Ujumbe kwa Joyce Mhavile: Waandishi wako hawajui tofauti ya Mahatma Gandhi na Indira Gandhi - pathetic!

Siku hizi ITV haina tofauti kubwa na TBC. Imekuwa inahabarisha kwa kujipendekeza kwa serikali.

Kwa mantiki hiyo ndio maana wanaandika habari kama hiyo lengo kumfurahisha Hangaya na timu yake bila kujali uhalisia wa habari yenyewe.
 
Siku hizi ITV haina tofauti kubwa na TBC. Imekuwa inahabarisha kwa kujipendekeza kwa seriali.

Kwa mantiki hiyo ndio maana wanaandika habari kama hiyo lengo kumfurahisha Hangaya na timu yake bila kujali uhalisia wa habari yenyewe.
Hata TBC kwenye taarifa ya habari saa 1 asubui 10.10.23 wameendeleza makosa toka itv na radio1 kwa kusema eti Tanzania na India wanaendeleza uhusiano ulioanzishwa na Nyerere na Mahtima Ghandi.
 
Hiyo siyo TBC wana haki ya kutangaza chochote
Wana haki ya kutangaza chochote? Hapana. Nakumbusha tu: ITV na Radio One ni vyombo vya habari.

Kazi ya vyombo vya habari ni kuhabarisha, kuburudisha na kuelimisha. Hapa kwenye kuhabarisha, waandishi wa habari wanaongozwa na ukweli na usahihi. Kinyume na hapo ni kujiondolea uaminifu kwa wasomaji/wasikilizaji.

Kitendo tu cha kuwekwa bandiko hilo hapa JF ni kudhihirisha hilo swala la kujiondolea uaminifu.

CC: Waandishi wa habari wote.
 
Walikuwa wanaburudisha
 
Wewe ndiyo inabidi ujiongeze...kwani kuanzisha mahusiano lazma watu hao wawili waonane? Mahatma Ghandi aliweka misingi ya India kushirikiana na mataifa mengine kupigania Uhuru..jambo ambalo mrithi wake aliendeleza kwahiyo msingi ni kutoka kwa Mahatma Gandhi
 
Sasa mkuu mambo ya ITV dola inaingiaje ?
 
ITV watakuwa wamerusha habari kama walivyoipokea bila kufanya uhariri. Lakini Mkuu wetu pia kwenye press moja fupi aliyoitoa kule India ...
Sikumuelewa!
Naendelea kujifunza.
 
bila shaka atakuwa Farhia ndo alikuwa anasoma.Mara kadhaa nishamshauri awe anapitia kabla ya kusoma
 
Usiwaonee ITV hiyo ni kauli imenukuliwa kutoka kwenye kinywa Cha Rais nao wameireport hivyohivyo na sio wao pekee bali
vyombo vyote
kwa hiyo wa kulaumiwa hapo ni
Rais na kurugenzi ya mawasiliano IKULU maana wao ndio wameiwasilisha habari kwa
vyombo husika
 
Uchawa ukizidi mambo kama haya hujitokeza.ITV ya Sasa si Ile ya 1980s.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…