Ni ujumbe kuntu kabisa huu. Nawashauri viongozi wa Chadema hasa Mwenyekiti Mbowe na Makamu wake Tundu Lissu wakae waone namna ya kufanya damage control ya kinachoendelea sasa ndani ya Chadema. Tuhuma anazotoa Tundu Lissu zina mashiko na kama zikafanyiwa kazi na Chama kikaja na tamko la pamoja la jinsi gani zimefanyiwa kazi na wakosaji wakashughulikiwa chama kitapona. Kukaa kimya kwa Mwenyekiti akiamini kuwa tuhuma hizi zitapita kama upepo ni kujidanganya.
Na kwa upande mwingine Tundu Lissu kuendelea kutupa mawe haya japo yana ukweli ajue kwamba anaifanyia kazi kubwa CCM ya kuimaliza Chadema tena bila ya malipo yoyote. Nimeona hata hapa jukwaani jinsi anavyoshangiliwa na wana CCM siyo kwa vile wanampenda bali kwa vile anawasaidia kufanya kazi ambayo imekuwa ngumu kwao kwa muda mrefu tena kwa gharama kubwa sana lakini haikuzaa matunda tarajiwa, lakini kwa hali iliyofikia ni kama wamerahisishiwa kazi kwani kazi hiyo inafanywa na Chadema wenyewe.
Nasikitika sana kama Tundu Lissu halioni hili kuwa anawasidia watesi wake kuimaliza Taasisi ambayo ameshiriki kuijenga kwa damu na jasho lake. Kwa msimamo wake wa kuyasema anayosema hadharani na kwa ukimya wa Mwenyekiti bila kukalishana chini na kuweka msimamo wa pamoja naona kabisa Chadema ikifuata njia ya NCCR Mageuzi.