Ujumbe kwa wanachuo na wahitimu wanaodharau wenye elimu za chini

Huwezi kunidanganya chohote kwenye ulimwengu huu wenye internet, mmiliki wa facebook alipewa tu honorary degree kama ilivyokuwa kwa bill gates, wala hakuingia darasani...

Naona umesoma lakini hata internet huwezi kutumia,

View attachment 2410812
upo wrong mkuu, mark alisoma sema hakumaliza tu degree yake, yaani mark hawezi kua kundi la wasiopiga kitabu hata kidogo, mark alijua alichokua anafanya, huku wengi hatujui hata nini tunachofanya, hiyo doctorate Havard walimpa kama kurecognize kazi yake pia kama aliyewahi kua mwanafunzi wao
 
samaki ana mwendo wa kuogelea, farasi ana mwendo wa kukimbia, njiwa ana mwendo kwa kupaa .. elimu ni mwendo na huwezi kusema kisa samaki hawezi kukimbia kama farasi basi hawezi kuwa na mwendo.
Mkuu pesa inaokotwa ila degree haiokotwi.
 
tusijazane ujinga, shule ni muhimu sana kama tunataka kusonga, nyie mliokosa bahati ya kusoma basi wapeni fursa watoto wenu, shule sio vyeti maana hapa ndio panachanganya wengi, shule ni kile kinachobaki kichwani baada ya darasa
 
Huwezi kunidanganya chohote kwenye ulimwengu huu wenye internet, mmiliki wa facebook alipewa tu honorary degree kama ilivyokuwa kwa bill gates, wala hakuingia darasani...

Naona umesoma lakini hata internet huwezi kutumia,

View attachment 2410812
Wewe bwana ni famba hujui ata kupresent mada ikakubalika kwa watu ndo maana unapata upinzani mkali kwenye huu uzi wako jishitukie basi Kaka selemala.
 
Naona unajitekenya tu, Mark ali drop out chuo cha Havard, Degree aliyopata sio ya kusomea darasani kama wanafunzi wengine, yeye alipewa honorary degree baada ya kutoa speech + mafanikio yake.

Hizo degree za honorary degree hata mtu ambae hajaingia darasani anaweza pewa.

Pia kwa Muanzilishi wa facebook kwake degree haina faida (kwa mtazamo wake)

 
mkuu amini kwamba ujinga bado ni janga kwa Tanzania yetu hii!!, kikubwa ajikubali tu ana asimamie anayoamini ipo siku haohao wakiona matokeo utawaona wanakuja tena kujifanya wanamkubali
 
mkuu sawa ni kama umeamua kua mbishi tu, ila ukitoa mifano ya wasioenda shule, Mark ni irrelevant kabisa, huwezi kumfananisha na ngumbaru wa huko buchosa mkuu!
 
Swala la kusoma na kutokusoma ni Mambo yako tofauti Sana maisha ni jitiada zako na kumtanguliza mungu hakuna SoMo linaloitwA maisha lingekuwepo Kila mtu angesoma ili afanikiwe kimaisha na maisha na pesa Haina mwenyewe tufanye kazi kwa bidii na kumtanguliza mungu
 

huyu mletamada ni st 7,lakini kwa kutokujiamini kwako umeamua ututaje na wa form four!!!!sijui shida yenu watu wa degree huwa nini!!!
 
tusijazane ujinga, shule ni muhimu sana kama tunataka kusonga, nyie mliokosa bahati ya kusoma basi wapeni fursa watoto wenu, shule sio vyeti maana hapa ndio panachanganya wengi, shule ni kile kinachobaki kichwani baada ya darasa
Hivi umeweza ku comprehend ujumbe wa hii maada na kujua inawahusu kundi lipi ??
 
Hili jinga kisa eti linawazidi kipato wasomi wasio kua na ajira basi linajiona limeyaweza kweli.

Wewe kubali tu na kisha move on.
 
Wewe bwana ni famba hujui ata kupresent mada ikakubalika kwa watu ndo maana unapata upinzani mkali kwenye huu uzi wako jishitukie basi Kaka selemala.
NO RESEARCH, NO DATA , NO RIGHT TO SPEAK .... Endelea kubwabwajika maneno ya kanga, mimi nimeleta facts wewe unaleta maneno.

Muanzilishi wa Facebook aliacha chuo na kuikosa degree ya darasani, degree aliyopea ni kwajili ya mapinduzi kwenye ulimwengu wa teknolojia, alivyotoa tu speech akapewa.

Jua utofauti wa honoary degree na degree ya darasani, nafadhaika kukueleza hivi vitu mtu unaejiona ni msomi ila vitu hivi vidogo hata huvijui.
 
Ifike hatua wapumzisheni wasomi na masimango, yaan mtu akipata tu hela ya kubadirisha mboga akapata nafasi kwenye platform yoyote ni masimango tu kwa wasomi kwani ambao hawajasoma na wanapigika uko mtaani hawapo? Kama hustling zinakulipa usiwadhiaki waliosoma kama kusoma kunakulipa usiwadhiaki hustlers wote lengo letu ni kufanikiwa
 
mkuu sawa ni kama umeamua kua mbishi tu, ila ukitoa mifano ya wasioenda shule, Mark ni irrelevant kabisa, huwezi kumfananisha na ngumbaru wa huko buchosa mkuu!
Hivi kwa mfano kwenye hii maada huyo Mark nashangaa hata umemuingizaje ... Unaweza kutoa mfano wowote Mark Kadharau wenye elimu ya chini ??

Tunamuongelea Mark hapa, jamaa yupo very humble despite being a dropout who has been awarded a honorary degree from one of the best universities in this world, Sio kama mtu aliemaliza masters yake kwa kukariri anawaona wenye elimu za chini ni maji na yeye ni mafuta.. Did you even comprehend this post ama umeona kichwa tu umekimbilia ku comment ?
 
Kwenda tu Harvard inaonyesha ni kiasi gani mack alikua kipanga nazani unalijua hilo.

Anyway tuachane na mack wewe kama selemala mwenye kagari uliyejaa ulimbukeni elewa basi elimu ni muhimu.
 
Kwenda tu Harvard inaonyesha ni kiasi gani mack alikua kipanga nazani unalijua hilo
Narudia tena kukuuliza swali, Humu ndanimarrk umemuingizaje, Maada inazungumzia baadhi ya wasomi wanaodharau wenye elimu za chini, ni vipi umemweka Mark humu ambae hana dharau kwa wenye elimu za chini kiasi kwamba kaajiri hata wasio na degree kwenye kampuni yake ??
Anyway tuachane na mack wewe kama selemala mwenye kagari uliyejaa ulimbukeni elewa basi elimu ni muhimu.
Elimu ni muhimu, Bila elimu dunia itajaa matatizo hii,

Kujifunza upishi ni elimu bila hii elimu tutaishia kula mapera,

Kujifunza hesabu ni elimu ukishindwa hutaweza hata kutoa chenchi,

kujifunza kuishi na watu ni elimu bila hivyo huta changamana vizuri wenye jamii,

kujifunza useremala ni elimu bila hivyo watu watakaa kenye mawe badala ya viti,

kujifunza biblia / korani ni elimu bila hivi watu watadhani uzinzi hauna madhara.

kujifunza kiingereza ni muhimu, bila hii elimu hata vitu vyepesi kwenye google utashindwa kuvielewa

Binafsi hata baada ya kufeli form 4 niliweza kujielimiesha kiingereza, useremala, coding, driving, bible, n.k. na bado naendelea kujifunza mengi hasa humu jamiiforums,
 
ok nimekupata mkuu
 
Very arrogant fellow, Jua kutofautisha akili na uwezo wa kujibu mtihani darasani.
Kwa majibu yako naona Kuna kitu umekikosa maishani na kinakusumbua. Maana hii Mada unaikomalia sana na wala hakuna anayekudharau.
Ulipania sana kufaulu ukakwama sasa kila aliyekuzidi elimu unaona anakudharau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…