WANABODI.
IFUATAYO NI SEHEMU YA HOJA YA MBUNGE STEPHEN KAHUMBI KATIKA KIKAO CHA 41 CHA MKUTANO WA 16,MAJADILIANO YA BUNGE -BUNGE LA TANZANIA.TAREHE 5-08-2004.
MASWALI NA MAJIBU NAMBA 385. UKURASA 43 HADI 46.
NAMKUU.
"Kwanza naomba niombe Mungu anisaidie kwa sababu tangu nimeingia kwenye bunge hili, sijazungumzia habari kama ninayotaka kuizungumza hapa, kwa hiyo ni mara yangu ya kwanza kuzungumzia habari ya idara.
Mheshimiwa spika kazi yetu wabunge ni kushauri na siyo kutafuta malumbano, hatutaki kulumbana na mtu, hatutaki kulumbana na waziri wala hatulumbani na wafanyakazi wa idara.
29-julai 2004-Hotuba ya waziri wa kazi, maendeleo, vijana na michezo mimi nilitoa maelekezo kuhusu mfanyakazi wa TRA, ALIYEFUKUZWA KAZI MBEYA akapeleka suala lake baraza la usuluhisho la mkoa mbeya akashinda, TRA hawakuridhika kwa kushindwa na mwanamke, waka appeal wizara ya kazi na maendeleo, vijana na michezo.
kwa vile wizara ya kazi inajua vizuri sheria za kazi wakatoa uamuzi kwamba tuhuma walizomtuhumu hazikuthibitika
. kwa hiyo arudishwe kazini- mtu huyo hakurudishwa, nimeongea na waziri Mramba na commissioner wa TRA juu ya jambo hili lakini bado hakuna ufumbuzi.
na suala hili limeandikwa kwenye Hansard ya 29-07-2004.
Mheshimiwa spika cha kushangaza watu wa TRA wanaona kama mimi nina confrontation nao. leo wameniletea barua kwa Ems, ambayo haina ukweli wowote, ninasikitika ninayo hapa yaani baada ya kusikia tumezungumza humu(bungeni) wakakaa kule Dar-es-salaam, kupinga Bunge barua hii imeandikwa 2-08-2004. mimi nilizungumza tarehe 29-07-04. hii ni kukujulisha kuwa msimamo w mamlaka ya mapato (TRA), ni kuwa haikubaliani na maamuzi ya baraza la usuluhishi Mbeya au ya waziri yaani waziri wa kazi , maendeleo, vijana na michezo anadhalauliwa na commissioner wa TRA maana yake nini? tuna serikali ngapi?
mheshimiwa spika huwezi ukaacha mtu anaonewa kwa kuvunja sheria kwa sababu mtu hajui sheria, mfanyakazi wa serikali huwezi ukamhukumu kwa sheria ya wafanyakazi wa ofisi za watu binafsi, kama unamchukia ondoka wewe,
HATUWEZI KUVUMILIA WATU WANAONEWA KWA SABABU YA UBAGUZI ,UKABILA AU NINI HAIWEZEKANI, KWANINI BUNGE LINADHAULIWA KIASI HIKI NA TUNARUHUSU?".
wanabodi kazi kwenu bunge linadhauliwa nini sisi kina mswahili? tizameni muone nini tunasema.WATU wamelumbana na bunge na tumeona hapo kuwa kuna ubaguzi wa kikabila.na walitoa hoja ni wabunge anayebisha afuate hiyo ripoti.