VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Nawaambia haya, kwa uzoefu wangu ndani ya Serikali, CCM na kwenye Idara Nyeti za nchi hii. Nisikilizeni na muelewe:
1. Uchaguzi mkuu wa Tanzania ni zaidi ya uchaguzi kati ya CCM na vyama vya upinzani. Uchaguzi hubeba mustakabali wa nchi kiusalama, kiuchumi na kadhalika. Kuuchezea uchaguzi ni kuyaweka mamabo hayo rehani. Haijawahi kuwa rahisi au kuruhusiwa na Jumuiya ya Kimataifa na hata vyombo vyetu vya ulinzi na usalama hapa nchini kuhatarisha usalama na ustawi wa Taifa kwenye uchaguzi. Mshindi atapewa ushindi wake na hakutakuwa na uminywaji wowote wa demokrasia wala kuchezea matokeo yoyote.
2. Wakati wa uchaguzi mkuu, vyombo vyetu vyote vya ulinzi na usalama huitazama Tanzania kwa ujumla wake na mustakabali wake. Vyama vya siasa hutazamwa kama nyongeza tu. Vyombo husika huwa na mtazamo wa kitaifa huku ikiweka kando kwa muda uwepo wa CCM,CHADEMA,CUF,NCCR, ACT na kadhalika. Vyama vitapita, Tanzania itabaki. Nawaambia, mshindi kwenye sanduku la kura atatangazwa na kupewa ushindi wake.
3. Kusema kuwa ubabe na vitisho vitatumika uchaguzini ni kujitisha wenyewe kama wagombea na wapigakura. Rejeeni na mtafakari vya kutosha kuhusu 1 na 2 hapo juu.
4. Ni wazi kuwa CCM, kwa miaka mitano, imefaidi matayarisho makubwa na ya peke yake ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Hilo limewapa kiburi kikuu viongozi wa chama na hata wagombea watarajiwa kuwa CCM itazoa viti vyote vya Ubunge na Udiwani na hata cha Urais. Hilo halitatokea. Wapo wagombea wa Upinzani wanaokubalika pamoja na kukosa maandalizi ya kiuchaguzi. Wakigombea na kushinda, watapewa ushindi wao. Tena, haitatokea Tanzania kudhibitiwa na chama kimoja tena.
5. Hakuna haja ya kujaa hofu. Hakuna haja ya kuingia kinyonge kwenye uchaguzi mkuu. From a distance, God is watching. From within and without, international community is watching. Tanzania si kisiwa pweke linapokuja suala la haki na amani.
Kwanini makada wengine wanakatazwa kuchukua Fomu ya Urais wa JMT hapa Dodoma?
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dodoma