Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Tukatae tukubali ukabila upo, hauwezi kuisha ila unaweza kunyimwa nafasi ili kisiwe kigezo katika mambo yanayohusu umma.

ukabila nini labda ? maana naona wengine hatujui chimbuko la ukabila.

Ukabila ni kipengele ndani ya ubinafsi. neno binafsi lina tokana na mimi au sisi. Kila mwanadamu ana ubinafsi. huanza kujiangalia yeye "yaani mimi" akiridhika yeye kama eye au akiona peke yake hawezi basi hukimbilia kundi gani ambalo na yeye atakuwemo ndani yake linaloweza kurahisisha yeye kupata anachokitaka kama kakosa au ni nani yuko karibu na yeye ambaye baada ya yeye kupata huyu hajapata "yaani anaangalia sisi"
Ubinafsi huu hujitokeza kama mtu binafsi, au kimakundi kama familia, koo, kabila, dini, jinsia, makundi kama ya siasa, mpira, jamii nakadhalika.

Mimi naamini watanzania wote ni wabinafsi kama walivyo wanadamu wote. Kila mwanadamu anaangalia nafsi yake, na ubinafsi ndio chimbuko la wivu, kwani mtu hujiuliza kwanini sio yeye apate kile ila anacho mtu mwingine, kwa nini asiwe yeye bali ni mtu mwingine.

Kutokana na utofauti wa wanadamu kimatamanio ubinafsi wetu hujionyesha katika mambo tofautitofauti kila mtu katika jambo lake ingawa kuna mambo tunafanana wakati mwingine.

ubinafsi unapokuta nchi inayolegea katika uongozi mara nyingi sura kama hizi za kikabila, kidini, kifamilia, kikoo nakadhalika hujitokeza.

tukiangalia hapa tanzania tuangalie hivi kweli tukiangalia mfumo wa ajira kama mada ilikopitia kweli kuna usimamiaji wa kuhakikisha ushindani wa kiutendaji unatumika katika kuajiri au tunaajiriana kwa kujuana, wataalamu wanasema ili upate ajira kiushindani unahitaji "know how" lakini kwa tanzania unahitaji "know who"

sasa katika mfumo huu wa kuajiriana kwa kujuana tutakataaje kuwa ukabila haupo?, ufamilia haupo?. Hivi katika tanzania hii ni nani ataacha kumfanyia mpango ndugu yake ili apate ajira kama anajulikana na anaushawishi wa kumpatia ndugu yake ajira?
Siku zote ukaribu wa watu huanzia nyumbani "undugu". ukikutana na mtu mbali na kwenu mnaotokea sehemu moja utamuona ndugu yako na hapo usisi huanza, ukiwa mfano ulaya ukaona mtu anaongea kiswahili unamuona ndugu yako. katika nchi watu huonana ndugu kuanzia familia, ukoo, kabila, dini na kadhalika na hivyo pale ambapo hakuna ufuatiliaji wa sheria kuhakikisha kuwa watu hawatumii nyadhifa zao kuridhisha nafsi zao, katika ajira sura za kibinafsi hujitokeza katika mrorongo kama ulivyoorodheshwa hapo juu.

Hivyo ubinafsi katika Tanzania, katika nyanja ya ajira umejitokeza sana kifamilia ambapo unakuta familia fulani wameshikilia nyadhifa kubwa kubwa au zilizonona kimapato, sio kwa ushindani wao bali kwa kuwa na "good god father in family". sio lazima tutajane
kwa yale makabila ambayo wanakabila wake wamekuwa wakijisikia kwa mtu kujitaja mbele za watu kuwa mimi kabila fulani kutoka na picha fulani kwenye kabila hilo wamejikuta wakitambuana mijini na kujiona wako karibu na wale ambao mfumo wa ajira wa zamani ulikuwa umkipatia nafasi kila mtu ulikuwa umewawekea wajumbe wa kutosha katika nyadhifa muhimu wamenufaika na na mfumo huu wa sasa wa kuajiriana kwa kujuana inayotokana na uzembe katika uongozi katika kusimamia taratibu.

Kwa ujumla ubinafsi ndio chachu ya maendeleo, bila wewe kujiuliza kwa nini wewe uwe masikini wakati kuna watu wengine matajiri huwezi kupiga hatua, bila kujiuliza kwa nini familia yenu masikini au ikose vitu fulani na familia nyingine ziwe mbele huwezi kwenda. Bila kujiuliza kwa nini kabila lako liwe masikini wakati makabila mengine yamepiga hatua mbele, bila kujiuliza kwa nini sisi watanzania tu masikini hakika hatuwezi kupiga hatua. siri ya mafanikio ni kutoridhika na kile ulichonacho au na pale ulipo.

ila bila serikali kusimamia sheria ili kila mtu atambue mipaka yake na watu wakaanza kutumia mali za umma kama ni zao binafsi, ana mwajiri ndugu yake kwa sababu ni ndugu yake sio kwa sababu yeye ndiye bali zaidi ki taaluma kwa nafasi hiyo, au jamaa yake au rafiki yake wa kweli hapo ubinafsi utabadilika na kuwa chanzo cha kurudi nyuma na unaweza kuwa chanzo cha vurugu pale wale ambao hawana ndugu zao kwenye mfumo kuwaingiza watakapokata tamaa.

MTU YEYOTE AKIPEWA WADHIFA WA KUAJIRI AKAMUAJIRI NDUGU YAKE WA KULAUMIWA NI YULE ALIYEMPA WADHIFA HUO AU ANAYESTAHILI KUMSMAMIA. hivyo katika sekta ya umma kuajiriana kidugu wa kulaumu ni serikali. na serikali ya tanzania ni uongozi wa watanzania.

katika sekta binafsi usindani kwenye soko ndio utawafanya watu watoe ajira kwa ushindani na sio kwa kujuana
 
Mtukwao
Inaonekanduguyangu Mpira wa miguu unakushinda unaaza kutumia mikono wakati hairuhusiwi kwaniinaonyesha umejaribu saaana kutetea ukabila wako lakini inaonyesha umeshindwa kwahiyo unajaribu kuwaambia watu wako waazi kabisa kwa kuamua kubadilsha jina nakutumia(MTUKWAO) HAPO TUMEKUPATA, Lakini kwanini usitimie hilo jina katika Campeni zako ? au uibandike katika kile chombo chako unacho tumia katika kuwakusanya akina mbeku?,
Sio ajabu kwani wapo wengi wametumia misamiati ya kila aina kwa utashi wao kwa mfano BABAYKO ANALO?,SIRI YAKO,nk kwahiyo sio mbaya utumie kifungio cha mihazara yako kwa hayo maneno MTU,,,,, KWAAOOOOOO, MTU,,,KWAOOOO, CHAGA, OYEEEEE,CHAGA,OYEEEEEE, ahsateni hatulali mpaka kieleweke,pm umekuwa kinyoga jibu hoja sio kubadilkabadilika.
 
Mtukwao
Inaonekanduguyangu Mpira wa miguu unakushinda unaaza kutumia mikono wakati hairuhusiwi kwaniinaonyesha umejaribu saaana kutetea ukabila wako lakini inaonyesha umeshindwa kwahiyo unajaribu kuwaambia watu wako waazi kabisa kwa kuamua kubadilsha jina nakutumia(MTUKWAO) HAPO TUMEKUPATA, Lakini kwanini usitimie hilo jina katika Campeni zako ? au uibandike katika kile chombo chako unacho tumia katika kuwakusanya akina mbeku?,
Sio ajabu kwani wapo wengi wametumia misamiati ya kila aina kwa utashi wao kwa mfano BABAYKO ANALO?,SIRI YAKO,nk kwahiyo sio mbaya utumie kifungio cha mihazara yako kwa hayo maneno MTU,,,,, KWAAOOOOOO, MTU,,,KWAOOOO, CHAGA, OYEEEEE,CHAGA,OYEEEEEE, ahsateni hatulali mpaka kieleweke,pm umekuwa kinyoga jibu hoja sio kubadilkabadilika.
 
Nyinyi jamaa mnafanya kazi rahisi iwe ngumu kweli. Ni rahisi sana kuonesha mahali kuna ukabila na nimewapa njia kama kadhaa za kufanya hivyo, ambazo ukizipeleka kwenye tume huru au watu huru wakiona tu wataamini kuwa something is wrong. Nitazirudia hapa kwa faida ya wengine. Kuna watu wanaodai nina maslahi fulani huko TRA sina, sijawahi kuwa nayo. Sina ndugu, jamaa, au mtu nimjuaye ambaye ameajiriwa huko!

1. Wakati TRA ilipoundwa mwaka 1996, wafanyakazi kadhaa walipunguzwa kwa sababu mbalimbali. Kati ya karibu wafanyakazi 4000 hivi 1400 walitemwa. Endapo kuna mtu ataonesha kuwa uwiano wa walioachishwa wakati huo na wale waliobakizwa unawapendelea wachagga nitaanza kuhisi kuna walakini. Mswahili et al, nionesheni kuwa wale 1400 walioachishwa hawakuwemo wachagga, na waliobakizwa wengi walikuwa wachagga.

2. Naomba nielekezwe utaratibu wa ajira huko TRA ambao unaweza kuwa na matundu makubwa ambayo yanaweza kuruhusu ukabila. Kuchagua jina la mtu mmoja au wawili na kusema ati walinyimwa ajira kwa vile hawakuwa wachagga ni takwimu za kitoto. Ni lazima uoneshe mwelekeo (pattern) wa tabia hiyo. Kati ya watu 500 walioajiriwa TRA ni wangapi ambao hawakuwa wachagga na walinyimwa nafasi hizo wakati wakiwa na sifa zote, wakati baadhi ya Wachagga wasio na sifa waliajiriwa?

3. TRA tangu kuundwa kwake imekuwa ikiwafukuza watu kadhi kwa sababu mbalimbali, nitafurahi kuoneshwa kuwa idadi ya watu wa makabila mengine wanafukuzwa zaidi kuliko wachagga wakituhumiwa makosa ya aina ile ile

4. Kuna njia rahisi ya kuona inawezekana vipi kuwa na wachagga wengi sehemu za kazi TZ. Ni zoezi rahisi. Mtu atangaze kwenye gazeti kuwa kampuni XY ina nafasi za kazi za uhasibu n.k na anayetakiwa kuomba awe ni mwenye shahada ya Biashara, mwenye uzoefu wa miaka mitano. (sifa hizo mbili tu) halafu tuone proportion ya makabila watakaoitikia wito huo. Nadharia yangu hapa ni kuwa Wachagga watakuwa wengi. Swali litakalofuatia ni "Kwa nini"?
 
Waislamu mara kwa mara wamekuwa wakitoa majina ya wafanyakazi wa mashirika mbali mbali na kuainisha idadi ya waislamu na wakristo kuwa haiwiani na takwimu za mgawanyo wa waislamu na wakristo nchi nzima.

mimi nakubaliana na wewe kuwa ukabila upo, au binafsi upo ila ninatofautiana na wewe kwa kusema "ili kujua kama kuna ukabila au udini tulinganishe idadi ya dini au kabila katika nyadhifa."
ukabila ni sababu moja ila kuna sababu nyingine nyingi zinazoleta utofauti wa idadi ya watendaji katika nyadhifa katika makundi mbalimbali
kumnyima mtu nafasi kwa sababu ya dini au kabila au kundi atokalo ni ubaguzi lakini vile vile kumpa mtu nafasi kwa sababu ya dini au kabila au kundi lolote ni ubaguzi pia.
hivyo tutakuwa tunafanya ubaguzi tukitaka kulinganisha idadi ya makabila au dini au makundi mbalimbali ndani ya nyadifa na wala hili haliwezi kutuletea maendeleo.
tukianza kuteua watendaji sio kwa ushindani bali kwa kuangalia kulinganisha makundi tutaishia pabaya kwani ukilinganisha dini kutaibuka madhehebu ndani ya dini na kujiona utofauti.bado kuna dini za kijadi ambazo hazijafuata dini za kigeni nazo zitadai nafasi. Tanzania siyo nchi ya ukristo na uislamu tu hivyo ukitoa nafasi kidini lazima kila mtu katika dini yake apate nafasi.
Kuna makabila mngine mpaka sasa hivi hapa tanzania yako yanayoishi maisha ya porini ila itabidi uwatoe porini na uwape nyadhifa kubwa ili kuleta usawa wa kabila iwapo uaamua kuleta usawa wa kikabila.
ubaguzi unaondolewa kwa ushindani na yule aliyeoneka bora katika waliojitokeza kuwania nafasi hiyo, hivyo wanaweza kuwa wote kabila moja, wote dini moja wote jinsia moja ilimradi hawajawekwa kwenye nyadhifa hizo kutokana na makundi yao bali kutokana na ubora wao wa kuziba nafasi hizo, na hakuna walionyimwa kutokana na makundi yao
 
Mzee Mwanakijiji,

Kufukuzwa kazi sio kabisa sababu ya kuwepo Ukabila. kati ya wafanyakazi hao 1400 wanaweza kufukuzwa wote toka makabila tofauti kwa mara moja ama muda tofauti, lakini kundi linaloingia ndilo likawa na tatizo. Tatizo hapa ni kabila kuwa kigezo cha utoaji ajira!.. Ukimfukuza mchagga kazi kisha ukamweka Mchagga mwingine bado hujabadilisha kitu pamoja na kwamba hesabu ya Wachagga waliofukuzwa ilikuwa kubwa.

Kisha nilivyoelewa mimi mada hii haizungumzii wingi wa kabila fulani iisipokuwa ugawaji wa ajira ktk baadhi ya sehemu zimetumia kwa kigezo cha Kabila...(merit) kwa hiyo basi,
1. Yawezekana walioajiriwa baada ya kufukuzwa wale 1400 kuwa ni wachagga wengi.
2. Yawezekana nafasi nyeti zote ktk uongozi wa TRA zinachukuliwa na Wachagga. Kumbuka tu kwa Mdanganyika nafasi nyeti ni ile yenye Ulaji!
3. Sikubaliani na tafsiri ndefu ya hili neno kutumika hapa kwa sababu Ukabila una sura tofauti. Upo Ukabila ambao hauna madhara ya ubaguzi kama vile mtu kuchagua mke/mume wa kabila lake. Pia kuna Ukabila wa kutowapendelea kabila lako. mathlan Wakerewe na Wajita siku zote hawawezi kumpa nafasi mtu wa kwao ajira labda awe ndugu yake na kwa msisitizo toka kwa wazee wake. Kutokana na kijimila hili, hawa jamaa wako radhi kumtoa roho mtu wa kabila lake wanapo gombea nafasi.

Kwa hiyo tunapozungumzia Ukabila haina maana kabisa kuwa nchi nzima imekuwa na Ukabila. hata AIDS ni maradhi ambayo tunaweza kusema Tanzania ina asilimia kubwa ya waathrika, ama Tanzania kuna AIDS!. Hii haina maana hesabu kubwa ya wananchi wana ugonjwa huo kuliko waliokuwa wazima. Navyofahamu mimi kuna kama asilimia 10 tu ya wagonjwa wa AIDS nchini lakini kukataa kwamba hakuna AIDS, Tanzania ndipo naposhindwa kuelewa.

Hata hivyo Hoja za mada hii zimeisha kuwa dhaifu sana kwa sababu sioni kabisa uhusiano wa jeshi letu na Ukabila ikiwa jeshini ni sehemu huru ambayo inaandikisha watu kila siku. Tena basi wanatafuta wanajeshi zaidi isipokuwa kuna kabila moja ambalo linaipenda kazi hiyo na ndio wenmgi wanaojiandikisha.
Je, mtapenda sheria ya kujiunga na jeshi iwe wajibu?..sidhani kwa hiyo jiungeni na jeshi kisha nambieni maanake navyofahamu mimi Ukimaliza chuo kikuu ukajiunga na jeshi moja kwa moja unashika nafasi ya juu yaani ofisa!.. mh. rais wetu ni mfano bora.

Kwa hiyo kuna mchanganyo wa hoja hapa sioni kabisa kinacheoendelea ikiwa watu mmeshindwa kwenda kwa hatua..yaani Taasisi kwa Taasisi.
 
Mkandara, finally angalau kwa mbali unaanza kuona tatizo hili la msingi mzima wa hoja. Kama watu kumi wakioneshwa kuwa wana ukabila haiwezekani kuifanya taasisi nzima iwe na ukabila! Na pili umelipata pia kuwa ukabila siyo idadi! kuwa na watu wengi wa kabila moja mahali fulani haifanyi kuwe na ukabila!

Madai ya ukabila ni mazito na watu kutulazimisha tuone ukabila mahali ambapo haupo basi wanawajibu mkubwa wa kutushawishi tuuone ukabila huo! Watanzania wanaoishi na kushirikiana pamoja hapo London au mji mwingine wowote na kuanzisha jumuiya zao haiwafanyi wao wabaguzi!

Na kufuatialia madai haya hatuwezi kuchukua taasisi moja bila kuangalia taasisi nyingine zenye hoja zinazolingana i.e kama idadi ya watu wa kabila moja inafanya kuwe na ukabila kwanini tusiangalie taasisi nyingine ambazo zina watu wengi wa kabila moja na kuhitimisha vivyo hivyo?

Hivi tunavyozungumza, Kamisheni ya Ushindani Sawa wa Biashara (Fair Competition Commission) inaendesha usaili wa waombaji kadhaa wa nafasi mbali mbali. Baada ya kuangalia watu zaidi 500 wafuatao wamaietwa kwenda kufanya mahojiano (interview). Kwa kuangalia majina tu ni kina nani wanapendelewa?

Uchumi
Lihoya Antony
Zawadi Mlingwa
Lemmy Nhende Shumbusho
Frank Materu
Chester Kapinga
Nyange Lugoe
Venance Mutayoba
Gladiness Foya
Clay Vitus Manda

Sheria
Salma Maghimbi
Khadija N. Sijaoma
John E. Mponela
Agustine Kusalika
Justine Aldo Nyenza
Angela P. Msechu

Utafiti
S .J M Kaitila
Magret Katole
Nixon Sembe
John Chassama
Salvator Chuwa
Provident Dimoso
Utukufu Ezekeil Kyando
Miligwa Sasa

Madai ya Walaji na Ulalamishi
Thabitha Maro
Frank Shanel Mdimi
Victor A. Muneni
Peter Mapigano Edward
Matukio Chuma
Wilfred Minja

Advocacy Officer
Felix Joseph Chile
Nuru Ephrahim
Magdalena Utouh
Pamela M. Mmassy
Mgosi Erick Shao
Adella Ndagala
Nasra Kara
Liliane Pasape

Afisa Uchunguzi
Kinabo J. Minja
Laiton Mhesa
Elizabeth J. Kaganda
Jane Shuma
Charles MMbando
Job Andrew Geleja
Janeth Boaz
Mercy Chimtawi
Consolata Andrew

Enforcement Officer
Kitandu P. Ugula
Grace Kamugisha Kazoba
Andisya Abihudi
Jacquiline Munemu
Joseph Neman Kiula
Josephat T. Mkuzungo
Brenda Syril Mlulla
Mairiam Bakari
Grace Freedom Nicholas
Shani Mayosa

Sasa, what are the chances kwamba wachagga kadhaa wanaweza kuajiriwa hapo na baada ya miaka michache mtu akasema kuna ukabila?

The venue for the interview is Fair Competition Commission Office, Azikiwe Street, Office Accommodation Scheme Building (that houses CRDB HQ), 7th floor.

Candidates will meet all costs relating to their participation in the interview process, including travel and per diem costs as applicable. FCC will not reimburse candidates for these costs.

All selected candidates should come with adequate ID and original certificates.
Lobbying and canvassing for employment will not be entertained and may work to the candidate's disadvantage.


Those who submitted applications for employment at FCC but are not included in this invitation list should consider their application to be unsuccessful


DIRECTOR GENERAL,
FAIR COMPETITION COMMISSION,
AZIKIWE STREET,
OFFICE ACCOMMODATION SCHEME BUILDING,
P.O. Box 7883,
DAR ES SALAAM
 
Mtukwao
Inaonekanduguyangu Mpira wa miguu unakushinda unaaza kutumia mikono wakati hairuhusiwi kwaniinaonyesha umejaribu saaana kutetea ukabila wako lakini inaonyesha umeshindwa kwahiyo unajaribu kuwaambia watu wako waazi kabisa kwa kuamua kubadilsha jina nakutumia(MTUKWAO) HAPO TUMEKUPATA, Lakini kwanini usitimie hilo jina katika Campeni zako ? au uibandike katika kile chombo chako unacho tumia katika kuwakusanya akina mbeku?,
Sio ajabu kwani wapo wengi wametumia misamiati ya kila aina kwa utashi wao kwa mfano BABAYKO ANALO?,SIRI YAKO,nk kwahiyo sio mbaya utumie kifungio cha mihazara yako kwa hayo maneno MTU,,,,, KWAAOOOOOO, MTU,,,KWAOOOO, CHAGA, OYEEEEE,CHAGA,OYEEEEEE, ahsateni hatulali mpaka kieleweke,pm umekuwa kinyoga jibu hoja sio kubadilkabadilika.

Reference to Mtukwao could also be to Tanzania, as any right thinking Tanzania should be doing?

But asuming I was what you think I am, nobody can avoid to identify with the basis of hios or her existence, like his tribe, clan, grandfather, race, etc etc. as long as they are used properly in society. Why do we have Makumbusho then?

IMHO, some of these arguments are tending towards driving people from some tribes to the defence. Just because they appear to be above average in some dev statitics. As if that was a crime. Well, it isnt, and it better not be, if we want to avoid wasting precious time that should be used to build our nation into a prosperous one.

As i have indicated above, reading between the lines of many an arguments hear reveals a lot. Especially when you really want find out who really is a MKABILA, MDINI etc.
 
Hongera Mzee mwanakijiji kwa hoja nzito.

Kwa Tuipendeinchiyetu:
Nakupa mfano mdogo tu lakini ni juu yako kuchambua pumba na mchele. Wilaya ya Mbozi, mkoani Mbeya wakazi wake ni Wanyiha na Wanyamwanga. Cha ajabu miaka ya sabini hadi ya tisini 1970's - 1990's) wanafunzi wengi wa shule za msingi waliokuwa wanafaulu kwenda sekondari mkoani Mbeya na Iringa ni Wanyakyusa wakifuatiwa na Wandali. Na hata Wanyiha waliofaulu na kwenda sekondari waliachia form two, form three au form four wakiwa na matokeo mabaya wakiwaza kwenda kulima kahawa. Mifano hai ninayo kwani nimesoma huko. Sasa unatarajia nini kiasi cha wasomi wa kabila la Wanyakyusa ukilinganisha na Wanyiha??? Unatarajia vipi waliotangulia kufikiwa kirahisi na waliochelewa?? Bila shaka kasi ya kusoma ya makabila waliotangulia inaendelea kukuwa kasi ukilinganisha na wanaoshtuka kuvuta shuka kungali kumekucha. Vivyo hivyo kwa wilaya za Chunya, Mbalali, Mbeya mjini na Vijijini. Cha ajabu huwakuti makabila mengine kwa wingi huko wilayani Rungwe (Tukuyu) na kyela...Unatarajia nini??????
Kuna mtu alipata div. II ya point 18 form four mwaka 1987 Njombe secondari na kuchaguliwa kujiunga Dar Tech enzi hizo, lakini kwa fikira za kulima kahawa akaacha kwenda chuo. Hali ya huyo mtu huyo nilipo muona mwaka juzi ilinisikitisha sana.

Kumbuka hata Dr. Che Mponda (nafahamu udaktari wake bado unashakiwa) aliwahi kutoa tuhuma za ukabila UDSM akiwa lecturer kwa Mwl. Julius K. Nyerere akiwa Rais lakini alishindwa kuthibitisha. Sana sana alionekana mjinga pamoja na udaktari wake.

Mwisho, Tuipendenchiyetu umesoma hadi kiwango cha elimu gani??? kama umefikia umefika ngazi ya elimu ya juu, jiulize darasani mwenu kulikuwa na wachaga wangapi??? wanyakyusa wangapi???? Wahaya wangapi??? wangapi kutoka kabila lako??? na kadharika??? Bila shaka utapata ukweli. Wachaga wangapi wanasoma mkoani mwako na wangapi kutoka kabila lako wanasoma Kirimanjaro ktk ngazi ya shule za msingi, sekondari na kadharika???
Nadhani inatosha kwa leo
 
Mzee mwanakijiji,

No... mzee usiyaweke maneno mdomoni mwangu!
Kama watu kumi wakioneshwa kuwa wana ukabila haiwezekani kuifanya taasisi nzima iwe na ukabila

Nasema yawezekana ikiwa kipimo cha utoaji ajira hizo umetumika kwa kigezo cha kabila. ndio maana huko nyuma nikasema kuna watu wana vyeti feki na wameshika nafasi za juu. Hata kama kuna watu wawili UDSM na wamepata ajira swala hili ni muhimu kulitazama kabla halijawa sugu.

Tukisikia Kipindupindu kimeingia Ngara hali waliokufa ni wawili lazima tuseme Kipindupindu kimeingia Ngara na sio kusema hao watu wawili walioathirika kwa sababu gonjwa hili husambaa.
Tunachohofia wengi ni kwamba Ukabila ni maradhi mabaya sana na husambaa haraka sana. Work force ya tanzania ni kama asilimia 20 tu na kati ya hizo wakiwepo waajiri kumi tu wenye Ukabila ndugu yangu hili ni tatizo kubwa lazima litazamwe.
Kisha hatuwezi kuruka huku na kule kutafuta suluhu ya swala hili ikiwa sehemu moja tu tumeshindwa. hakuna aliyesema tusitazame Uchumi, Ikulu na sehemu nyinginezo isipokuwa TRA tumepata hoja zinye uzito wa kuthibitisha kuwepo kwa Ubaguzi wa aina hiyo.
Na kibaya zaidi ndugu yangu ktk mada hii labda wewe tu ndiye hukutumia maneno mazito ya kuonyesha kuwa wachagga ni superior na sisi hapa kinachotusumbua ni xenophobia kwa sababu Mswahili kasema blaaa! blaaaa! blaaa!
Issue ya Ukabila ikageuzwa kuwa ni maneno kati ya pro Wachagga wa TRA na Mswahili.
baadaye nimekuja gundua kuwa kweli hata wewe huzungumzi kwa interest ya ku-solve tatizo hili ila kwa interest zako binafsi. sielewi reason zako isipokuwa unapiga chenga kiasi kwamba umesha vuka hata goli bado unaendelea na danadana nje ya uwanja. You are good ni ball control lakini mchezo huu ni zaidi ya ball control.

I rest my case!
 
Mkandara, ukisema kuna kipindu pindu kwa vile watu wanaharisha haina maana kuna kipindu pindu. Ili uweze kusema kwa uhakika usio shaka kuwa kuna kipindupindu, utaalamu wa kisayansi hufanyika na kuonesha kuwa vibakteria Vibrio cholerae. vimepatikana. Lakini kwa kuangalia watu kuharisha peke yake siyo lazima kuwe na kipindu pindu inawezekana ikawa ni typhoid ambayo husababishwa na bacterium Salmonella Typhi.

Sasa kwa vile magonjwa yote haya mawili yana vitu vinavyolingana haina maana ni ugonjwa mmoja.! Kuona watu wameajiriwa wa kabila moja haina maana ni ukabila inawezekana ni ugonjwa mwingine! Hivyo ukilazimisha kutibu ukabila wakati tatizo siyo ukabila huondoi tatizo. Ukimpa mgonjwa wa typhoid (homa ya matumbo) dawa za kipindu pindu (cholera) haimsaidii ingawa magonjwa yote husababishwa na bacteria.

Nilichojaribu toka mwanzo ni kuhakikisha kuwa tatizo lililopo TRA au taasisi nyingine ni kweli ni ukabila na siyo ugonjwa mwingine. Tatizo nyinyi hamtaki kuangalia chanzo cha tatizo bali mnataka kutibu dalili (symptoms) za tatizo!

On this one, I'll not back down, hadi tukubaliane kwanza kuwa ukabila haujathibitishwa, tuangalie kuna tatizo gani katika ajira Tanzania siyo kwenye chombo kimoja tu bali vingi, na kujaribu kutatua tatizo hilo. What say you?
 
Wazee,
Mnajua kuwa kuna kitu duniani kinaweza ku-exist lakini ikawa vigumu ku-prove existence ya hicho kitu?? Was thinking aloud...
 
Mikael(PM) na Mtukwao.
Wewe kwani unataka kujifanya kuwa hujui kama shemegi yenu Mkapa amelipa fadhila kwenu na kwafupi(mramba..kwakumuachia mke)
Mkapa kawapa TRA sasa katika kila wafanya kazi kumi saba ni niwachaga hayo kwenu haitoshi kuwa niukabila.

Mwanakijiji.
sasa hivi unasema kuwa JK kuwa sio mdini kwasababu baada ya Migiro kupata kazi umoja wataifa akachagua mawaziri wanne wote wakiristu lakini alipo chaguliwa Athman mmoja akawa kelele.sasa tunasubiri na wanaukumbi siku kikwete atakapo chagua waislam wawili na mkiristu akiwa mmoja itakuwa udini.
Kama tuana takia nchi yetu mema pasi tuwe wakweli wakati wote.

[Tuipende nchiyetu na tusiharibu miji ya watu
 
Mikael(PM) na Mtukwao.
Wewe kwani unataka kujifanya kuwa hujui kama shemegi yenu Mkapa amelipa fadhila kwenu na kwafupi(mramba..kwakumuachia mke)
Mkapa kawapa TRA sasa katika kila wafanya kazi kumi 3tatu niwachaga hayo kwenu haitoshi kuwa niukabila.

Mwanakijiji.
sasa hivi unasema kuwa JK kuwa sio mdini kwasababu baada ya Migiro kupata kazi umoja wataifa akachagua mawaziri wanne wote wakiristu lakini alipo chaguliwa Athman mmoja akawa kelele.sasa tunasubiri na wanaukumbi siku kikwete atakapo chagua waislam wawili na mkiristu akiwa mmoja itakuwa udini.
Kama tuana takia nchi yetu mema pasi tuwe wakweli wakati wote.

[Tuipende nchiyetu na tusiharibu miji ya watu

Watu wengine mnapotoa hoja mfikiri kidogo!

yaani katika kila wafanyakazi 10 watatu ni wachagga? hao saba ni kabila gani! na ulipata wapi takwimu hizo!! Na kuna wafanyakazi wangapi TRA. kwa mahesabu yako, kama kuna wafanyakazi 100, thelathini peke yake ni wachagga na wale 70 ni kina nani? mweh.. kichwa kinauma!
 
Hamna cha kufunga wala nini, ukweli uendelee kusemwa hapa hadi wale wote wenye hisia za ukabila wajiweke wazi!
 
topic hii ni vema ikafungwa sasa.


unawazimu?

topic ishasomwa mara karibu 10,000 na hakuna dalili za Mwanakijiji kupata majibu wala philemoni kulala

Huku Mkandara na Dua wakiongeza kahwa ilihali Mswahili kaenda kuleta Gomba halafu wewe unasema topiki ifungwe?

sikiliza wewe kama umeboreka kusoma unaweza kuchangia sub forums za michezo na kadhalika maana huhitaji kuwa na watu milioni wajibu hoja...hii ni special debate na watu wana mengi ya kuongea na waache waongee..wakichoka wataenda makazini ,kula au kulala na jioni wakija moto ni ule ule

jamani topiki haifungwi na endeleeni tuuu na kama mtaenda kukodisha majeshi hakuna tabu kwani yote sawa tuuu ni kama BOMU na ASHANTI lakini uwanja ni wa jeshi UKONGA hivyo natumai hakutokuwa na vurugu
 
MKJJ

Nimeweka ripoti iliyochunguza TRA na URA na mojawapo ya lililochunguzwa ni patronage na ukabila, URA walionekana kulalamikia Ukabila lakini TRA hawakuliona hilo ingawa waliona mapungufu mengine.

Hii ripoti unayoongelea ilikuwa commissioned na NORAD kwamba ilifanya uchunguzi wa kisayansi kuhusu swala la Ukabila Tanzania na Uganda huu ni uongo ni sayansi ipi unayotumia kufahamu mtu wa kabila lake amemuajiri mtu wa kabila lake - katika kazi ambayo hana qualifications zinazotakiwa? kama huwezi kuelewa hili utaelewa lipi?

Naomba utuwekee terms of reference ya hii study kule Tanzania na majina ya wale waliohojiwa pamoja na official reports na literatures kutoka serikalini ambazo walitumia kwa nchi zote mbili. Vile vile kutokana na mwandishi kusema kwamba kulikuwa na malalamiko ya ukabila yaliyotolewa uganda kuhusiana na swala hilo. (Ukiweka terms of reference tutafahamu vizuri zaidi)

Napenda vile vile kukuonyesha kwamba hii haikuwa study kama unavyotaka wanabodi wakubaliane na wewe kwa sababu moja kubwa ya Norwegians kujipigia debe kwamba serikali hizi ziajiri Key managerial expatriates ili kuongeza pato la ukusanyaji. Hapa hakuna tofauti na JK alipokuwa kule na kusema hatuna wataalamu wa ku-negotiate mikataba. Je mikataba yote ambayo tumeifanya tangu uhuru walikuwa wanatufanyia nani? Kwa taarifa yako hawa NORAD etc jukumu lao ni kuona jinsi wanavyo create employment kwa raia wao na pesa wanayokupa wanahakikisha inarudi kwao. Ipo mifano mingi tu jinsi wanavyochuma katika nchi zetu ndio sababu nilisema lazima tuwe makini na hizi reports. (http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=1867&page=39)

Undugunasation ni swala la kuajiri ndugu zako tu katika ofisi ambayo umepewa dhamana kuiendesha kiutaalam na huwezi kuita Ukabila ni undugunaisation hapo ni upotoshaji wa lugha yetu fasaha labda kama unataka kuitumia lugha hiyo Kenya, Congo, Uganda, Rwanda na Burundi au Zambia kwani hawafahamu Kiswahili fasaha.

Ni sawa vile vile kusema Uingereza hakuna ubaguzi wa rangi, lakini upo hata ukiutamka tu na wewe uko kwenye ngazi ya uongozi inabidi ujiuzulu au uwajibishwe. Lakini sisi Tanzania Huyo boss wa TRA na sio siri kamuweka huyo mdogo wake kule bandarini hakuna noma.
http://news.bbc.co.uk/1/hi/uk_politics/6431005.stm
http://news.bbc.co.uk/1/hi/uk_politics/6431645.stm

Utaalamu wa kisayansi unaoongelea umewaua wazungu wengi tu huku Ulaya kwa sababu ya kutoamini kuwa wanaumwa malaria, na hivi sasa huwa wanauliza kama ulikuwa umesafiri nje ya Europe kama unapandisha homa kali. Vile vile usisahau kuna mambo mengi ambayo hayahitaji sayansi, huo ndio tunaita ulimbukeni kila kitu unataka sayansi, kwani unafahamu sayansi leo? HAPANA. Tusisahau hata viongozi wetu wanakuwa malimbukeni kwani wanafikiria hakuna Mtanzania anayeweza kunegotiate mikataba bali Norwegian etc. ambao wanakuja kujifunzia kazi kwetu na kutudhalilisha. Kwa hili la ukabila HATUHITAJI sayansi tunahitaji kuangalia mienendo ya wale wanaoajiri.
 
Mwanaijiji na masapota wako, nawaomba muelewe na kukubali kuwa UKABILA UPO! nitatoa hoja:
1 Mfano wa nyerere UMEPITWA NA WAKATI, kama ni kweli nipe takwimu za wanafunzi waliopo mlimani unielee ni asilimia ngapi ni WACHAGGA, WANYAKYUSA au WAHAYA. Pia uniambie kwanini wao wanakuwa ni wengi huko vyuoni.

Nijuavyo ni kwamba pale mlimani au vyuo vyovyote vikuu kuna wanafunzi toka makabila yote, na marea nyingi walio bora huwa sio wachagga.

2. dalili ya pili ya ukabila ni SEHEMU WANAZOFANYA KAI HAWA JAMAA, kwanini wanapatikana wa wingi sehemu zenye pesa? Kwanini tusiwakute JESHINI, POLISI, MAGEREZA na kwengineko kama kwenye sekta ya ualimu nk? Wao wanapatikana pale PENYE ULAJI NA WANAJIWEKEA MIZIZI KWA KURITHISHANA.

3: Ili muelewe ni ukabila, jibu kalitoa mwanakijiji, kwamba ni HISTORIA, kwa vyovyote vile hajira za serikalini hazitegemei vyeti peke yake, inategemea ia kufaulu usahili, sasa kama aliyeanz kuajiriwa ni mchagga, akapewa suala la kutunga maswali ya kuwasahili waajiriwa wapya, miongoni mwa "wagombea" akawemo mchagga wanaefahamiana, hivi atasita kumpa maswali? Pili, katika hilo la usahili, iwapo alianza kuajiliwa mnyakyusa, akapewa RUNGU la kuwahukumu wagombea, atampa yupi masi nyingi kati ya MKURYA NA MNYAKYUSA?
 
Haihitaji digrii kuliona hilo, chukulia sasa iwapo itakuwa ni suala la baba na mtoto, au mjomba, shangazi, mjukuu nk. Hivi nitaacha kumwajiri mwanangu, au mtoto wa rafiki, kisa kuna mtu kamzidi kwenye intervie?

Mwenyewe nilikumbana na hili wakati naajiriwa serikalini (nilisha achana nao) Mojawapo ya masharti ya kuomba kazi ili ilikuwa ni kwamba muombaji lazima awe na VYETI VYOTE VYA DIGRII, lakini tulifanya usahili na kijana ambaye alikuwa bado hajapewa vyeti, yaani wakati alipoomba kazi alikuwa bado anasoma, tena huyo kijana akafaulu!! alifanyiwa usahili na ndugu yake na wengine tukafanyiwa usahili na JOPO!!

Niliongoza kwa kufaulu, kwa maan ahiyo ilibdi mie ndie nianze kupata promosheni au vi-safari au kusoma nje nk. Lakini hali ilikuwa kinyume, jamaa kwanza hakuwa anajua chochote kwenye fild na ndie alikuwa anafaidi matunda ya uhuru, eti mie nilitakiwaninyenyekee na kujikomba ili nipete, nilikataa wazi waz na wakajifanya kunitenga, sikukaa zaidi ya miezi 3 nikawatema nipo majuu nakunywa mvinyo ki-ulaiini!!

Mnaosema hakuna ubaguzi ni miongoni ya wale wanaopendelewa, kama mnastrago kama mie, mtauona ubaguzi!!

Kwangu mie ubaguzi haunitishi kwani naamini kama kuna nafasi 2 basi nikigombea azima nichukue moja, yaani huwa nafaulu usahili kwa maksi kubwa hadi wanaonaaibu kunitema!

Ubaguzi upo kila mahala hapa duniani, kila nchi hali ni hiyo hiyo, hata tukiwa watoto pale kwa mzee wangu wazazi walikuwa hawatupendi kwa namna moja, kuna mtoto au watoto wanaopendwa ama kuchukiwa zaidi ya wengie!! Hada tunaposoma madarasani hali ni kadhalika, unachotakiwa kufanya ni kuuuchukulia ubaguzi kama HALLENGE NA UKABILIANE NAO
 
Back
Top Bottom