Ujumbe wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kuhusiana na mwenendo wa ugonjwa unaosababisha 'Changamoto ya Upumuaji'

Hata na nyie ni walewale tu waoga.Mnashindwa kisema tu kwamba kuna korona?Hata njia za kujikinga mlizotoa ni za kujikinga dhidi ya korona.Muache uoga nyie bwana.
Hii nchi yetu ina laana. Kila mtu ni mwoga. Tamko halijulikani lina lenga nini? Madaktari wanahimiza watu kutumia dawa za asili! Ujinga wa karne huu.
 
Magrupu niliyojounga na kuungwa ya WhatsApp Yana michango ya misiba wengi wakipoteza wazazi wao
 
Hapa hakuna uwazi wowote. Naona tamko limetolewa kiwoga woga na hata hailieleweki dhumuni lake ni nini. Hivi kweli na madaktari wanatoa tamko la aina hii?
Kwa level yao inatosha wasije wakapoteza kazi zao bure kama yule professor
 
Acha kujitoa ufahamu wewe! Hivi lini Tanzania kulikuwa na vifo vingi kiasi hiki hadi Watanzania wengi kuwa na hofu kubwa kiasi hiki?
Changamoto la upumuaji lipo miaka mingi sana. Ni ugonjwa unaoshika nafasi ya pili kwa kuua baada ya Malaria. Hata bila covid lilikuwepo. Fuateni taratibu za kujikinga badala ya kuleta ushabiki
 
Huu uandishi ni matokeo ya utawala unaoficha maradhi ya covid kiasi kwamba wataalamu wanashindwa kuelezea gonjwa husika moja kwa moja na kwa uzito wake.

Magu hakufaa kabisa kuwa kiongozi
 
Wanazunguka kweli kusema huo ugonjwa ni Uviko au laa kwani kuna kigugumizi gani ili hali dunia yote inapitia changamoto hii?
Jamii yetu imejengeka katika woga na unafiki. Madakatari na wasio madaktari, wote tunanajua tatizo tulilo nalo, lakini madaktari wanaandika kwa kuzunguka, sawa na wale wanasiasa uchwara.

Bado tuna safari ndefu ya namna ya kuifanya elimu utupe uhuru wa kunena.
 
Acha kujitoa ufahamu wewe! Hivi lini Tanzania kulikuwa na vifo vingi kiasi hiki hadi Watanzania wengi kuwa na hofu kubwa kiasi hiki?
Ni tz pekee ndio watu wanakufa?
 
Leo kati ya mabandiko ya kisenge kuwahi kuandikwa na hili ni moja wapo.

Uwandishi mbovu sana ambao unauoga ndani yake.

Ugonjwa wa changamoto ya kupumua....wakati huo huo wanasema changamoto ya kupumua siyo ugonjwa bali ni dalili za awali....qumanina zao kabisa.

Wameacha kutumia taaluma zao kuokoa watanzania wengi, wanatumia taaluma zao kuwajaza matumbo wanasiasa.

Covid haiishi leo wala kesho, ipo na itaendleea kuwepo, cha muhimu tujue jinsi ya kuishi nayo, tofauti na hapo ni ubatili mtupuuuuu....

Chama cha madaktari na viongozi wenu, tumieni akili zenu na utashi wenu mkiwa na hofu ya Mungu ndani yenu na siyo woga wa kifukuzwa kazi kwa kusema ukweli.
 
Wameamua kuchimoa betri sasa na kuweka wazi kuhusu corona
Hakuna sehemu yoyote ya waraka yenye msisitizo kuwa ujumbe unahusu Korona ila wameelzea changamoto ya kupumua na magonjwa mengine ya mlipuko yanavyoweza kupata upenyo katika sintofahamu.

Usiwalishe maneno yako unayotamani kila wakati uyasikie kwa kufurahisha mtima wako.

Wote wanaoshabikia ugonjwa huu ndio watakaonaswa nao. Utasubiri wengine unaotamani wapate lakini kila jitihada ukizifanya kuombea hivyo unabadili mwelekeo na kuja kwako au jamaa wako wa karibu kwa hiyo chuka maandishi haya yasikutie kitanzi.

Waraka unagusia watu welio hatarini kukumbwa na changamoto ya kupumua ni wale wenye magonjwa sugu kama kisukari, ugonjwa wa moyo, figo, ini, kansa, vvu,Pneumonia nk.

Kila mtu achukue tahadhari dhidi ya magonjwa ya aina zote na kubadili mfumo wa maisha yenye kuvuta mazingiara hatarishi kwa afya.

Acha sisa kwenye mambo ya msingi yanayohusu uhai wa watu.
 
Nawashauri wazee wa road trip kuelekea vijijini ili upepo huu upite kwanza huko Mjini.

Kama ilivyofanyika Mwaka jana, si mnakumbuka?
 
At least wameongea, na wenye kusoma between the lines wataelewa, na wasiotaka kuelewa nao vilevile..., ingawa hii diagnosis ya Ugonjwa unaosababisha changamoto za kupumua imekaa kisiasa zaidi na sio kidokta dokta..., na haya ni maendeleo ya awamu ya tano. politics na propaganda kwenye kila kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…