N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 7,427
- 10,905
Waziri Ndugulile najua umechukua hii Wizara hivi karibuni. Baada ya kusimamia suala la vifurushi vizuri; nashauri sasa ugeukie Vibao vya Anuani za Makazi ili tuwe na mfumo rasmi wa utambuzi wa Makazi na zoezi hili liwe la lazima na liwe na vibao vya udongo inavyofanana kote nchini ili tuwe na utaratibu rasmi wa utambuzi wa makazi.
Katika hili nashauri majina ya mitaa utaratibu uwe ni makubaliano ya serikali ya mtaa kuhusu majina ya mitaa badala ya watu wachache kujimilikisha majina ya mitaa.
Aidha barabara za mitaani zilizowekwa mageti ya machuma kuzuia watu kupita huko yaondolewe kwa kuwa barabara sio mali ya watu binafsi wa mtaa huo ni mali ya umma.
Nawasilisha.