Uchaguzi 2020 Ujumbe wa wazi kwa wanademokrasia Tanzania: Uchaguzi uwe huru na wa haki au la, washindi watapewa ushindi wao. Hakuna haja ya kuwa wanyonge!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Nawaambia haya, kwa uzoefu wangu ndani ya Serikali, CCM na kwenye Idara Nyeti za nchi hii. Nisikilizeni na muelewe:

1. Uchaguzi mkuu wa Tanzania ni zaidi ya uchaguzi kati ya CCM na vyama vya upinzani. Uchaguzi hubeba mustakabali wa nchi kiusalama, kiuchumi na kadhalika. Kuuchezea uchaguzi ni kuyaweka mamabo hayo rehani. Haijawahi kuwa rahisi au kuruhusiwa na Jumuiya ya Kimataifa na hata vyombo vyetu vya ulinzi na usalama hapa nchini kuhatarisha usalama na ustawi wa Taifa kwenye uchaguzi. Mshindi atapewa ushindi wake na hakutakuwa na uminywaji wowote wa demokrasia wala kuchezea matokeo yoyote.

2. Wakati wa uchaguzi mkuu, vyombo vyetu vyote vya ulinzi na usalama huitazama Tanzania kwa ujumla wake na mustakabali wake. Vyama vya siasa hutazamwa kama nyongeza tu. Vyombo husika huwa na mtazamo wa kitaifa huku ikiweka kando kwa muda uwepo wa CCM,CHADEMA,CUF,NCCR, ACT na kadhalika. Vyama vitapita, Tanzania itabaki. Nawaambia, mshindi kwenye sanduku la kura atatangazwa na kupewa ushindi wake.

3. Kusema kuwa ubabe na vitisho vitatumika uchaguzini ni kujitisha wenyewe kama wagombea na wapigakura. Rejeeni na mtafakari vya kutosha kuhusu 1 na 2 hapo juu.

4. Ni wazi kuwa CCM, kwa miaka mitano, imefaidi matayarisho makubwa na ya peke yake ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Hilo limewapa kiburi kikuu viongozi wa chama na hata wagombea watarajiwa kuwa CCM itazoa viti vyote vya Ubunge na Udiwani na hata cha Urais. Hilo halitatokea. Wapo wagombea wa Upinzani wanaokubalika pamoja na kukosa maandalizi ya kiuchaguzi. Wakigombea na kushinda, watapewa ushindi wao. Tena, haitatokea Tanzania kudhibitiwa na chama kimoja tena.

5. Hakuna haja ya kujaa hofu. Hakuna haja ya kuingia kinyonge kwenye uchaguzi mkuu. From a distance, God is watching. From within and without, international community is watching. Tanzania si kisiwa pweke linapokuja suala la haki na amani.

Kwanini makada wengine wanakatazwa kuchukua Fomu ya Urais wa JMT hapa Dodoma?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dodoma
 
Very True yaani kuchezea uchaguzi 2020-2025 ni kuhatarisha uchumi wa nchi na hali itakuwa tofauti sana nawaambia uwenda tukakosa hata pesa za kuwalipa wanajeshi, polisi kwa vikwazo.
 
Very True yaani kuchezea uchaguzi 2020-2025 ni kuhatarisha uchumi wa nchi na hali itakuwa tofauti sana nawaambia uwenda tukakosa hata pesa za kuwalipa wanajeshi, polisi kwa vikwazo.

Ikitokea hivyo maana yake Tanzania Mpya itazaliwa bila shaka.
 
Kama Daudi tuko tayari kupambana na Goliath.
We shall overcome. Amen
 
MkuuMkuu andiko lako limeshiba barikiwa sana
 
Very True yaani kuchezea uchaguzi 2020-2025 ni kuhatarisha uchumi wa nchi na hali itakuwa tofauti sana nawaambia uwenda tukakosa hata pesa za kuwalipa wanajeshi, polisi kwa vikwazo.
Kukosa pesa chini ya JPM haiwezekani kamanda!
Labda kama tutachagua wanywa FARU JOHN.
 
Usiwe na wasiwasi mzee. Uchaguzi utaendeshwa kama kipindi kile ulipokuwa ukipata uzoefu kwenye nafasi nyeti serikalini na CCM.
 
Wakati wa uchaguzi mkuu, vyombo vyetu vyote vya ulinzi na usalama huitazama Tanzania kwa ujumla wake na mustakabali wake. Vyama vya siasa hutazamwa kama nyongeza tu. Vyombo husika huwa na mtazamo wa kitaifa huku ikiweka kando kwa muda uwepo wa CCM,CHADEMA,CUF,NCCR, ACT na kadhalika. Vyama vitapita, Tanzania itabaki. Nawaambia, mshindi kwenye sanduku la kura atatangazwa na kupewa ushindi wake.

Looh hili halijawahi kutokea. Eti ni lini hili lilitokea. Kwamba Policcm wawe polisi kabisa? Hawatavalisha magwanda ya jeshi lao wale wa kijani tena? Na wale wa kijani waliokuwa wanavamia wapinzani mbele ya police watakuwepo? Je watathibitiwa?
 
From a distance, God is watching. From within and without, international community is watching
VUTA-NKUVUTE unajua katika watu ninao waamini kujenga hoja you are among them! Sasa mbona unaniangusha? You should not jeopardise your intellectual integrity!
Back to your submissions: From a distance, God......... nchi zote ambazo zimeingia kwenye vita hivyo vitu viwili havikuwepo? From world history, Dictators never heed to "mere word" unless external physical force is used! like in the case of Yahayah Jameh, short of that Jameh would have assumed power!
 
Tupatupa napenda copy ya bandiko lako umtumie Ndugai.
 
Ikitokea hivyo maana yake Tanzania Mpya itazaliwa bila shaka.
Hakuna, kuna limitation myfriend, mkifurukuta sana mtapewa kwenye Ubunge na Udiwani, lakini kwenye lile jumba jeupe TISS huwa wanashirikiana na CCM kuwasaidia wasiumbuke.
 
Mzee Tupatupa mtihani wa hesabu za darasa la 7 wamepewa Vyama pinzani,lakini cha kusikitisha CCM wamepewa mtihani wa hesabu wa darasa la chekechea na wapewa msaada wa Mwalimu bingwa.
 
Very True yaani kuchezea uchaguzi 2020-2025 ni kuhatarisha uchumi wa nchi na hali itakuwa tofauti sana nawaambia uwenda tukakosa hata pesa za kuwalipa wanajeshi, polisi kwa vikwazo.

Polisi, TISS, time, wakurugenzi, n.k Ni Watanzania pia na Wana Ndugu zao. Sasa Hawa Ffu wakiumiza mkoa huu, kule wenzao wamekuumizia Ndugu zako...patamu hapo...mzunguko unaendelea.

Vyombo vya Dola Sio machuma au computer...Ni watu na Wana moyo wa nyama... nafsi zinawasuta...sio wote watapokea amri za kuumiza na wakatekeleza. Yetu macho..

Na mataifa yanatufatilia, tutapigwa vikwazo na tutakosa misaada, NA Tutakosa heshima Duniani...

Tutakosa washirika wa biashara.
 
Uchumi utaanguka, Mishahara na posho Hakuna...Hakuna pesa kugharamia elimu...wachezee tu uchaguzi...uwezo wanao..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…