ufupi nilimshari mwenyekiti achague katibu mkuu Muoslam na ingewezekana naibu katibu mkuu wake. Na nilipendekeza Sheikh Ponda angekuwa katibu mkuu wa chadema.

Lkn hajachelewa kwa msaada wa idara ya intelijensia ya chadema wanapaswa kufanya utafiti wa muislam gani awe mgombea Urais. Anaweza pia kuleta OMo wa ACT au Prof Njozi wa Mum kuwa mgombea Urais wa JMT

Kinyume cha hapo falsafa ya nguvu ya umma, au strong together itaishia kwenye mabango tu.
Marais wte-Zenji na Tangnyika waislam na wa2 wamefnga midomo. Wajumbe toka Zenji wote waislam, watu kimya. Katiba hazishabikii dini na walochagliwa walijituma wenyewe kugombea hivyo kama mtu kagwaya kugombea, nlifikiri ni uoga binafsi. Wasituletee mambo ya udini usio kuwepo, tulisghapita huko toka zmani
 
Baada ya CUF kusambaratika wako wanachama waliofatia Maalim Seif, (MwenyeziMungu amsamehe makosa yake) na kundi jengine lilikwenda kwa Mzee Lipumba. Kundi la tatu ambao pengine ni wachache ni kundi lile linaloamini 'You can only Fool some Pple some time, but you can't fool all the pple all the time.

Sisi wachache tusikubali kuburuzwa (bendera kufata upepo)tuliamini kama kweli Maalim Seif alikuwa mtaka mabadiliko angejiunga na chadema, kwasababu hoja ya Prof Lipumba kujitoa kwa muda CUF ktkt ya harakati za uchaguzi ilikuwa ni kuwapinga Chadema kumsimamisha Lowasa nafasi ya Urais.

Hivyo kama Lipumba hakuwa sahihi, ilibidi Maalim aungane na chadema. Lkn matokeo yake anajiunga na ACT.

Hivyo wote ACT na CUF walituthibitishia kuwa wanatumiwa na ccm kuvuruga Umoja wa wataka mabadiliko.

Lkn ktk uchaguzi wa Mwenyekiti Chadema tuliaminishwa kwa kuambiwa Mbowe nae anatumiwa na ccm kudhoofisha harakati kupitia mapesa ya Abdul.

Kwa hiyo sisi tuliamua kujiunga chadema haikuwa kwa bahati mbaya. Kwani hatukuamini kufata watu (wasaliti) bali sera. Na kwa kuwa trust imepungua kwa watu. Sera ya chadema ya majimbo yenye uhuru zaidi wa kujiamulia mambo yetu wenyewe ilikuwa ndio suluhisho la taifa letu.

Titaiogopaje sera hii ambayo ngome ya mwambao ndio chanzo cha mapato ya nchi kwa zaidi ya 85%.

Vijana wa nchi hii kila kanda wanaona potential za kiuchumi za maeneo yao Lkn kikwazo ni mfumo wa Serikali Kuu.

Kwa utafiti nilioufanya mfumo sahihi wa serikali za majimbo tz ni kucopy na kupaste mfumo wa taifa la Switzerland.

Politics of Switzerland - Wikipedia

Nilifanya utafiti wa kuwauliza vijana wa jimboni kwa kwann wamekata tamaa kushiriki kupiga kura. Wengi walijibu. 'Hatutopiga Kura bali tutaungana na jukwaa lolote ambalo linatoa wito na wanahamasisha kugawana fito.

Wako tayari kuunga mkono jukwaa (chama) kinachotoa wito wa kugawana fito.

Kwamba hawamuamini mgombea yyt wa urais atoke huko anakotoka awaeleze anataka kuwatawala ili awaletee maendeleo. Hakuna wanaemuamini. Si Samia, Si Lissu, Si Magufuli kwa case ya 2020.

Nikasema kumbe watu wangu hawajui sera ya majimbo ya CHADEMA. Majimbo yatakayokuwa na Uhuru zaidi wa kujiamulia mambo yake wenyewe, kiuchumi, kiutamaduni, kisiasa, kijamii ambapo wengi ktk jimbo/kanda husika ndio watunga sheria. Kwa kuanzia mamlaka ya mtaaa.

Kwamba Lissu au Samia anapogombea nafasi ya Urais anapokwa mamlaka yake yote ya kiunga waliyoanayo sasa na kuwa ni mfariji mkuu tu. Kama sasa alivyo Rais wa JMT akienda Znz. Anakuwa hana mamlaka yyt kwa Znz. Case study nyingine ni Rais za Ethiophia.

Sera ya majimbo yenye uhuru zaidi wa majimbo (kanda) kujiamulia mambo yao wenyewe ni mfumo bora zaidi wa muungano kwa tz, EA, afrika. Na ndilo kimbilio la mataifa yote duniani yaliyoungana.

Ni Muungano wa safaru pekee. Sio jeshi, Sio nini.

Sasa nirudi kwenye msingi wa andiko.

Baada ya uchaguzi wa kumtafuta Mwenyekiti wa chadema moja ya ajenda ya mabadiliko ya uongozi mpya wa chadema aliohubiri Lissu ni kuunganisha majukwaa yote ya wapenda mabadiliko.

Bahati mbaya sana, mimi au sisi watu wa ukanda wa mwamvai kama ngome ya wapenda mabadiliko. kwa kuzingatia propaganda za CCM na ACT kuwa CHADEMA ni chama cha Udini na ukanda. Tulitegemea sana uongozi mpya ungekuja kukata hizi cheap propaganda kwa kuunganisha uongozi wa juu na majukwaa haya hasa makubwa. Nazungumzia jukwaa au ngome ya Watu wa mwambao.

Hali iliyojitokeza baada ya uchaguzi ni kama ulikuwa ni uchaguzi wa kutafuta domination kati ya KKKT na Catholic Tz.

Na kwamba kwa maumivu makubwa Catholic wameamua kudominate nafasi zote za juu za chadema.

Kuanzia nafasi za kuchaguliwa na kuteuliwa. Tunajiuliza sisi minority ktk chama lkn majority ktk population ya Tz, ni bahati mbaya au walipanga.

Sisi kama watu wa mwambao Uwakilishi wetu uko wapi chadema. Kwamba wanaamini kabisa sisi tunaweza kupanga foleni ya kupiga kura kuchagua watu wa tabaka moja. Hivi ni kweli inteligensia ya chadema hawakuliona hilo.

Au ni mkakati Maalum wa Mwenyekiti Mpya wa kuwapa Waislam minority ndani ya chama mkono wa kwa heri ili wapeleke nguvu zao kwa chama kilichojiandaa kuwa ngome kuu ya ukanda wa pwani hata kama ni ccm B .

Mwenyekiti Lissu kapoteza nafasi hii adhimu ya kuyaunganisha majukwa nchini. Na kwamba chama kitamshinda mapema sana.

Nipo tayari kusahihishwa ili niweze kurejesha imani yangu kwa chadema. Na ninaamini imani hii ndio imani ya walio wengi ambao kwasasa wamesusa kabisa mambo ya kupiga kura.

Matamanio yangu kwasasa yanavutiwa na CHAUMMA
Kwani sisiemu tangia iwape nafasi watu wa mwambao mlipata faida gani? Siasa zaudini zimepitwa na wakati Rais kua Muislam au mtu wa pwani imewasaidia vipi kuondokana na umasikini mmekua mkichagua sisiemu maisha yenu yote imewasaidia nini mkiwa ni moja ya maeneo masikini nchini? Muacheni TAL aunde team yake kadiri anavyoona inafaa mlitabiri kusambaratika kabla yanuchaguzi tunzeni kumbukumbu safari hii atawashangaza
 
Marais wte-Zenji na Tangnyika waislam na wa2 wamefnga midomo. Wajumbe toka Zenji wote waislam, watu kimya. Katiba hazishabikii dini na walochagliwa walijituma wenyewe kugombea hivyo kama mtu kagwaya kugombea, nlifikiri ni uoga binafsi. Wasituletee mambo ya udini usio kuwepo, tulisghapita huko toka zmani
Utaratibu wa ccm ni kupingana kwa awamu kati ya waislam na wakristo. Wameamua kufanya hivyo tutafute legitimacy kwa wananchi. Hiki kitu ni muhimu lkn kama hamuelewi muda utaongea.

Kuhusu znz wanafata demokrasia ya kweli. Kwani pamoja kina asilimia ndogo ya wahindi na wakristo. Lkn ktk kila teuzi basi wanashirikishwa.

Ndio ni kanuni ya kidemokrasia ya majority lead, minority wanatambuliwa
 
Kwani sisiemu tangia iwape nafasi watu wa mwambao mlipata faida gani? Siasa zaudini zimepitwa na wakati Rais kua Muislam au mtu wa pwani imewasaidia vipi kuondokana na umasikini mmekua mkichagua sisiemu maisha yenu yote imewasaidia nini mkiwa ni moja ya maeneo masikini nchini? Muacheni TAL aunde team yake kadiri anavyoona inafaa mlitabiri kusambaratika kabla yanuchaguzi tunzeni kumbukumbu safari hii atawashangaza
Mimi ni muislam Minority chadema.

Ubaduguzi wa ccm kwa waislam, kuwadhulu na kuwatumia sheria kali dhiki ya waislam ndio sababu ya waislam wengi kuchukua ccm. Kwass SISIEM inachukua madaraka kwa wizi. Si kwa ridhaa ya wananchi. Kimbilio ni chama kikuu cha upinzani chadema. Lkn mbona sasa nayo ni wabaguzi kama ccm. Mfumo kristo, Mfumo Kristo ni anguko
 
Back
Top Bottom