Ujumbe kwa Prof. Assad: Hatutaki Rais anayesikiliza kila mtu na la kila Mtu!

Na. M. M. Mwanakijiji

Mojawapo ya maajabu makubwa ni hili la watu kuamini kuwa ujio wa Katiba Mpya utawapa Rais ambaye ataweza kudhibitiwa na "taasisi". Kwamba, Katiba Mpya itazuia Rais kufanya lolote na kuwa atakuwa analazimishwa kusikiliza mashauri mbalimbali. Prof. Assad ni miongoni mwa watu ambao amejionesha kukerwa mno na jinsi Magufuli alikuwa; hasikilizi, hapigwi maneno ya wataalam, na watendaji wenye maneno ya kitalaamu. Inawezekana siyo yeye tu bali wapo wengine ambao nao walikuwa wanakerwa kuwa Magufuli "hasikilizi". Na tunawaona wengine ambao nao wanafikia mahali pa kusema "Magufuli hakufanya lolote".

Sasa, wanataka tuwe na Rais ambaye anapewa ushauri na kila mtu na anatakiwa kusikiliza kila ushauri kwani asipousikiliza au kuukubali basi anakuwa "haambiliki". Inanikumbusha maneno yaliyosemwa wakati wa Nyerere; aliitwa pia "Haambiliki". Ati Magufuli alikuwa anawakera kwa sababu walitaka awasikilize na asiwaulize; akubali bila maswali! Sasa inawezekana wanaona Rais Samia ni wa kuambiwa kila kitu; kwamba wanampa mashauri ya kila namna na anaonekana anayafuata. Inawezekana wanaona kuwa Rais Samia anawakubalia kila mashauri hata ambayo matokeo yake siyo mazuri. WAnachofurahia ni kuwa wamelipata "sikio la mama".

Ndio maana tunaweza kuona wanashindana kukandia awamu ya tano (ambayo wao walikuwemo). Inaonekana kabisa kuwa ili mama akupe sikio inabidi umpapase kwa maneno mazuri ya kumkandia mtangulizi wake. Magufuli hakujenga kiwanda hata kimoja, uwekezaji ulipungua, maisha yalikuwa Magumu, watalii walikimbia, uchumi ulidorora... wanasema na kusema ili waseme "ila sasa awamu ya sita" mambo yamekavaa vizuri! Wanajaribu kutenda kana kwamba Rais Samia alishinda uchaguzi mahali bila ya Magufuli! Lakini hawa wanaotaka Rais anayesikiliza kila ushauri inabidi tuwakatae.

Tunawapinga na kuwakataa kwa sababu wanataka kumchukua Rais kuwa mateka wa fikra zao na mashauri yao. Watamshauri akikataa wataanza kusema "Rais hatusikilizi tena". Ukweli ni kuwa Rais - hata ije Katiba Haramu Mpya - hatakiwi kukubali ushauri wa kila mtu, hata kama ni maprofesa kama Assad. Anatakiwa kusikiliza na kuuliza; hatakiwi kukubali bila maswali! Na ni hatari zaidi kumtaka Rais awafurahishe kwa kuwa karibu na watu wenye kumsifia na kumwambia mambo mazuri.

Profesa Assad na watu wenye fikra kama zake hawamtakii mema Rais, wanamtega, na wanajaribu kumfanya awe Rais wa picha!

Hili tunawakatalia; waache ufyatu!

MMM
Wewe huna hoja una viroja.

Sasa ndiyo umesema nini, taka utakacho na kila mtu atake atakacho ili mradi hakuna anaevunja sheria ya nchi.

Wewe hujuwi kwanini Dr. Assad aifanyiwa mizengwe na utawala wa Magufuli? Huelewi kuwa alisema ukweli kwenye ile "interview" na kuna watu kama wewe ambao hamuupendi ukweli kwa "ignorance" tu.

Bichwa lako la habari lingine na utumbo wako wa habari mwingine.
 
hivi wabongo tunataka Rais wa aina gani? anaesikiliza au asiesikiliza? tusifungane midomo tupige kura tujuane!!
Nchi imegawanyika. Kuna wengi wanataka kuongozwa kidikteta na kuna wengi wanataka kuongozwa kidemokrasia. Taifa haliwezi kubaki pamoja kama huo mgawanyiko ukiendelea. Korea zamani ilikuwa ni nchi moja baadaye ikagawanyika, Korea Kaskazini na Korea Kusini. Kaskazini wanaongozwa kidikteta, Kusini wanaongozwa kidemokrasia. Tanzania nayo itagawanyika tuu kama hakuna cha kuwaunganisha.
 
Jibu lako lina maana kuwa Magufuli alikuwa hasikilizi, lakini siyo kweli kwani kuna mifano mingi sana inayoonyesha akiwa anasikiliza ushauri. Tatizo la Assad ni kuwa alitaka Magufuli amsikilize na achukue ushauri wake oja kwa moja, jambo ambalo siyo kweli, kwani Magufuli naye alikuwa na analytical skills za kujua banba ya kuacheive malengo yake. Ukimpa ushauri ambao hauko kwenye malengo yake anakuachia hapo hapo.
Jibu langu liko based na kauli ya mleta mada kuwa "Inawezekana siyo yeye tu bali wapo wengine ambao nao walikuwa wanakerwa kuwa Magufuli "hasikilizi", na tukichukulia kama alichosema ni kweli, ndo nikajibu kama nilivyojibu. Sikujikita zaidi kama kauli hii ina ukweli au la.
 
Sidhani kama Magufuli alikuwa hasikilizi. Mara ngapi tuliona anasikiliza vilio vya watu kila anapokuwa ziarani sehemu mbalimbali?? Kuna wa kusikiliza ila kuna wa kutimua hapo hapo. Nakumbuka kuna mkurugenzi ama das aliwahi kujikanyaga maelezo akampa nafasi mwingine kuelezea na akamsikiliza vizuri hadi huyo aliyetoa maelezo ndo akapewa uongozi wa juu na kumvua aliyeshindwa. Danadana hatuzitaki
Usinijibu mimi hivyo wewee!!!!! Sema Magufuli alikuwa na roho mbaya sana, na alikuwa anaionyesha hadharanni...Idd Amin alikuwa na roho mbaya, lakini hakuwahi kuionyesha hadharani.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Mojawapo ya maajabu makubwa ni hili la watu kuamini kuwa ujio wa Katiba Mpya utawapa Rais ambaye ataweza kudhibitiwa na "taasisi". Kwamba, Katiba Mpya itazuia Rais kufanya lolote na kuwa atakuwa analazimishwa kusikiliza mashauri mbalimbali. Prof. Assad ni miongoni mwa watu ambao amejionesha kukerwa mno na jinsi Magufuli alikuwa; hasikilizi, hapigwi maneno ya wataalam, na watendaji wenye maneno ya kitalaamu. Inawezekana siyo yeye tu bali wapo wengine ambao nao walikuwa wanakerwa kuwa Magufuli "hasikilizi". Na tunawaona wengine ambao nao wanafikia mahali pa kusema "Magufuli hakufanya lolote".

Sasa, wanataka tuwe na Rais ambaye anapewa ushauri na kila mtu na anatakiwa kusikiliza kila ushauri kwani asipousikiliza au kuukubali basi anakuwa "haambiliki". Inanikumbusha maneno yaliyosemwa wakati wa Nyerere; aliitwa pia "Haambiliki". Ati Magufuli alikuwa anawakera kwa sababu walitaka awasikilize na asiwaulize; akubali bila maswali! Sasa inawezekana wanaona Rais Samia ni wa kuambiwa kila kitu; kwamba wanampa mashauri ya kila namna na anaonekana anayafuata. Inawezekana wanaona kuwa Rais Samia anawakubalia kila mashauri hata ambayo matokeo yake siyo mazuri. WAnachofurahia ni kuwa wamelipata "sikio la mama".

Ndio maana tunaweza kuona wanashindana kukandia awamu ya tano (ambayo wao walikuwemo). Inaonekana kabisa kuwa ili mama akupe sikio inabidi umpapase kwa maneno mazuri ya kumkandia mtangulizi wake. Magufuli hakujenga kiwanda hata kimoja, uwekezaji ulipungua, maisha yalikuwa Magumu, watalii walikimbia, uchumi ulidorora... wanasema na kusema ili waseme "ila sasa awamu ya sita" mambo yamekavaa vizuri! Wanajaribu kutenda kana kwamba Rais Samia alishinda uchaguzi mahali bila ya Magufuli! Lakini hawa wanaotaka Rais anayesikiliza kila ushauri inabidi tuwakatae.

Tunawapinga na kuwakataa kwa sababu wanataka kumchukua Rais kuwa mateka wa fikra zao na mashauri yao. Watamshauri akikataa wataanza kusema "Rais hatusikilizi tena". Ukweli ni kuwa Rais - hata ije Katiba Haramu Mpya - hatakiwi kukubali ushauri wa kila mtu, hata kama ni maprofesa kama Assad. Anatakiwa kusikiliza na kuuliza; hatakiwi kukubali bila maswali! Na ni hatari zaidi kumtaka Rais awafurahishe kwa kuwa karibu na watu wenye kumsifia na kumwambia mambo mazuri.

Profesa Assad na watu wenye fikra kama zake hawamtakii mema Rais, wanamtega, na wanajaribu kumfanya awe Rais wa picha!

Hili tunawakatalia; waache ufyatu!

MMM
Mwanakijiji hajapinga katiba mpya ,muwe mnasoma na kuelewa, yeye anapingana na maoni ya professor Assad, ya kutaka kulazimisha mkuu wa nchi asikilize na kutetekeleza kila ushauri anaopewa.

Ndio maana mwanakijiji akasema hata katiba mpya ikija haitamlazimisha rais kufuata ushauri wa kila mtu.

Someni muelewe kwanza kabla ya kujibu hoja ya mleta mada
Wengine wanasema bila kusoma...
 
Asad na mazuzu wengine hawana hoja taifa halina dira halina mipango ya muda mrefu (30-50-100 Years) na hivi havifungamani na katiba, angejikita kushauri viongozi wazingatie weledi katika uhuru wa kiutendaji wa watumishi waliowateua kukidhi na kuishi sheria kanuni taratibu na miongozo. Nyakati zake zilipita kwa sasa tunaona ya kwamba alikuwa snitch kama ambavyo Samia anaona Magufuli akichafuka yeye anang'aa nawaambieni Rais wa nchi hii ajaye 2025 kamwe haitatokea akawa Samia wala mwanamke yeyote. Taifa lina agenda nzito saana huyu atimize matakwa ya katiba hadi 2025 basi awe mstaafu wa 2 in one.

Tunamkubali Ila si kwa nafasi ya Urais na ndiomana hakuwa Rais.

Shukrani. HAHM ndiye mpango wa nchi na haitabadirika ifahamike hivyo.

NB: Katiba Bora msingi wake ni maarifa ya watu wa nchi husika.
Tanzania mna maarifa ya kutengeneza katiba bora?
Mbona mnasifia katiba ya Kenya mnashindwa nini kuitohoa kama ilivyo? Mnajua uzuri wa katiba ya Uganda ya 1995?

Chukueni katiba ya Kenya itafsiriwe kwa kiswahili tupewe muda tuisome kisha tuainishe mapungufu tupige kura ya referendum.
 
hivi wabongo tunataka Rais wa aina gani? anaesikiliza au asiesikiliza? tusifungane midomo tupige kura tujuane!!
Waweke mgomba pale uwe raisi! Hatujielewi! Mungu kaamua kutuacha Tu maana Kwa Mungu hatupo. Kwa shetani hatujafika, hatuna dira wala muelekeo!
Rais asisikilize na kumfanyia kazi ushauri wa kila mtu! Achanganye na za kwake.
 
Umemamliza huyu MMM ni taka taka kama Paskali
Afadhali hata P huyu alijijengea jina kipindi cha Kikwete kumbe haikuwa lolote ni dini na ukabira tu..kukaa kwake marekani hakujambadirisha kitu.na yule mzee Kichuguu. Udine mbaya sana ... Pascal hana huo udine.
 
M
Na. M. M. Mwanakijiji

Mojawapo ya maajabu makubwa ni hili la watu kuamini kuwa ujio wa Katiba Mpya utawapa Rais ambaye ataweza kudhibitiwa na "taasisi". Kwamba, Katiba Mpya itazuia Rais kufanya lolote na kuwa atakuwa analazimishwa kusikiliza mashauri mbalimbali. Prof. Assad ni miongoni mwa watu ambao amejionesha kukerwa mno na jinsi Magufuli alikuwa; hasikilizi, hapigwi maneno ya wataalam, na watendaji wenye maneno ya kitalaamu. Inawezekana siyo yeye tu bali wapo wengine ambao nao walikuwa wanakerwa kuwa Magufuli "hasikilizi". Na tunawaona wengine ambao nao wanafikia mahali pa kusema "Magufuli hakufanya lolote".

Sasa, wanataka tuwe na Rais ambaye anapewa ushauri na kila mtu na anatakiwa kusikiliza kila ushauri kwani asipousikiliza au kuukubali basi anakuwa "haambiliki". Inanikumbusha maneno yaliyosemwa wakati wa Nyerere; aliitwa pia "Haambiliki". Ati Magufuli alikuwa anawakera kwa sababu walitaka awasikilize na asiwaulize; akubali bila maswali! Sasa inawezekana wanaona Rais Samia ni wa kuambiwa kila kitu; kwamba wanampa mashauri ya kila namna na anaonekana anayafuata. Inawezekana wanaona kuwa Rais Samia anawakubalia kila mashauri hata ambayo matokeo yake siyo mazuri. WAnachofurahia ni kuwa wamelipata "sikio la mama".

Ndio maana tunaweza kuona wanashindana kukandia awamu ya tano (ambayo wao walikuwemo). Inaonekana kabisa kuwa ili mama akupe sikio inabidi umpapase kwa maneno mazuri ya kumkandia mtangulizi wake. Magufuli hakujenga kiwanda hata kimoja, uwekezaji ulipungua, maisha yalikuwa Magumu, watalii walikimbia, uchumi ulidorora... wanasema na kusema ili waseme "ila sasa awamu ya sita" mambo yamekavaa vizuri! Wanajaribu kutenda kana kwamba Rais Samia alishinda uchaguzi mahali bila ya Magufuli! Lakini hawa wanaotaka Rais anayesikiliza kila ushauri inabidi tuwakatae.

Tunawapinga na kuwakataa kwa sababu wanataka kumchukua Rais kuwa mateka wa fikra zao na mashauri yao. Watamshauri akikataa wataanza kusema "Rais hatusikilizi tena". Ukweli ni kuwa Rais - hata ije Katiba Haramu Mpya - hatakiwi kukubali ushauri wa kila mtu, hata kama ni maprofesa kama Assad. Anatakiwa kusikiliza na kuuliza; hatakiwi kukubali bila maswali! Na ni hatari zaidi kumtaka Rais awafurahishe kwa kuwa karibu na watu wenye kumsifia na kumwambia mambo mazuri.

Profesa Assad na watu wenye fikra kama zake hawamtakii mema Rais, wanamtega, na wanajaribu kumfanya awe Rais wa picha!

Hili tunawakatalia; waache ufyatu!

MM
Magufuli alikuwa kichaa kabisa na kama vichaa wengine walivyo huwa hawajitambui kuwa na tatizo na hujiona wana akili kuliko watu wote na hawatakagi ushauri. Mwenye akili timamu hupokea ushauri na kuichambua na kufanya maamuzi
 
Rais ambaye hasikilizi watu wake nae hatumtaki.tumejionea miaka mitano ya tabu na mateso kama siyo Mungu kuingilia kati hali ingekua mbaya sana muda huu.
Labda hakukusikiliza wewe lakini J.P.M Alikuwa anatembea kila mahali kuzikiliza watu wake ambao ndo walimchagua nae huyu wa sasa kutwa anazunguka ulaya na kwa matajiri maana ndo anaamini watamulinda katka urahisi wake
 
Asad na mazuzu wengine hawana hoja taifa halina dira halina mipango ya muda mrefu (30-50-100 Years) na hivi havifungamani na katiba, angejikita kushauri viongozi wazingatie weledi katika uhuru wa kiutendaji wa watumishi waliowateua kukidhi na kuishi sheria kanuni taratibu na miongozo. Nyakati zake zilipita kwa sasa tunaona ya kwamba alikuwa snitch kama ambavyo Samia anaona Magufuli akichafuka yeye anang'aa nawaambieni Rais wa nchi hii ajaye 2025 kamwe haitatokea akawa Samia wala mwanamke yeyote. Taifa lina agenda nzito saana huyu atimize matakwa ya katiba hadi 2025 basi awe mstaafu wa 2 in one.

Tunamkubali Ila si kwa nafasi ya Urais na ndiomana hakuwa Rais.

Shukrani. HAHM ndiye mpango wa nchi na haitabadirika ifahamike hivyo.

NB: Katiba Bora msingi wake ni maarifa ya watu wa nchi husika.
Tanzania mna maarifa ya kutengeneza katiba bora?
Mbona mnasifia katiba ya Kenya mnashindwa nini kuitohoa kama ilivyo? Mnajua uzuri wa katiba ya Uganda ya 1995?

Chukueni katiba ya Kenya itafsiriwe kwa kiswahili tupewe muda tuisome kisha tuainishe mapungufu tupige kura ya referendum.
HAHM !
 
hivi wabongo tunataka Rais wa aina gani? anaesikiliza au asiesikiliza? tusifungane midomo tupige kura tujuane!!
Huwa ninasemaga kiumbe binadamu hakijawahi kueleweka..lakini trust me kuna kiumbe kinachoitwa mtanzania 🙆‍♀️🙆‍♀️ Huyu kiumbe hajawahigi na wala hata kuja kueleweka aise..🤨🤨

Tunachuki na wivu wa ajabu sana.mtu akifanya vizuri watamponda,akifanya vibaya watamponda,akijiua watamponda,akiendelea kuishi na kufanya mambo Yake watamponda😳😳😳ni watu wa kulalamika Kwa kila kitu hatujui kushukuru kabisa😩😩
 
Back
Top Bottom