Kwa vile mjadala huu utaendelea bila kukoma na ndugu zetu watetezi wa Ukabila wanaendelea kumwaga "data" nimeamua kuweka manyanga chini na kuwaacha ndugu zetu hawa washinde. Hata hivyo, kwa vile wao wanalijua tatizo hili kwa undani, nimeamua kupendekeza tume* ambayo ije na mapendekezo ya jinsi ya kuondoa ukabila huo TRA. Badala ya wao kuendelea kulalamika na kutugongelea kama msumari hii hoja ya ukabila nina uhakika watakuwa na nia na kusudi la kuamua kuondoa tatizo hilo.
WAJUMBE WA TUME
Mswahili - Mwenyekiti
Dua- Katibu
Mzee ES
Chinga
Mkuu
Mkandara
Jamberi
WAJUMBE WA ZIADA
Mtu yeyote ambaye amekubali kuwa kuna ukabila TRA anaruhusiwa kushiriki katika mijadala ya tume hii teule.
JUKUMU LA TUME
Jukumu la Tume hiyo litakuwa ni kutoa mapendekezo ambayo endapo yatatendewa kazi na wahusika yatasaidia katika kuondoa ukabila wa Wachagga kwenye taasisi nyeti ya Mamlaka ya Mapato.
UWEZO WAKE
Tume itakuwa na uwezo ufuatao:
Katika utekelezaji wa jukumu lake kuu, tume itakuwa na uwezo wa kupendekeza jambo lolote lile ambalo litapunguza na kuondoa kabisa ukabila wa wachagga kwenye Mamlaka ya Mapato. Tume haitakuwa na uwezo wa kupendekeza jambo lolote kuhusu ukabila wa makabila mengine kwenye taasisi hiyo wala kutafuta ushahidi wa kuwepo ukabila wa aina hiyo.
MIPAKA YAKE
Tume katika kutekeleza majukumu yake haitakuwa na uwezo wa kuita na kuhoji mashahidi, kutafuta ushahidi wa ukabila (kwani imeshabitishiwa kuwa upo) wala kumtaka Mwanakijiji awahoji wahusika, kwani sababu ya kufanya hivyo haipo.
MAMBO YA KUZINGATIA
Katika kutoa mapendekezo ya kuondoa ukabila TRA tume itapaswa izingatie yafuatayo:
- Mapendekezo hayo yatahusu ukabila wa Wachagga hapo TRA peke yake na si kwingineko
- Mapendekezo hayo yatapunguza idadi ya Wachagga TRA
- Mapendekezo hayo yatahakikisha Wachagga hawashiki nafasi yoyote nyeti kwenye taasisi hiyo
- Mapendekezo hayo yatasababisha waombaji wa kazi kutoka makabila mengine wanaongezeka TRA
- Mapendekezo hayo yatahakikisha kuwa hakuna Mchagga mwenye ndugu TRA atakayeajiriwa huko
- Mapendekekezo hayo yatahakikisha kuwa watu wa makabila mengine wanaweza kuajiri ndugu zao kama hawafanyi hivyo bado huko TRA
- Mapendekezo hayo yataharakisha kuondolewa kwa Wachagga wengi TRA ili kulinda usalama wa Taifa
- Mapendekezo hayo yataharakisha kuajiriwa kwa watu wa makabila mengine TRA hasa watu kutoka pwani na kupewa nafasi nyeti
- Mapendekezo hayo yatahakikisha kuwa mtanzania Mchagga hatabaguliwa kwa misingi ya ukabila wake TRA
MUDA WA TUME
Tume itapewa wiki moja kuanzia tarehe 12/03/2007 hadi 18/03/2007 ili kufanya mjadala wa hoja zake hadharani kwenye Jamboforums. Wanajambo Forums ambao hawakubali kuna ukabila na wamekubali kushindwa kwa hoja watakaa kimya
BILA KUCHANGIA LOLOTE, na kuwaacha ndugu zetu hawa kuja na mapendekezo haya na hivyo kuondokana mara moja na daima na tatizo la ukabila wa Wachagga TRA.
JAMBO LA KUKUMBUKA
Tume haijaundwa ili kutafuta kama kuna ukabila wa Wachagga kwani hilo katika kurasa zaidi ya 70 limethibitishwa na wale wanauona ukabila huo.
NA TUME IANZE KAZI ZAKE MARA MOJA!
NB* Mamlaka ya kuunda tume nimejipachika na hamruhusiwa kuhoji iweje "mimi" niunde tume. Tunakaa chini sasa tuone nani "atamkoma nyani giledi!"