Rais ambaye hasikilizi watu wake nae hatumtaki.tumejionea miaka mitano ya tabu na mateso kama siyo Mungu kuingilia kati hali ingekua mbaya sana muda huu.
Watu wake ni kina nani?
Je hao watu wake wote kwa umoja wao wanakubaliana kwa kila hoja?
Au unaamini wana hoja moja?
Kimsingi ni Raisi pekee ndio anayewajibika kwa maamuzi yote anayofanya. Kwa kuwa yeye ndio aliyepigiwa kura.
Je kama atasikiliza kila mtu huyo mtu atakayemshauri atawajibika kwa ushauri wake kama utakuwa na matokeo mabaya?
Tambua kuna maeneo mengi ambayo Rais anatakiwa asikilize ushauri kwa mujibu wa Katiba. Hao ndio wanatakiwa kusikilizwa na watawajibika kwa ushauri walioutoa. Hebu chukua mfano huu;
1. Wewe fala mmoja ushauri jambo A lifanyike.
2. Mimi fala mwingine nashauri afanye B badala ya A
3. Halafu yule fala mwingine aseme hao wote wapumbavu tufanye C.
Halafu wote sisi hatutoulizwa kwa chochote mambo yakienda mrama afuate ushauri upi sasa wa kwako au wa kwangu au yule?
Hebu fikiria tutakuwa na Raisi wa aina gani leo kasema A kesho B keshokutwa anasema C.
Nikupe mfano wa uwajibikaji.
Rais Clinton alikuwa anaziara ya kikazi Japan. Ndege yake ikachelewa kwa nusu saa.
Wamarekani wakashangaa inakuwaje Raisi achelewe nusu saa nzima? Wakaambiwa Mpambe wa Raisi alishauri Raisi anyoe kwanza kabla ya kupanda ndege kwa kuwa muonekano haukuendana na hadhi yake.
Mpambe wa Rais aliwajibishwa kwa kusababisha msafara wa Raisi kuchelewa kwa nusu saa.
Watu wengine wanatoa maoni sio Ushauri. Wa kumshauri wapo kikatiba na kisheria na wanalipwa sio wewe au mimi vidampa..