Ujumbe kwa wizara ya Afya-Sitisho la misaada ya Marekani lazua Taharuki

Ujumbe kwa wizara ya Afya-Sitisho la misaada ya Marekani lazua Taharuki

TrueVoter

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2008
Posts
3,034
Reaction score
3,032
Wiki hii taarifa kutoka shirika la misaada la USAid kwenda kwa Taasisi mbalimbali ikiwemo Taasisi ya Benjamin Mkapa juu ya kusitisha ufadhili wa miradi inayohudumia waathirika wa ugonjwa wa UKIMWI na Magonjwa ya kuambukiza ikiwemo TB limeleta taharuki hasa kwa wagonjwa wanaohudumiwa na mradi huu kupitia Hospitali mbali mbali nchini. Ningependa kuuliza maswali yafuatayo kwa Wizara ya Afya..

1. Je ni kweli serikali imeridhia huduma za kuhudumia wagonjwa wa ukimwi waliokuwa chini ya miradi inayosimamiwa na Taasisi ya Benjamini Mkapa isimamishwe?

2. Ni kweli serikali imeridhia waliokuwa wafanyakazi chini ya Taasisi ya Benjamin Mkapa kuhudumia wagonjwa wa ukimwi wasimame kufanya kazi?

3. Taasisi ya Benjamin Mkapa na washirika wengine wa maendeleo wanaisaidia serikali jukumu la kutoa huduma kwa wagonjwa wa ukimwi, kuna mpango upi kuendelea kutoa huduma hizi zilizokuwa chini ya Taasisi ya Benjamini Mkapa..

Kwa hali ilivyo kufuatia mabadiliko ya uongozi nchini Marekani ni vyema na muhimu kujenga utamaduni wa kuwa na mpango wa dharula pale inapotokea hali km hii ya kusitisha ufadhili wa miradi ya maendeleo kwa ghafla km ilivyotokea ili kufanya miradi iendelee km ilivyopangwa angalau kwa kipindi cha siku 90 wakati serikali inaangalia namna nyingine ya kusimamia matibabu kwa wagonjwa kulingana na uwezo uliopo.

Huduma za wagonjwa wa ukimwi zinatolewa kwa upekee kwa sababu nyingi za kitabibu na hivyo sioni km itafaa kuzirejesha kwenye muundo wa zamani yaani zitolewe sabamba na huduma za magonjwa mengine, ikifanyika hivyo itakuwa ni kutengeneza tatizo kubwa sana ambalo madhara yake yatakuwa na gharama kubwa kwa nchi! Asante..!
 
Nioneshe top officials wa chama au serikali anayetegemea msaada. Ndio utajua kwanini haiwaumi
 
Back
Top Bottom