Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Naomba mnitafutie idara nyingine yoyote ambayo imechukua hatua za kuzuia ufisadi kama TRA!!

Mwanakijiji,
Kuongea ni suala jingine na kutenda ni suala jingine. Hizo report ni blah blah tu lakini behind the scene ufisadi ni kama kazi. Ni sawa na mkuu wa usalama barabarani kukwambia wanapambana na askari wanao kula rushwa wakati huo huo jioni wanatakiwa wampelekee mgao wake.
Tukiacha hilo kwenye huu mjadala una hoja nzito ambazo wanaokupinga wameshindwa kupambana nazo zaidi ya kulazimisha mambo. Umetoa mifano hai ya MUCHS na UDSM na watu hawataki kuiangalia kwa sababu ina support contentions kwamba Wachaga wamesoma. Kama kweli wingi wa Wachaga TRA ni ukabila mbona hatuambiwa wingi wao Muhimbili ni ukabila pia? Kama Lauwo mkubwa kampa kazi Lauwo mdogo wakati hata sifa hana huo sio ukabila bali nepotism.
 
Tabasamu, nimewaonesha Mahakama Kuu majaji watatu wachagga wametoa uamuzi na kurudisha kesi kwa jaji mchagga utakaomfaa mhaya! Kama suala ni wingi tu wa watu wa kabila moja basi ukabila uko sehemu nyingi! Nakubaliana na wewe kuwa taratibu peke yake hazitoshi kwani ni ukiritimba tu. Hata hivyo, angalau wao wana utaratibu unaoeleweka... Ni taasisi gani yenye angalau utaratibu kama wa TRA?

Hili suala la TRA linahusu pesa na wachagga, hakuna cha ukabila wala nini? Kama ni ndugu kupeana ajira au watu wanaojuana kwanini tuishie TRA peke yake, na kwanini tuanzie TRA peke yake? Je Bosi Mchagga akimuajiri kijana aliyehitimu na mfanisi ambaye ni mchagga lakini hajuani naye ni baya zaidi kuliko bosi mchagga atakayemuajiri Mkwere anayejuana naye na ambaye hana qualifications? Wateteao ukabila watapiga kelele hilo la kwanza, lakini hilo la pili hawataki hata kuliangalia! kwani kwao Mchagga hawezi kumuajiri Mchagga mwenzake mahali pa taasisi za umma! akifanya hivyo ni Ukabila!!
 
KNKU,
Well, kusema kuwa kuundwa kwa TRA imetokana na mapendekezo ya Tume ya Mtei!..
inanipa picha nzima ya mwandishi kama mwandishi mmoja aliyesema - Chama cha Mrema badala ya jina la chama sijui kama umeelewa!
 
Mkandara wrote: Tume ya Edwin Mtei!. Ok now I know!

wana jamboForums,
Mwanzoni mwa miaka ya 1990 Raisi Mwinyi aliunda Tume ya kuchunguza utendaji kazi wa Idara za Ushuru wa Forodha na Kodi ya Mapato.

Tume hiyo ilikuwa chini ya Uenyekiti wa Edwin Mtei. Nimejaribu google search nimeona mjumbe mwingine alikuwa Juma Volta Mwapachu. I wish ningeipata tume nzima.

Mapendekezo ya Tume yalikuwa kuvunjwa kwa hizo Idara mbili na kuundwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania. Wafanyakazi wote walilazimika kuomba kazi upya.

Kamishna Mkuu wa kwanza Melkzedeck Sanare[rip] aliteuliwa na Raisi Mwinyi. Marehemu Sanare[mwenyeji wa arusha] alitokea ATC akiwa GM. Bodi ya Wakurugenzi ilizinduliwa na Raisi Mkapa na Waziri wa Fedha Prof.Simon Mbilinyi. Mwenyekiti wa Bodi alikuwa Dr.Benno Ndulu.

Bodi ya Wakurugenzi wa ATC inakuwa na wajumbe 10. Mwenyekiti huteuliwa na Raisi, na wako wajumbe wengine 5 wanaoingia kutokana na nyadhifa zao serikalini na TRA. Waziri wa fedha huteua wajumbe wanne. Sasa kabla hatujaanza kuwalaumu wakina Mramba ni vizuri tukalizingatia hilo.

Tanzania tumekuwa na Tume nyingi tu zilizoundwa na Maraisi mbalimbali. Imekuwa kama utamaduni kuzipa Tume hizo majina ya wenyeviti wake. Mifano michache ni, Tume ya Edward Ayila,Tume ya Jaji Nyalali,Tume ya Warioba,Tume ya Jaji Kipenka n.k. I dont think one has to read too much into the name "Tume ya Edwin Mtei."
 
Well said!
 
Mkandara wrote:
KNKU,
Well, kusema kuwa kuundwa kwa TRA imetokana na mapendekezo ya Tume ya Mtei!..
inanipa picha nzima ya mwandishi kama mwandishi mmoja aliyesema - Chama cha Mrema badala ya jina la chama sijui kama umeelewa!

KNKU,
Lengo hapa ni Wachaga na siyo kitu kingine. Kila tume imekuwa ikipewa jina la mwenyekiti wake: Tume ya Jaji Warioba, Tume ya Jaji Nyalali, Tume ya Jaji Mussa Kipenka,Tume ya Brig.Gen.Hashim Mbita.

Utamaduni huu wa kuzipa tume majina ya wenyeviti wake ni suala la KIMATAIFA. Unaweza kurudi nyuma mpaka miaka ya 1960 kulikuwepo Tume ya Chief Justice Warren iliyochunguza kifo cha Raisi Kennedy. Ripoti ya Tume hiyo inatambulika kama Warren Commission Report. Kuna tume ya kuangalia masuala ya Iraq, Baker- Hamilton Commission. Koffi Annan naye alichunguzwa na Tume ya Paul Volker.

Kusema TRA imeanzishwa kutokana na mapendekezo ya Tume ya Edwin Mtei imekuwa nongwa!!
Ndiyo maana mimi nikajisemea hii forum imekuwa kama gazeti la Kangura. Huu UKABILA jamboforums haukuanza na thread hii.
 
Jokakuu,
Tume ya Mtei ilikuwepo 1989 ktk kuitazama sera ya kodi.. sioni kabisa uhusiano wa kuundwa kwa TRA, unless wewe una maana nyingine unapotumia jina la Mtei.
 
KNKU,
Tume ya Mtei ilihusu mapendekezo ya sheria za kodi nchini mwaka 1989 hakuna kipengele kinachosema kuvunjwa kwa uongozi wa zamani ama kuundwa kwa TRA. TRA imeundwa mwaka 1995 chini ya kifungu cha sheria (act) namba 11. nadhani unaelewa Act inatokana vipi.
 
Mkandara wrote:
Jokakuu,
Tume ya Mtei ilikuwepo 1989 ktk kuitazama sera ya kodi.. sioni kabisa uhusiano wa kuundwa kwa TRA, unless wewe una maana nyingine unapotumia jina la Mtei.

Mkandara,
Ndiyo, Tume ya Mtei iliundwa mwaka 1989. Kuvunjwa kwa idara za ushuru na kodi ya mapato, na kuundwa kwa TRA, ni kati ya mapendekezo ya tume hiyo.

Tume hiyo ilichukua muda kidogo kufanya kazi yake, na sina uhakika walitoa ripoti yao mwaka gani. Ninachoelewa Kamishna Mkuu aliteuliwa na Raisi Mwinyi, na Bodi iliteuliwa na kuzinduliwa wakati wa Raisi Mkapa.
 
Mkandara!
Lakini isije ikawa katika mapendekezo ya sheria ya kodi Nchini hiyo tume ilitoa na mapendekezo ya kuvunjwa mamlaka ya mapato ya zamani na kupelekea kuundwa huko kwa TRA 1995?
 
KNKU,
Kuundwa kwa TRA hakuna tofauti na kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi. Mswada wa sheria ya vyama vingi ulitokana na mapendekezo ya Tume ya Jaji Nyalali.

Vyombo kama Idara ya Ushuru na Forodha, na Kodi ya Mapato vilikuwepo pale kwa mujibu wa sheria ya Bunge. Ili kuviondoa vyombo vile na kuunda TRA serikali ndiyo ililazimika kupeleka mswada bungeni.

Kinachogomba hapa ni hilo jina EDWIN MTEI na kabila lake MCHAGA.
 
This mwanakijiji is FOOLiNG YOU ALL!!!!!!why can't you STOP THIS TOPIC??!!

YEYE NDIYE MWENYE DEFINITION SAHIHI YA UKABILA,

SASA MWANAKIJIJI LENGO LAKO HASA NI NINI JUU YA HII TOPIC?

MAANA KILA IKIWEKWA SAWA UNAGEUZA WATU VICHWA CHINI MIGUU JUU!!!!!!!!!!!
 
naona wanajaribu kuonesha ukabila ulianzia wapi:

Edwin Mtei - Mchagga - tume iliyorekebisha TRA
Edwin Mtei - Kiongozi wa Chadema
TRA -imejaa wachagga - iliundwa kutokana na tume ya Mtei (Mchagga) ambaye baadaye alikuwa ni mwasisi wa Chadema (chama kinachodaiwa kuwa cha Wachagga)!

Wow... break the principle and the principle will find a way of breaking you... keep going
 
This mwanakijiji is FOOLiNG YOU ALL!!!!!!why can't you STOP THIS TOPIC??!!

YEYE NDIYE MWENYE DEFINITION SAHIHI YA UKABILA,

SASA MWANAKIJIJI LENGO LAKO HASA NI NINI JUU YA HII TOPIC?

MAANA KILA IKIWEKWA SAWA UNAGEUZA WATU VICHWA CHINI MIGUU JUU!!!!!!!!!!!

Mkira umenivunja mbavu!!! yaani nusura nipaliwe...
 
Jokakuu,
Hiyo tume iliwakilisha lini mapendekezo yake. .... 1989.

Je, unayo mapendekezo ya tume hiyo ama unafanya kubisha tu ili mradi makosa uliyoyafanya yapate uzito na kuendeleza issue!.

Sintapenda kubishana zaidi maanake sioni hata faida ya mjadala mzima!.
 
Back
Top Bottom