Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
HATARI YA MTAWALA KUJIPA SIFA YA "mungu"
Kwa Mkono wa Robert Heriel.
Mwaka Juzi niliandika makala niliyoipa kichwa kisemacho "NJAMA ZA IKULU, HATA RAIS/MFALME ANAWEZA KUDANGANYWA"
Soma hapa 👉👉👉👉Hata Rais hudanganywa: Njama za Ikulu ndizo hizi
katika makala hiyo nilieleza kinaga ubaga namna watawala wanavyoweza kujiingiza mkenge au kuingizwa mkenge wakaishia pabaya. Nilimtahadharisha pia aliyekuwa Rais wa wakati huo, Hayatti Magufuli. Sasa ni wakati wa kumtahadharisha Rais mpya, Mama yetu, Mhe. Samia Suluhu. Ikikupendeza fuata ushauri, isipokupendeza acha kwa maana sio lazima.
Ni NINI MAANA YA MTAWALA KUJIPA SIFA YA "mungu" Ilhali yeye ni Binadamu?
Ni kile kitendo cha Mtawala iwe ni Rais/ Mfalme, Mkurugenzi au kiongozi yeyote kujifanya yeye ni muweza, hagusiki, haambiliki, kupenda utukufu, kukataa kukosolewa, kufanya maamuzi yoyote hata kama yanavunja sheria za nchi, taasisi au sheria za Mungu, kutaka kutawala milele, kujifanya hakuna kama yeye, yaani asipokuwepo anaamini wengine hawatafanya. Hiyo ndio maana ya kiongozi kujipa sifa ya mungu wakati ni binadamu.
Historia inaonyesha wale wote waliojipa sifa ya uungu/mungu waliishia pabaya, waliangamia kabla ya wakati wao. Wapo wafalme walioonja joto la jiwe baada ya kujitia miungu watu, na wote waliangamia kabla ya wakati wao.
Sifa za MUNGU zinazochukuliwa na Watawala na kujifanya mungu ni kama ifuatavyo;
1. Uweza
Mungu ni muweza wa kile kitu, hana mshirika, yeye ndiyo muweza wa yote, haihitaji mshirika ili afanye mambo yake. Watawala hujipa sifa hizi kwa kujifanya wao ndio wawezeshaji wa mataifa yao. Hujitukuza na kusema bila mimi jambo fulani lisingefanyika, bila mimi hii nchi haiwezi kuendelea, hakuna mwingine kama mimi anayeweza kuongoza. Ilhali inafahamika kuwa Watawala hawana uweza isipokuwa uwezo wa kuongoza watu. Tunajua Rais/ Mfalme huongoza kwa kushirikiana na wananchi wake, bila kushirikiana Rais au Mfalme hawezi kufanya jambo lolote.Na hivyo hana UWEZA bali anaouwezo. Marais waliojitia wao wana uweza badala ya uwezo wengi wao walionja joto la jiwe. Hivyo Rais, Mhe. Samia Suluhu jihadhari na hili, wewe ni mtu kama watu wengine, huna la ziada isipokuwa majaliwa ya Mungu ndio yamekufanya uwe Rais. Sasa sio umepewa Lift alafu unataka kubonyeza na Honi kabisa. Mungu akikupa Lift muache yeye ndio apige Honi.
2. Umilele
Sifa nyingine ya Mungu ni Umilele, tangu na tangu. Mungu ndiye mtawala milele zote. Wapo viongozi wakishapewa madaraka hujiahau na kujiona kuwa wataishi na kutawala milele. Mifano yao ipo, ni kama Mfalme Nebukadreza, na Mfalme Belteshaza mwanaye ambao nao walipokalia viti walidhani watatawala milele, hivyo wapambe wao, na wasaidizi wao kila uchwao waliimba Mfalme uishi milele, sijui utawala milele, wote waliangamia kabla ya wakati wao.
Kutaka kutawala milele ni kukufuru, ni kujipa sifa ya Mungu, ni uchu wa madaraka. Ni kumchokoza Mungu, na wote tunajua ukimchokoza Mungu nini kinafuata.
Mhe. Samia suluhu, jihadhari wewe mwenyewe na kutaka mambo usiyo yaweza yatakayokugharimu wewe mwenyewe, pia jihadhari na wapambe wote watakaojifanya wanataka utawala milele kwani lengo lao ni kukufitinisha na Mungu wako. Wapambe wote waliotaka Wafalme/ Marais watawala milele hawakuwa na nia nzuri bali walijali maslahi yao na kumfitinisha mtawala na Mungu Mkuu.
3. UFALME WA WAFALME
Sifa ya Mungu pia ni ufalme wa wafalme, mkuu wa wakuu. Watawala wanaojipa sifa hii hujifanya wao ndio wafalme bora au marais bora kuliko waliowahi kutokea, hujitukuza na kujisifu kuwa wao ndio viongozi bora na wala hapana na hapatakuja kutokea kama wao. Sifa hizi niza Mungu. Mtu yeyote anayejitukuza hivi huchukua umungu mtu na anavunja kanuni isemayo, Ajikwezaye hushushwa na ajishushaye hukweza'
Hii pia aliifanya Nabii Eliya kama sijakosea, alipoulizwa na Mungu unafanya nini hapa, akajibu amemkimbia Yezebeli kwani anataka kumuua, Eliya anaongeza kumwambia Mungu kuwa, yeye ndio Nabii pekee aliyebaki pale Israel anayemtumikia Mungu wa kweli ni yeye pekee. Hapo Mungu akamwambia kuwa asiseme hivyo kwani wapo Manabii zaidi ya 400 ambao hawamtumikii Baali, isipokuwa Mungu wa kweli(yeye). Kauli ya Nabii eliya ni kujitukuza, na kujipa utukufu kuwa yeye ndiye mwema pekee aliyebaki, lakini Mungu anamuambia wapo wema wengi zaidi ya 40o.
Somo hili linawafunza wale wenye tabia ya kujiona bora kuliko wengine, wanaojiona wafalme wa wafalme, ati wao pekee ndio waliobaki na hakuna kama wao. Mhe. Samia lazima ujichunge na fikra za namna hii ni hatari kwani zimeshawagharimu waliowahi kutawala hapo zamani na hata sasa.
4. UKAMILIFU ASIYEKOSEA
Mungu anasifa ya ukamilifu asiyekosea, mwanadamu ni mkamilifu anayekosea kwa sababu ya Free will ya kuchagua wema na ubaya. Mwanadamu akichagua Ubaya ni mkamilifu kwenye ubaya, akichagua wema ni mkamilifu kwenye wema. MUNGU ni mkamilifu asiyekosea kwani yeye hana uchaguzi yeye anachofanya ndio hicho hicho, hapaswi kuchagua kwa sababu vyote ni vyake.
Wapo watawala wanaojipa sifa ya MUNGU kuwa nao niwa KAMILIFU wasiokosea, hivyo hawataki kukosolewa ilhali wanakosea kila uchao. Watawala wa hivi hujikuta katika udikteta mkubwa usiomithilika. Wengi waliishia kuangamia. Mhe. Samia Suluhu Rais wetu, wewe ni Mkamilifu unayekosea, hivyo lazima ukoseapo ukubali kukosolewa ili usijikute katika wakati mgumu na kuingia katika shimo la Udikteta. Mwisho ukaanza kudhuru watu.
5. JUU YA SHERIA
Mungu yupo juu ya Sheria kwa sababu yeye ni muweza wa yote. Lakini sisi binadamu wote tupo chini ya sheria, "Rule of Law; no one is above the laws" Watawala washenzi wapatapo nafasi ya Ufalme au Urais hujipa sifa ya umungu kuwa wao wapo juu ya sheria, wanaweza kuvunja sheria yotote ile na hakuna wakuwafanya kitu, wengine huamua kuua watu wengine pasipo kufuata sheria, kuvunja sheria waziwazi pasipo hofu kwani wao ni mungu. Watu hawa hujikuta katika vita ngumu kwa vita hiyo wanapigana na Mungu pasipo wao kujua.
Embu tusome kisa hiki hapa tuone mfano wa viongozi wa namna hii wanaojifanya miungu, na kile Mungu anachowafanyaga;
Ezekiel 28:
1. Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia: 2. “Wewe mtu! Mwambie mfalme wa Tiro kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi:
Wewe una kiburi cha moyo,
na umesema kwamba wewe ni mungu,
kwamba umekalia kiti cha enzi cha miungu,
umekaa mbali huko baharini.
Lakini, wewe ni binadamu tu wala si Mungu,
ingawa wajiona kuwa una hekima kama Mungu.
3. Haya! Wewe wajiona mwenye hekima kuliko Danieli,
wadhani hakuna siri yoyote usiyoijua.
4.Kwa hekima na akili yako
umejipatia utajiri,
umejikusanyia dhahabu na fedha
ukaziweka katika hazina zako.
5. Kwa busara yako kubwa katika biashara
umejiongezea utajiri wako,
ukawa na kiburi kwa mali zako!
6. Kwa hiyo mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi:
Kwa vile unajiona mwenye hekima kama Mungu,
7. basi nitakuletea watu wageni,
mataifa katili kuliko yote.
Wataharibu fahari ya hekima yako
na kuchafua uzuri wako.
8.Watakutumbukiza chini shimoni,
nawe utakufa kifo cha kikatili kilindini mwa bahari.
9. Je, utajiona bado kuwa mungu
mbele ya hao watakaokuua?
Mikononi mwa hao watakaokuangamiza,
utatambua kuwa wewe ni mtu tu, wala si Mungu!
10. Utakufa kifo cha aibu kubwa
mikononi mwa watu wa mataifa.
Ni mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Aya hizo ni kisa kinachomhusu Mfalme wa Tiro aliyejipa sifa zote za Mungu kama nilivyozitaja hapo juu. Kilichotokea tunakijua, kwa wasiojua waendele kusoma hiyo aya mpaka mwisho.
Mtawala anapojifanya mungu wakati sio, kinachofuata ni kupewa mapigo mazito kabla ya kifo chake, kuweza kupewa balaa la njaa, magonjwa makubwa, vita, matetemeko miongoni mwa mambo mengine.
Jambo moja la Ku-note hapa ni kuwa Mfalme au Rais anapofanya haya, wale wote wanaomuunga Mkono nao huhusishwa katika mapigo hayo. Kwa wale walionyamaza japo hawakumsapoti huyo mtawala nao huonja joto japo sio kubwa kama wahusika wakuu..
Wafalme wengine walijifanya mungu wakaangamizwa ni pamoja na Farao wa Misri na wote tunajua kilichompata.
Somo hili, halimhusu Rais, Mhe. Samia Suluhu, bali linahusu viongozi wote katika nyanja mbalimbali za ngazi zote za maisha kuanzia Familia mpaka taifa.
Na hii ni sababu moja wapo ya watu wote waliotegemezi kwenye familia zao Kufa mapema. Unakuta yule mtoto au ndugu anayetegemewa na Ukoo ndio anakufa mapema kwa sababu ya watu kumgeuza kama Mungu mtu ilhali ni binadamu wa kawaida sana, na hata akifa mambo yanaweza kuendelea kama kawaida.
Ujumbe huu unahusu pia wale watu wote ambao wamebarikiwa na tegemeo la familia au ukoo, jitahidini kuwa humble, msijifanye ni miungu watu, mkikaidi nawahakikishia mtaishi miaka michache hapa duniani.
Wale wanaosema watu wazuri hawadumu wanakosea, kwani watu wengi waliowema huishi miaka mingi sana, hasa wakiwa humble wasiochukua nafasi ya Mungu, na kujigeuza miungu watu au kugeuzwa miungu watu na wale wanaowategemea.
Ulikuwa nami, Nyota ya Tibeli
Robert Heriel
Takon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Katavi