Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Dua, tatizo ni kuwa mnaotetea uwepo wa ukabila hamuhitaji uchunguzi kwani mmeshaamua kuwa upo!


Jibu la swali kama hili nilitoa hapa: http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=23186#post23186

Uchunguzi uliotoa na report ya NORAD nimekujibu utuletee terms of reference ya hizo report n.k. hapa:

http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=1867&page=66

Wakati Watanzania wanaendelea kuona mazingaombwe kuhusu ukabila ni jukumu letu kuwafahamisha wengine ambao bado wanalifumbia macho swala hili kwa namna moja au nyingine na hawataki ukweli uonekane.
 
mimi nakubaliana na wewe kuwa ukabila upo, au binafsi upo ila ninatofautiana na wewe kwa kusema "ili kujua kama kuna ukabila au udini tulinganishe idadi ya dini au kabila katika nyadhifa."
ukabila ni sababu moja ila kuna sababu nyingine nyingi zinazoleta utofauti wa idadi ya watendaji katika nyadhifa katika makundi mbalimbali
kumnyima mtu nafasi kwa sababu ya dini au kabila au kundi atokalo ni ubaguzi lakini vile vile kumpa mtu nafasi kwa sababu ya dini au kabila au kundi lolote ni ubaguzi pia.
hivyo tutakuwa tunafanya ubaguzi tukitaka kulinganisha idadi ya makabila au dini au makundi mbalimbali ndani ya nyadifa na wala hili haliwezi kutuletea maendeleo.tukianza kuteua watendaji sio kwa ushindani bali kwa kuangalia kulinganisha makundi tutaishia pabaya kwani ukilinganisha dini kutaibuka madhehebu ndani ya dini na kujiona utofauti.bado kuna dini za kijadi ambazo hazijafuata dini za kigeni nazo zitadai nafasi. Tanzania siyo nchi ya ukristo na uislamu tu hivyo ukitoa nafasi kidini lazima kila mtu katika dini yake apate nafasi.
Kuna makabila mngine mpaka sasa hivi hapa tanzania yako yanayoishi maisha ya porini ila itabidi uwatoe porini na uwape nyadhifa kubwa ili kuleta usawa wa kabila iwapo uaamua kuleta usawa wa kikabila.
ubaguzi unaondolewa kwa ushindani na yule aliyeoneka bora katika waliojitokeza kuwania nafasi hiyo, hivyo wanaweza kuwa wote kabila moja, wote dini moja wote jinsia moja ilimradi hawajawekwa kwenye nyadhifa hizo kutokana na makundi yao bali kutokana na ubora wao wa kuziba nafasi hizo, na hakuna walionyimwa kutokana na makundi yao

mjomba
kuna kitu kinaitwa SPACING ya PARAGRAPH...wengine macho mabovu hebu jitahidi basi mwinyi au unasemaje?

12_indent.jpg
 
mwanakijiji,

hebu kwanza tueleze wachagga ni asilimia ngapi ya watanzania, na utueleze katika hao wachagga, ni asilimmia ngapi wameenda shule kwa maana kwamba angalau wana ki-digrii, kisha utuambie hapo TZ wenye ki-digrii angalau kimoja ni asilimia ngapi, na utuambia wachagga walioajiliwa ni asilimia ngapi ya wana-jamhuri wote, ili mwisho tuamue kwamba, KATIKA WASOMI TZ. WACHAGA NI ASILIMIA FULANI NA KATIKA RAIA WOTE WALIO AJILIWA, WACHAGGA NI ASILIMIA FULANI

Hizi stori na historia za KUKARIRI kwamba kabila fulani ni wasomi zimepitwa na wakati, tunahitaji data na wenye nazo wazitoe ili kuthibitisha kwamba IDADI KUBWA YA KABILA FULANI KUSHIKA NAFASI NYETI INATOKANA NA WINGI WAO KATIKA JAMII AU WINGI WAO KATIKA JAMII ILIYOSOMA.

Kisha, kwa kuangalia jamaa yangu mmoja hapo juu aliposema TRA kuna wachagga 30% ya waajiriwa wote, hii ni alali au la?

Nijuavyo mie ni kwamba:

1. TZ kuna makabila zaidi ya 120

2 hakuna kabila lenye idadi kubwa ya watu TZ zaidi ya WASUKUMA, ambao hawazidi hata 15%

3 sitegemei zaidi ya 5% ya kabila fulani KUJIKUTA likiwa limeajiriwa kwenye taasisi moja, kwa hisabati rahisi tu ya probabilite, yaani chukulia MATUKIO yanatokea "randomly" na kwamfano wachagga waliosoma ni asilimia 3 ya wasomi wote TZ, natarajia kukuta asilimia inayoendana na hiyo kwa zaidi ya 95% POPOTE PALE PENYE AJIRA, kwa maana kwamba wachagga watakuwa ni asilimia 3 ya waajiriwa WA FANI ZOTE!

4. Kama hao wachagga watajaa mahala fulani na KUKOSEKANA kwingineko, hilo ni kinyume na "natural laws", na hapo maswali mengi tu yataulizwa, ikiwemo la UKABILA

Hapo mimi nitawauliza swali hili, INAMAANA WACHAGGA WAME-SPESHOLAIZI KWENYE MAMBO FULANI NA WANAANDALIWA TANGU MWANZO KUWA NA FANI FULANI FULANI, AU TUSEME MAUMBILE NA AKILI ZAO HAZIWAWEZESHI KUFAULU FANI ZINGINE.

Mwanakijiji tueleze kwanini wachagga wamejaa sekta zenye ulaji tu!
 
Jamberi.

asikudanganye mtu hawa watu wanaojitia wamesoma sana tuliwambia watuletee wagombea urais ambapo hata qualification ilikuwa digrii wao walileta wagombea wanane toka mkoani kwao na sita hawana digrii.
sasa nafasi muhimu ya urais wa nchi wameshindwa kuleta watu wenye minimum qualification hiyo historia ilikuwa wapi?

nenda hata wenyekiti wa vyama vya siasa, CCM mwenyekiti wao ni graduate, CUF mwenyekiti wao ni professor, Chadema mwenyekiti wao mchagga(mbowe) hana hata diploma, NCCR-mwenyekiti wao mchagga (MBATIA) kidato cha sita,NRA-mwenyekiti mchagga (OLOTU) hana hata fomu six, nenda hadi demokrasia makini na vyama vingine hakuna graduate.

sasa iweje TRA ndio tuambiwe kuna wasomi?

kabila kama wakwere limetoa mwenyekiti graduate wao wameshindwa hilo lakini watang'ang'ania tumesoma. na hizo ni nafasi nyeti kwa mustakabali wa nchi.

Mwanakjj amekuwa bias kiasi fulani mfano aliopewa na Bakaa kuwa mawaziri waliochaguliwa mara ya mwisho na JK ni wakristu watupu wanne hapo hakuwa na hoja za udini na hata wakuu wa wilaya waislam hawafiki asilimia 30 hilo mwanakjj ukaona sawa, ila walipochaguliwa akina Adadi RAJABU ukaja juu sana, na hilo uliliundia mjadala kwenye redio yako. na ukaweka mada ya mahakama ya kadhi na kulaani sana .

lakini PAPA benedect alipowakashfu waislam hukutoa kauli yako. u bias wako kwenye udini ndio sawa na huu wa ukabila. bunge limejadili udhaifu wa TRA WEWE bado unabisha?

nauliza Reginald Mengi kwa KUTUMIA mgongo wa ukabila kapitisha benzi likiwa na document kama za chama cha walemavu. lakini Benzi hilo anazunguukana nalo yeye. na amekuwa akipitisha vitu vingi hadi pikipiki kwa kisingizio za walemavu huku KITIILYA NA George Lauwo wakijua anadanganya.

sasa Mwanakjj WATU kama walemavu wanadhulumiwa kupitia mtandao wa ukabila na wewe wala humii?

nimekupa data kodi ya billion 5 aliyokwepa mengi kupitia mgongo wa ukabila wewe huumia . hujui pesa hizo zingesaidia mengi kwa wananchi?

nakuomba pitia majadiliano ya bunge mkutano wa 16 kikao cha 41 5-august 04 uone hoja za mbunge stephen Kahumbi KUHUSIANA na dada aliyefukuzwa kazi TRA kiuonevu.
 
Phillimon Mikael.

mimi nimekuwa nikikusuta kila mara kwa uongo wako. ulikuja humu na uongo kuwa LUOGA NA LAUWO hawana ndugu TRA nikakwambia wako wapi na mdogo wake Lauwo ndio specialist wa mizigo michafu(ukwepaji kodi) watu wanasema kuna vifaa vya kilimo kumbe ni matairi na mizigo namna hiyo hutoka kimemo juu kabisa kuwa mzigo huo utakaguliwa na Junior Lauwo amri hiyo haipitii kwa officer incharge.

mbona hukusema mswahili muongo sio kweli. umekuwa ukirukaruka mada kila dakika.

Majina yote niliyokupa mwanzo hukukanusha nilikwambia Holili yuko ndupa mchagga ndio RRO. mbona hukuja na jina lingine?

nilichofanya katika orodha yako uliyodai ndio watendaji nikakuwekea watu karibu 16 na kukwambia wako wapi? na si watendaji na hawana digrii na nikakuwekea hadi majina sahihi mengine ulikosea. mbona hukuja kubisha kuwa majina yao ni hivi na hawako huko ulikosema Mswahili?

majina yale ulileta wewe na mimi nikakuambia wako wapi hapo ujue najua nasema nini?

PM wewe umeongopa humu kuwa DR.DAU hajafanya kitu nssf na hiyo chuki yako kwake kisa ni mswahili na mtoto wa ocean road(mutoto wa muji)? kwanini unatuchukia waswahili? nikakuambia DAU toka aingie chuoni UDSM hakuwahi kupitwa na mchagga yeyote alikuwa best student hadi anaondoka si yeye tu hata DR.Shukuru Kawambwa mtoto wa bagamoyo naye hakupitwa na mchagga yeyote huo usomi wenu ni huko ila kwa watoto wa mjini hamuwezi kitu.

naomba upitie hoja aliyoitoa mbunge Kahumbi juu ya ukabila TRA kikao cha bunge n0 41.august 5 2004.

nakupa NSSF iko vipi ili ujuwe watoto wa mjini wana uwezo wa kufanya maajabu kwani wao uaminifu au uadilifu na maumbile yao.

1999/2000 NSSF ilikuwa ina net worth 169 billion na sasa ina worth 450 billion ni zaidi ya ongezeko la asilimia 200.

2000/2001 wakati mtoto wa mjini anachukua michango ilikuwa makusanyo yake ni billion 39.9 hivi sasa ni billion 146 sawa na ongezeko la asilimia 216.
matumizi yameshuka hadi asilimia 14. wakati mswahili anachukua shirika matumizi ya shirika yalikuwa yanakwenda kinyume na kifungu no 61(4) cha sheria no 28 ya mwaka 1997 iliyoanzisha NSSF KINACHOTAMKA wazi kuwa matumizi ya shirika yasizidi asilimia 15 kwa hali yeyote. huko nyuma ya mswahili ilikuwa matumizi asilimia 22, 1999-2000. au 19% 2000-2001.

PM hutaki hata kuona kazi ya mafuta house au hosteli za chuo kikuu za mabibo ambapo hata wenye historia ya elimu wanafaidika nazo hiyo ni kazi ya DR,Dau ambapo makengeza wachache kama [phillimon mikael wanashindwa kuona.
naomba pm sema kama kuna uongo kwenye hizi takwimu.na ziko wazi kama mfuatiliaji utaziona. a word of causation hapokeki rushwa mswahili wala kuotoa,
jee huoni toka kwenye 169 billion hadi 450 billion kama ni hatua? au huoni toka kwenye makusanyo ya michango toka billion 39.9 hadi billion 146 kama ni hatua kubwa kafanya mswahili au kwa vile kafanya mswahili? ndio maana nikawa nakuuliza mswahili aliweza vipi ku survive ndani ya mkapa kama si mtendaji?

naomba unipe actuarial valuation ya shirika hivi sasa kama kweli wewe mkweli?

wanabodi.

KUNA watu wanadai mada imekwisha TRA twende sehemu nyingine. jee hapa hatujakubaliana kama kuna ukabila kwenye taasisi, huko kwengine tutakwenda lakini kwanza tukubaliane kuwa ukabila upo then twende kote.
 
tumekubaliana kuwa mmekubaliana kuwa ukabila upo TRA haya nendeni kwingine... tutawafuata!
 
Mwanakjj.
kama nyinyi mlivyokubaliana kuwa HAKUNA UKABILA TRA.masihara yako wenzako wanateketea kwa ukabila. tutaliendeleza hadi kuhakikisha wanyonge wanakuwa na sauti TRA.
 
Mwanakjj.
kama nyinyi mlivyokubaliana kuwa HAKUNA UKABILA TRA.masihara yako wenzako wanateketea kwa ukabila. tutaliendeleza hadi kuhakikisha wanyonge wanakuwa na sauti TRA.
Mswahili!
Nafikiri hili swala ni kwamba watu humu tukubaliane tu kutokubaliana kwani Kila upande inatetea msimamo wake na sioni kwa hapa tulipofikia kama kuna upande utakubali hoja ya mwenzake.
Kuhusu Mwanakijiji msimamo wake kuhusu hili upo wazi kwamba yeye hawezi kuwatafuta hao watu wa TRA kwasababu hicho ambacho anaombwa awatafute na kuwahoji yeye anaamini hakipo na nyinyi mnaamini kipo, hivyo kwake yeye kwenda kuwatafuta wahusika na kuongea nao haoni mantiki.
Ushauri kwa mswahili:
Kama swala nikuwahoji wahusika TRA na kupata ukweli kwanini msitafute chombo kingine ambacho kinaweza kuifanya hiyo kazi ya kuwatafuta na kuwahoji na kumpatia data zote ambazo unahakika nazo ili zitengeneze maswali ya msingi.
 
Phillimon Mikael.

1999/2000 NSSF ilikuwa ina net worth 169 billion na sasa ina worth 450 billion ni zaidi ya ongezeko la asilimia 200.

2000/2001 wakati mtoto wa mjini anachukua michango ilikuwa makusanyo yake ni billion 39.9 hivi sasa ni billion 146 sawa na ongezeko la asilimia 216.
matumizi yameshuka hadi asilimia 14. wakati mswahili anachukua shirika matumizi ya shirika yalikuwa yanakwenda kinyume na kifungu no 61(4) cha sheria no 28 ya mwaka 1997 iliyoanzisha NSSF KINACHOTAMKA wazi kuwa matumizi ya shirika yasizidi asilimia 15 kwa hali yeyote. huko nyuma ya mswahili ilikuwa matumizi asilimia 22, 1999-2000. au 19% 2000-2001.



jee huoni toka kwenye 169 billion hadi 450 billion kama ni hatua? au huoni toka kwenye makusanyo ya michango toka billion 39.9 hadi billion 146 kama ni hatua kubwa kafanya mswahili au kwa vile kafanya mswahili? ndio maana nikawa nakuuliza mswahili aliweza vipi ku survive ndani ya mkapa kama si mtendaji?

naomba unipe actuarial valuation ya shirika hivi sasa kama kweli wewe mkweli?

wanabodi.

KUNA watu wanadai mada imekwisha TRA twende sehemu nyingine. jee hapa hatujakubaliana kama kuna ukabila kwenye taasisi, huko kwengine tutakwenda lakini kwanza tukubaliane kuwa ukabila upo then twende kote.



Mswahili

hizi DATA unauhakika nazo? na umeweza kuzipata vipi? na kwa nini umetoa 2001-2002 wakati huu ni 2007 ?

in short ingekuwa vizuri ukaeleza NSSF muda wote aliokwepo Dr DAU performance pale ikoje?

vile vile ni vizuri tukajua kama je pale NSSF hakuna UKABILA? maana mada hii ni kuhusu UKABILA

SWALI HILI NILIWAHI KUMUULIZA philemon michale huko NYUMA NA HAKUNIJIBU

na mwisho mimi nimekubali kuwa UKABILA upo TRA na ni TATIZO ambalo inabidi kufanyiwa utatuzi
 
Mswahili Kumkoma Nyani Giladi Mwanangu, Admin,

mbona umefuta ile kitu safi ndugu yangu? Au ndio hizi staili mpya za ki-maijna majina na nini! na nini! na nini? that wo-sup, wooooooooooord Upppppppp!

Mswahili kazi kwako mwanangu, miye ngoja nirudi Samvula!

anyway Mzeee Admin, nimeiona umeihamishia chini hiyo sio haki kwa Mzeee Habari Leo, maana hiyo mada si ilikaaa kama siku mbili kabla sijaijibu mbona hukuishusha? Alipokuwa anatukanwa Makamu Wa CCM, Dr. John S. Malecela kuwa hafai kwa sababu ni mzee na analala sana usingizi mbona hukuifuta au kuishusha chini, mbona sasa? Tafadhali irudishe, mana mtoto akililia wembe mpe, mimi sikuianzisha hiyo mada nilikuwa nimejipumzikia nikaitwa sasa mbona umeitoa baada ya kujibu, ifunge lakini uirudishe hapa au naahidi sitaichangia tena, hata ukimpa huyo Mzee wa Majina nafasi aaandike anavyotaka mimi sitajibu lakini irudishe hapa maana hiyo ndio the best ya hii forum bwana Admin, irudishe tafadhali mkuuu hiyo ndio kwa kizaramo tunaita kumkoma nyani yenyewe hiyo,

anyway Admin, umenifurahisha sana kutoifuta maana naona hata huko kabrasha bado inafuatwa hata lile donge langu la kuonewa Mswahili limeisha bro, kazi njema na bravo ila again ikiwezekana irudishe hapa, lakini mimi mnyonge sitaichangia nitawaachia wenye nguvu lakini irudishe mwanangu hapa giladi!

Mswahili Kazi Kwako Mwanangu kula naye sahani moja mwanangu mtu mzima huyo kajileta mwenyewe huyo Mzeee wa Majina!

Ila kabla sijanawa mikono, nitoe pongezi kwa Ndugu Mnyika JJ, you are a true class politician maana sijawahi kukuona ukimtukana mtu hapa, pamoja na matusi yote unayorushiwa kila wakati hapa, now I see ninasema you have a bright political future! Na ustaarabu wako nitausema na kuufikisha panapotakiwa kwa wanyonge!
 
IMHO ...
Sasa kuna Rais "Mswahili" na Mwislamu. Mswahili wa humu mtadaoni ameamua kujipa jina hilo ili kuji-identify na Rais Mswahili, kwanza, na pili ni Mwislamu. Mswahili angependa yeye ndiye awe kinara pale TRA. Siyo ili afanye kazi kuzidi hao waliopo kwa sababu labda hao waliopo hawafanyi kazi vizuri, bali ili ALE!

Ni kama anaanza Kaulimbiu: Waswahili na Waislamu ni wakati wetu sasa, waondolewe wengine na sisi tupewe sisi KULA. Wala siyo nia ya kufanya kufanya kazi, kwa sababu kazi hazipo TRA tu. Luckily, president na uongozi watapuuza pressure kama hizi, mwelekeo siyo mbaya so far. MERIT! MERIT, MERIT is what matters!

Huko nyuma tumeona watu wa TRA waliokuwa wakichukua rushwa jinsi walivyokuwa "wakitesa mitaani". Kwamba na sisi tutafute njia ya kuingia pale tukatese, hicho ndo kinachowasumbua akina Mswahili, wala siyo ukabila, wala udini. Kama ni ukabila, basi wangeanza jeshini na kwingineko. Hata hivyo, nani alisema kwamba ajira zinagawiwa kwa kufuata kabila au dini?

Lakini kingine ni hiki, wivu wa waziwazi (wivu mbaya) hausaidii. Hawa jamaa zetu wachagga tunajua ni wahangaikaji wazuri. Kama hawakuajiriwa TRA watakuwa wanauza supu ya utumbo, wanapiga viatu rangi, wana baa, grocery, wanafuga ngombe, kuku n.k. n.k.

Its a reflection of some industriousness which should be emulated! Fact is, they are everywhere, not only in TRA. In the US, they know them to be the most hard working tribe in Tanzania!

But judging by vitriol I am starting to see in here, it will not be long before somebody starts torching them .....

_____________________________________
HARD, USEFUL WORK, THE TRUE LIBERATOR
 
IMHO ...
Kama ni ukabila, basi wangeanza jeshini na kwingineko. Hata hivyo, nani alisema kwamba ajira zinagawiwa kwa kufuata kabila au dini?

Kwa kusema kwamba wangeanza jeshini na kwengineko maandiko hayo yanapingana na swali lako, kwa mantiki hiyo unaamini hivyo vitu vipo.
 
Mswahili

hizi DATA unauhakika nazo? na umeweza kuzipata vipi? na kwa nini umetoa 2001-2002 wakati huu ni 2007 ?

in short ingekuwa vizuri ukaeleza NSSF muda wote aliokwepo Dr DAU performance pale ikoje?

vile vile ni vizuri tukajua kama je pale NSSF hakuna UKABILA? maana mada hii ni kuhusu UKABILA

SWALI HILI NILIWAHI KUMUULIZA philemon michale huko NYUMA NA HAKUNIJIBU

na mwisho mimi nimekubali kuwa UKABILA upo TRA na ni TATIZO ambalo inabidi kufanyiwa utatuzi


mswahili ,
hizi data umezipata wapi...kama unaweza tuletee hapa link ya FINANTIAL STATEMENT ya NSSF ndio itakayokuwa na taarifa ya kuaminika,hatujakataa ila tupe hiyo finatial statement[balance sheet...growth indicators ets]

Alafu pia uwambie wakuambie kama katika asset walizouza na kununua [dau akiwa md] vipi yale maghala waliyonunua kwa MANJI!!!....NA UJENZI WA DODOMA ets

pia lazima uelewe kuwa mashirika ya hifadhi ya jamii yanapanuka kutokana na wigo wa AJIRA unavyopanuka ,,so usishangae makusanyo yataaendelea kukua kadiri makampuni na waajiriwa wanavyoongezeka...

wasalaam...
 
Philemon Michael

lakini wewe katika mada hii uliwahi kusema hivi:

=phillemon mikael;21480 kuhusu NSSF naona hakuna tofauti kati ya dau na mkullo au mattaka...tena sanasana DAU bado hajafanya vivid investment kulinganisha na enzi ya kina mkullo au mattaka [hata mkimsema ..jamaa ni kichwa ]....ila aendelee kujitahidi ..na nafikiri ni mtu anayetumia sana propaganda chini chini..natambua ni PAN AFRICA mzuri na mtoto wa mjini ,,,but we want more results...


http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=21480&highlight=nssf#post21480


na mimi nikakujibu kwa kuuliza hivi:


Dr DAU aliingia NSSF lini?

Alikuta makusanyo pale NSSF chini ya MKULO yalikuwa kiasi gani?

Sasa hivi yako kiasi gani?

Je Kulikuwa na investments za kiasi gani?

Sasa hivi investments zimefikia kiasi gani?

Na ni Propaganda zipi anazitumia kuendesha shirika kubwa la wanachi la NSSF?

Na imekuwaje ameweza kusurvive pale muda wote huo tangu MKAPA amuweke pale?

Na ikiwa unaweza kuniconvince katika hayo then nitakuwa mtu wa kwanza kuanzisha "MWANAKIJIJI STYLE" kampeni zakumuondoa pale NSSF
 
Naona baada ya kimya kirefu ndio MSWAHILI kaja na data lakini huko nyuma bwana PHILEMON MICHAEL nilikuuliza swali hili hili na kwa kuwa tunakutegemea humu ndani kuwa wewe si MPGA DOMO hovo tuu bali unazungumza kutokana na uwezo wako wa kuambatanisha evidence basi naomba uniweke sawa katika maswali hayo hapo juu
 
Mwalimu alituasa kuwa tusiendekeze ukabila na mambo ya kujuana makabila yawe na maana sana, labda, kwenye matambiko na utani...

Kulikuwa na mzee mmoja aliyeitwa Mushi ambaye alipata ajali mbaya sana ya gari na kiasi cha kufikishwa chumba cha mahututi akiwa hajitambui. Kwa kudra za Mwenyezi Mungu, baada ya siku kadhaa alizinduka, na baada ya kupata fahamu akawaita wauguzi wamweleze nini kilichomsibu. Mmoja wa wauguzi akaanza kumwelezea jinsi alivyopata ajali.

Mzee Mushi akamaka, “Ajali ya gari! Lile Benzi langu la mbei mbaya? Limeharibika eeh?”

Muuguzi akamtuliza, “Mzee ilikuwa ajali mbaya sana na gari liliharibika vibaya sana…nasikitika kukuambia kuwa mkono wako wa kushoto ulivunjika kabisa na tumeshindwa kuuunga.”

Mzee Mushi akauliza, “Nimepoteza mkono? Na saa yangu ya Rolex aliyoniletea mwanangu Godlove wa Marekani iko wapi?”


Muuguzi akajitahidi kumfariji Mzee Mushi akimwambia asijali sana maana Mungu akipenda atapata nyingine. Akamwambia, ”Tena familia yako iko hapa, wamekuja kukuona."

Basi Mzee Mushi akaagiza wapite ndani. Walipokuwa wameingia ndani ya chumba alichokuwa na wakiwa wamezunguka kitanda chake, akaanza kuwaita majina mmoja mmoja.

"Mama Manka, uko hapa?"

"Ndiyo mume wangu, siwezi kukuacha," mkewe akajibu.

"Manka, na wewe uko hapa?", mzee akauliza.

"Ndiyo baba, na mimi siwezi kukuacha, pole sana", binti akajibu kwa huzuni.

Mzee Mushi akaendelea, "Aikaeli, uko hapa pia?"

Kama wenzie, Aikaeli naye akajibu, "Ndiyo baba, siwei kukuacha."

"Elibariki mwanangu, na wewe uko hapa?" Mzee Mushi akauliza.

Elibariki, mtoto wa kiume wa Mzee Mushi, akajibu kwa kujiamini, "Ndiyo baba, siwezi kukuacha kamwe."

Baada ya kimya cha sekunde kadhaa, Mzee Mushi akasema,"Ninyi wapumbafu sana…kama Manka, Aikaeli, Elibariki na wewe mama yao wote mko hapa duka nani yuko dukani?”
 
bwana who mimi sina tatizo la dau ,na wala si mimi niliyeleta hoja mezani ,haikua haki hoja alete mswahili alafu mimi ndio nijibu maswali juu hapo...mswahili amejibu na ni sawa,tatizo ametoA statistics za mapato hapo anawajibika kutupa source ,ndio maana nimemuuomba atupe link ya ANNUAL STATEMENT YA NSSF....hapo unaonaje?
kuhusu propaganda nilisema nilihisi kwamba mswahili anapiga sana propaganda dau...kiasi kwamba hamtyendei haki ...ni sawa na kumuharibia ..dau bado ni kijana na nauwezo wa kufanya zaidi sasa kama atahusishwa na mswahili itafanya mbele ya safari akose SIFA ZA KITAIFA...kama anafanya kazi watu wanaona ,hakuna haja ya kumpigia mayowe,wakurugenzi wa mashirika ya umma wapo wengi wanaofanya vizuri...

wakurugenzi waliotangulia wa NSSF kama sikosei mkullo mustapha ,ndie aliyejenga investments nyingi...zikiwemo hosteli za chuo ...sasa kama ujenzi ulipoisha alishastaaafu ..hilo sijui...ni kama uwanja wa taifa mpya utakapoisha mwezi wa saba ,..je tutasema umejengwa na kikwete au mkapa..kwa kifupi maendeleo ya taasisis yoyote ni TEAM WORK na sio ONE MAN SHOW...anaepokea kijiti anakuwa muendelezaji ....
 
Back
Top Bottom