Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Na. M. M. Mwanakijiji
Mojawapo ya maajabu makubwa ni hili la watu kuamini kuwa ujio wa Katiba Mpya utawapa Rais ambaye ataweza kudhibitiwa na "taasisi". Kwamba, Katiba Mpya itazuia Rais kufanya lolote na kuwa atakuwa analazimishwa kusikiliza mashauri mbalimbali. Prof. Assad ni miongoni mwa watu ambao amejionesha kukerwa mno na jinsi Magufuli alikuwa; hasikilizi, hapigwi maneno ya wataalam, na watendaji wenye maneno ya kitalaamu. Inawezekana siyo yeye tu bali wapo wengine ambao nao walikuwa wanakerwa kuwa Magufuli "hasikilizi". Na tunawaona wengine ambao nao wanafikia mahali pa kusema "Magufuli hakufanya lolote".
Sasa, wanataka tuwe na Rais ambaye anapewa ushauri na kila mtu na anatakiwa kusikiliza kila ushauri kwani asipousikiliza au kuukubali basi anakuwa "haambiliki". Inanikumbusha maneno yaliyosemwa wakati wa Nyerere; aliitwa pia "Haambiliki". Ati Magufuli alikuwa anawakera kwa sababu walitaka awasikilize na asiwaulize; akubali bila maswali! Sasa inawezekana wanaona Rais Samia ni wa kuambiwa kila kitu; kwamba wanampa mashauri ya kila namna na anaonekana anayafuata. Inawezekana wanaona kuwa Rais Samia anawakubalia kila mashauri hata ambayo matokeo yake siyo mazuri. WAnachofurahia ni kuwa wamelipata "sikio la mama".
Ndio maana tunaweza kuona wanashindana kukandia awamu ya tano (ambayo wao walikuwemo). Inaonekana kabisa kuwa ili mama akupe sikio inabidi umpapase kwa maneno mazuri ya kumkandia mtangulizi wake. Magufuli hakujenga kiwanda hata kimoja, uwekezaji ulipungua, maisha yalikuwa Magumu, watalii walikimbia, uchumi ulidorora... wanasema na kusema ili waseme "ila sasa awamu ya sita" mambo yamekavaa vizuri! Wanajaribu kutenda kana kwamba Rais Samia alishinda uchaguzi mahali bila ya Magufuli! Lakini hawa wanaotaka Rais anayesikiliza kila ushauri inabidi tuwakatae.
Tunawapinga na kuwakataa kwa sababu wanataka kumchukua Rais kuwa mateka wa fikra zao na mashauri yao. Watamshauri akikataa wataanza kusema "Rais hatusikilizi tena". Ukweli ni kuwa Rais - hata ije Katiba Haramu Mpya - hatakiwi kukubali ushauri wa kila mtu, hata kama ni maprofesa kama Assad. Anatakiwa kusikiliza na kuuliza; hatakiwi kukubali bila maswali! Na ni hatari zaidi kumtaka Rais awafurahishe kwa kuwa karibu na watu wenye kumsifia na kumwambia mambo mazuri.
Profesa Assad na watu wenye fikra kama zake hawamtakii mema Rais, wanamtega, na wanajaribu kumfanya awe Rais wa picha!
Hili tunawakatalia; waache ufyatu!
MMM