Verrazanno
JF-Expert Member
- Sep 15, 2021
- 454
- 1,011
anayesikiliza kila mtu na la kila Mtu!
"anayesikiliza kila mtu na la kila mtu"
Tofauti ni nini ?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
anayesikiliza kila mtu na la kila Mtu!
hahahaha. Kwamba mtego atauruka kwa style ya kwamba 'kila mliloniambia nimewasikiliza na kufanya.mbn mnanilaumu sasa'Nadhani Kuna watu wamesahau kabisa Baba wa Taifa alipoonya sana la Rais kupewapewa ushauri bila kuwa na msimamo wake. Kinachoendelea sasa ni kujaribu kumtega Rais Samia ili asiwaulize au kuwakatalia. Ni mtego mbaya sana.
Who was Magufuli..he was nobody! Try to see beyond a person.Rais kuwa msikivu ni kupitia mamlaka za kikatiba zilizowekwa kumshauri kama Bunge.
Rais anayejaribu kulicontrol Bunge ana kuwa na tabia kama za Magufuli, si msikivu tu, bali hata sheria zinazotungwa ni kwa maelekezo.
Prof Assad ni msomi na alilopendekeza ni kwa muktadha huo.
Aisee....basi bora hiyo katiba mpya ndiyo tuiapishe iwe rais!Who was Magufuli..he was nobody! Try to see beyond a person.
Siku katiba mpya ikija..ije na guidance kuwa, tukichagua RAIS mpya, hapo ikulu na taasisi yote ya urais nayo iwe na watu WAPYA wote! aliyetuumba hajawahi kuumba SUPERMAN..miaka 60 toka uhuru bado tunawaza na kubehave km taifa la miaka 18..hatuwezi kuwa wajinga wa kiwango hicho.
Kufikiri kwa aina hii ndio kati ya mafua nchi hii inahangaika nayo bila dawa..kiwango duni kabisa cha uwezo wa kufikiri.Aisee....basi bora hiyo katiba mpya ndiyo tuiapishe iwe rais!
Hahitajiki mtu pale au sivyo!
Mkuu, lakini kwa vigezo vyote vya utawala bora, makini na wenye kujali katiba, sheria, kanuni na miongozo mbalimbali, ufyatu ulikuwa wa kiwango cha juu sana katika utawala wa awamu ya tano. Na hapa ndipo kilipokuwa chanzo kikuu cha uwepo wa hoja fyatu kutoka kwa wasomi mbalimbali.Na. M. M. Mwanakijiji
Mojawapo ya maajabu makubwa ni hili la watu kuamini kuwa ujio wa Katiba Mpya utawapa Rais ambaye ataweza kudhibitiwa na "taasisi". Kwamba, Katiba Mpya itazuia Rais kufanya lolote na kuwa atakuwa analazimishwa kusikiliza mashauri mbalimbali. Prof. Assad ni miongoni mwa watu ambao amejionesha kukerwa mno na jinsi Magufuli alikuwa; hasikilizi, hapigwi maneno ya wataalam, na watendaji wenye maneno ya kitalaamu. Inawezekana siyo yeye tu bali wapo wengine ambao nao walikuwa wanakerwa kuwa Magufuli "hasikilizi". Na tunawaona wengine ambao nao wanafikia mahali pa kusema "Magufuli hakufanya lolote".
Sasa, wanataka tuwe na Rais ambaye anapewa ushauri na kila mtu na anatakiwa kusikiliza kila ushauri kwani asipousikiliza au kuukubali basi anakuwa "haambiliki". Inanikumbusha maneno yaliyosemwa wakati wa Nyerere; aliitwa pia "Haambiliki". Ati Magufuli alikuwa anawakera kwa sababu walitaka awasikilize na asiwaulize; akubali bila maswali! Sasa inawezekana wanaona Rais Samia ni wa kuambiwa kila kitu; kwamba wanampa mashauri ya kila namna na anaonekana anayafuata. Inawezekana wanaona kuwa Rais Samia anawakubalia kila mashauri hata ambayo matokeo yake siyo mazuri. WAnachofurahia ni kuwa wamelipata "sikio la mama".
Ndio maana tunaweza kuona wanashindana kukandia awamu ya tano (ambayo wao walikuwemo). Inaonekana kabisa kuwa ili mama akupe sikio inabidi umpapase kwa maneno mazuri ya kumkandia mtangulizi wake. Magufuli hakujenga kiwanda hata kimoja, uwekezaji ulipungua, maisha yalikuwa Magumu, watalii walikimbia, uchumi ulidorora... wanasema na kusema ili waseme "ila sasa awamu ya sita" mambo yamekavaa vizuri! Wanajaribu kutenda kana kwamba Rais Samia alishinda uchaguzi mahali bila ya Magufuli! Lakini hawa wanaotaka Rais anayesikiliza kila ushauri inabidi tuwakatae.
Tunawapinga na kuwakataa kwa sababu wanataka kumchukua Rais kuwa mateka wa fikra zao na mashauri yao. Watamshauri akikataa wataanza kusema "Rais hatusikilizi tena". Ukweli ni kuwa Rais - hata ije Katiba Haramu Mpya - hatakiwi kukubali ushauri wa kila mtu, hata kama ni maprofesa kama Assad. Anatakiwa kusikiliza na kuuliza; hatakiwi kukubali bila maswali! Na ni hatari zaidi kumtaka Rais awafurahishe kwa kuwa karibu na watu wenye kumsifia na kumwambia mambo mazuri.
Profesa Assad na watu wenye fikra kama zake hawamtakii mema Rais, wanamtega, na wanajaribu kumfanya awe Rais wa picha!
Hili tunawakatalia; waache ufyatu!
MMM
Rais siyo secretary wa kutekeleza tu anachoambiwa, ni hatari kwa nchi kuwa na rais wa aina anayomtaka Assad.Na. M. M. Mwanakijiji

Wacheni vitisho nyie hilo shimo likowapi?Rais Samia anategwa ili amridhishe kila mtu,shimo watakalomwingiza hatatoka.
Nimemwambia mtoa mada kama anadhani Mama anasikiliza kila kitu aende na yeye akampe ushauri wake..Kwamba Assad na wengineo wakisema kuwa Magufuli alikuwa hasikilizi maneno ya wataalamu, haimaanishi kuwa "Sasa, wanataka tuwe na Rais ambaye anapewa ushauri na kila mtu na anatakiwa kusikiliza kila ushauri kwani asipousikiliza au kuukubali basi anakuwa "haambiliki". "
Rais sio mjinga kama wewe,Soma hapa👇Rais Samia anategwa ili amridhishe kila mtu,shimo watakalomwingiza hatatoka.
HatujaelewanaWatu wake ni kina nani?
Je hao watu wake wote kwa umoja wao wanakubaliana kwa kila hoja?
Au unaamini wana hoja moja?
Kimsingi ni Raisi pekee ndio anayewajibika kwa maamuzi yote anayofanya. Kwa kuwa yeye ndio aliyepigiwa kura.
Je kama atasikiliza kila mtu huyo mtu atakayemshauri atawajibika kwa ushauri wake kama utakuwa na matokeo mabaya?
Tambua kuna maeneo mengi ambayo Rais anatakiwa asikilize ushauri kwa mujibu wa Katiba. Hao ndio wanatakiwa kusikilizwa na watawajibika kwa ushauri walioutoa. Hebu chukua mfano huu;
1. Wewe fala mmoja ushauri jambo A lifanyike
2. Mimi fala mwingine nashauri afanye B badala ya A
3. Halafu yule fala mwingine aseme hao wote wapumbavu tufanye C..
Halafu wote sisi hatutoulizwa kwa chochote mambo yakienda mrama afuate ushauri upi sasa wa kwako au wa kwangu au yule?
Hebu fikiria tutakuwa na Raisi wa aina gani leo kasema A kesho B keshokutwa anasema C
Nikupe mfano wa uwajibikaji.
Rais Clinton alikuwa anaziara ya kikazi Japan. Ndege yake ikachelewa kwa nusu saa... Wamarekani wakashangaa inakuwaje Raisi achelewe nusu saa nzima? Wakaambiwa Mpambe wa Raisi alishauri Raisi anyoe kwanza kabla ya kupanda ndege kwa kuwa muonekano haukuendana na hadhi yake. Mpambe wa Rais aliwajibishwa kwa kusababisha msafara wa Raisi kuchelewa kwa nusu saa.
Watu wengine wanatoa maoni sio Ushauri. Wa kumshauri wapo kikatiba na kisheria na wanalipwa sio wewe au mimi vidampa..
Nimecheka Sana ,mzee mwanakijiji anampiga bit prof, nchi ngum sanaNa. M. M. Mwanakijiji
Mojawapo ya maajabu makubwa ni hili la watu kuamini kuwa ujio wa Katiba Mpya utawapa Rais ambaye ataweza kudhibitiwa na "taasisi". Kwamba, Katiba Mpya itazuia Rais kufanya lolote na kuwa atakuwa analazimishwa kusikiliza mashauri mbalimbali. Prof. Assad ni miongoni mwa watu ambao amejionesha kukerwa mno na jinsi Magufuli alikuwa; hasikilizi, hapigwi maneno ya wataalam, na watendaji wenye maneno ya kitalaamu. Inawezekana siyo yeye tu bali wapo wengine ambao nao walikuwa wanakerwa kuwa Magufuli "hasikilizi". Na tunawaona wengine ambao nao wanafikia mahali pa kusema "Magufuli hakufanya lolote".
Sasa, wanataka tuwe na Rais ambaye anapewa ushauri na kila mtu na anatakiwa kusikiliza kila ushauri kwani asipousikiliza au kuukubali basi anakuwa "haambiliki". Inanikumbusha maneno yaliyosemwa wakati wa Nyerere; aliitwa pia "Haambiliki". Ati Magufuli alikuwa anawakera kwa sababu walitaka awasikilize na asiwaulize; akubali bila maswali! Sasa inawezekana wanaona Rais Samia ni wa kuambiwa kila kitu; kwamba wanampa mashauri ya kila namna na anaonekana anayafuata. Inawezekana wanaona kuwa Rais Samia anawakubalia kila mashauri hata ambayo matokeo yake siyo mazuri. WAnachofurahia ni kuwa wamelipata "sikio la mama".
Ndio maana tunaweza kuona wanashindana kukandia awamu ya tano (ambayo wao walikuwemo). Inaonekana kabisa kuwa ili mama akupe sikio inabidi umpapase kwa maneno mazuri ya kumkandia mtangulizi wake. Magufuli hakujenga kiwanda hata kimoja, uwekezaji ulipungua, maisha yalikuwa Magumu, watalii walikimbia, uchumi ulidorora... wanasema na kusema ili waseme "ila sasa awamu ya sita" mambo yamekavaa vizuri! Wanajaribu kutenda kana kwamba Rais Samia alishinda uchaguzi mahali bila ya Magufuli! Lakini hawa wanaotaka Rais anayesikiliza kila ushauri inabidi tuwakatae.
Tunawapinga na kuwakataa kwa sababu wanataka kumchukua Rais kuwa mateka wa fikra zao na mashauri yao. Watamshauri akikataa wataanza kusema "Rais hatusikilizi tena". Ukweli ni kuwa Rais - hata ije Katiba Haramu Mpya - hatakiwi kukubali ushauri wa kila mtu, hata kama ni maprofesa kama Assad. Anatakiwa kusikiliza na kuuliza; hatakiwi kukubali bila maswali! Na ni hatari zaidi kumtaka Rais awafurahishe kwa kuwa karibu na watu wenye kumsifia na kumwambia mambo mazuri.
Profesa Assad na watu wenye fikra kama zake hawamtakii mema Rais, wanamtega, na wanajaribu kumfanya awe Rais wa picha!
Hili tunawakatalia; waache ufyatu!
MMM
Kwa hiyo waachwe wasomi muingie nyie mburula au?
Mambo ya Wazalendo wa Chato haya 👇
View attachment 2232652
Attribute namba moja ya msomi ni kuwa objective sio subjective katika kujadili issue; pili anatakiwa ausimamie ukweli bila kujali gharama yake. Msomi wa kweli haongozwi na tumbo kayika kujadili issue ya umma.Kwa hiyo waachwe wasomi muingie nyie mburula au?
Mambo ya Wazalendo wa Chato haya 👇
Raisi hapaswi kwenda kinyume na ushauri wa kitaalamu kwenye maeneo ambayo expert opinion inatakiwa kufuatwa kwa mujibu wa sheria.Kwa hiyo kwa vile watalaamu wanashauri asiende kinyume nao?
Kwanza unaposema MAAMUZI YA KUUMIZA WATU una maana gani? Mtumishi anapokuwa mzembe au mwizi hakuna watu wanaoumia kwa yeye kuwa hivyo? Kwa nini unahukumu reaction ya tatizo badala ya kuhukumu tatizo limetokeaje..kama hupendi reaction za papo kwa papo be careful na kazi, usifanye makosa! Unatenda kosa halafu unataka uulizwe wakufanye nini baada ya kukosea..hakuna kitu cha hivyo mahali popote.Nimemwambia mtoa mada kama anadhani Mama anasikiliza kila kitu aende na yeye akampe ushauri wake..
Ukifuatulia hata ziara za Rais amekuwa akiruka viunzi vingi vya mambo binafsi ya watu kuchongeana..
Mfano juzi kuna mbunge kamchongea DED ,Rais kajibu tuu kwamba watu wafuate taratibu na sheria..
Mwendazake mpenda sifa angehemka na kufanya maamuzi waliyoita papo kwa papo huku yakiwa ya kukurupuka na kuumiza watu..
Rais Samia akiona jambo linahitaji consultations au hana ufahamu nalo mara nyingi huwa anasema nalichukua,huwa hakurupuki.
Tena kiuhalisia walitaka si asikilize ushauri wa kila mtu, Bali walichotaka ni kumfanya asikilize ushsuri wa kila mpumbavu aliyejiona ana nguvu Fulani, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Taasisi, Siasa, Wafanyabiashara, Wawekezaji, Matajiri, nk...Na. M. M. Mwanakijiji
Mojawapo ya maajabu makubwa ni hili la watu kuamini kuwa ujio wa Katiba Mpya utawapa Rais ambaye ataweza kudhibitiwa na "taasisi". Kwamba, Katiba Mpya itazuia Rais kufanya lolote na kuwa atakuwa analazimishwa kusikiliza mashauri mbalimbali. Prof. Assad ni miongoni mwa watu ambao amejionesha kukerwa mno na jinsi Magufuli alikuwa; hasikilizi, hapigwi maneno ya wataalam, na watendaji wenye maneno ya kitalaamu. Inawezekana siyo yeye tu bali wapo wengine ambao nao walikuwa wanakerwa kuwa Magufuli "hasikilizi". Na tunawaona wengine ambao nao wanafikia mahali pa kusema "Magufuli hakufanya lolote".
Sasa, wanataka tuwe na Rais ambaye anapewa ushauri na kila mtu na anatakiwa kusikiliza kila ushauri kwani asipousikiliza au kuukubali basi anakuwa "haambiliki". Inanikumbusha maneno yaliyosemwa wakati wa Nyerere; aliitwa pia "Haambiliki". Ati Magufuli alikuwa anawakera kwa sababu walitaka awasikilize na asiwaulize; akubali bila maswali! Sasa inawezekana wanaona Rais Samia ni wa kuambiwa kila kitu; kwamba wanampa mashauri ya kila namna na anaonekana anayafuata. Inawezekana wanaona kuwa Rais Samia anawakubalia kila mashauri hata ambayo matokeo yake siyo mazuri. WAnachofurahia ni kuwa wamelipata "sikio la mama".
Ndio maana tunaweza kuona wanashindana kukandia awamu ya tano (ambayo wao walikuwemo). Inaonekana kabisa kuwa ili mama akupe sikio inabidi umpapase kwa maneno mazuri ya kumkandia mtangulizi wake. Magufuli hakujenga kiwanda hata kimoja, uwekezaji ulipungua, maisha yalikuwa Magumu, watalii walikimbia, uchumi ulidorora... wanasema na kusema ili waseme "ila sasa awamu ya sita" mambo yamekavaa vizuri! Wanajaribu kutenda kana kwamba Rais Samia alishinda uchaguzi mahali bila ya Magufuli! Lakini hawa wanaotaka Rais anayesikiliza kila ushauri inabidi tuwakatae.
Tunawapinga na kuwakataa kwa sababu wanataka kumchukua Rais kuwa mateka wa fikra zao na mashauri yao. Watamshauri akikataa wataanza kusema "Rais hatusikilizi tena". Ukweli ni kuwa Rais - hata ije Katiba Haramu Mpya - hatakiwi kukubali ushauri wa kila mtu, hata kama ni maprofesa kama Assad. Anatakiwa kusikiliza na kuuliza; hatakiwi kukubali bila maswali! Na ni hatari zaidi kumtaka Rais awafurahishe kwa kuwa karibu na watu wenye kumsifia na kumwambia mambo mazuri.
Profesa Assad na watu wenye fikra kama zake hawamtakii mema Rais, wanamtega, na wanajaribu kumfanya awe Rais wa picha!
Hili tunawakatalia; waache ufyatu!
MMM
Wenzetu hao ni zaidi ya katiba, hata tukiwa na katiba kama yao bado hatuwezi kuwa kama wao.Binafsi nikupe mfano mzee mwanakijiji:
Raia wanahitaji katiba ambayo Rais kama binadamu anaweza kudhibitiwa katika baadhi ya mazingira mfano mzir ni Rais Trump alipotaka kujenga ukuta wa Mexico kwakua wawakilishi waliona sio kipao mbele waligoma na still Rais inabdi asikilizeaoni ya wengi