Ujumbe kwa wadai katiba mpya wote: Hakuna njia rahisi ya kupata katiba duniani

Ujumbe kwa wadai katiba mpya wote: Hakuna njia rahisi ya kupata katiba duniani

Prof Koboko

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2020
Posts
350
Reaction score
2,550
Katika hili naomba nieleweke kabisa kwamba katiba mpya si mali ya CHADEMA wala wanaharakati, ni mali ya watanzania wote wakiwemo wanachama wote wa CCM. Tusisikilize watu wachache wa taifa hili ambayo wanasema hakuna haja ya katiba sijui tusubiri kwanza.

Niwaambie wote tunaopigania katiba mpya ni kwamba duniani katiba mpya huambatana na matukio makubwa yakiwemo watu kuumizana na kupotezana hadi wengine kufungwa kwenye majela bila sababu za msingi. Mara nyingi walafi wa madaraka wasiopenda kupunguziwa madaraka yao ndio hua hawapendi kabisa mambo haya. Watanzania tupambane bila kujali kuna matukio gani yatatufuata lakini faida ni kubwa kuliko mbele udhaifu wa katiba iliyopo.

Tupambane, hata mwalimu Nyerere alikua akisikiliza wachache pale anapoona kuna umuhimu. Viongozi wetu wa leo wamejawa tamaa hawataki kabisa mambo haya na tusiwape nafasi ni bora tujaze majela yote Tanzania.

Leo watu wanalia na TOTO za kodi kwenye makato ya Miamala ya simu, wanalia na kuongezeka kwa gharama za LUKU,Pembejeo na mafu, hii ni kwa sababu ya watu wachache wasiojua maumivu ya wengine. Mtu moja kwa sababu ya udhaifu wa katiba iliyopo aliamua kujichagulia kundi lake la kulinda maslahi yake na ndilo linalotuumiza hivi sasa.

#KATIBA MPYA
#KATIBA MPYA
#DAI KATIBA MPYA
 
Mbowe aliwahi kuamrisha watu waandamane huku yeye akiwa Afrika kusini na familia yake kwa mapumziko , Lisu pia alipanga ya kwake huku yeye akiwa ubelgiji na Amsterdam wakiangalia waandamanaji kupitia BBC swahili katika TV,

Zito Kabwe yeye huandamana mitandaoni kama vile fb, Twitter na hapa JF, nyumbu wao huandamana barabarani matumbo mbele na matokeo yake huambulia kufungwa jela, kuvunjwa miguu na kupata ulemavu wa kudumu.

Kwahiyo kabla ya kuandamana ndugu zang naomba mkumbuke ule msemo unasema "Kila mchuma Janga, hula na Wakwao". Wanaoshauri maandamano hawatokuwa maandamanoni.
 
Back
Top Bottom