Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Dua nielekeze iliko link ya mazungumzo ya ukabila wa wachagga Bungeni.....I think I missed it
 
Dua, nilichohofia ndicho ulichofanya. Nimepitia mjadala wa Bunge kama ulivyonielekeza na nimeuweka hapa neno kwa neno!

MHE. STEPHEN M. KAHUMBI: Mheshimiwa Spika, kwanza nakushukuru
kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, naomba niombe Mungu anisaidie kwa sababu tangu nimeingia kwenye Bunge hili sijazungumzia habari kama ninayotaka kuizungumza hapa. Kwa hiyo, ni mara yangu ya kwanza kuzungumzia habari ya Idara. Mheshimiwa Spika, kazi yetu Wabunge ni kushauri na siyo kutafuta malumbano. Hatutaki kulumbana na mtu, hatulumbani na Waziri wala hatulumbani na wafanyakazi wa Idara.

Mheshimiwa Spika, tarehe 29 Julai, 2004 ilitolewa hotuba ya Waziri wa Kazi na
Maendeleo ya Vijana na Michezo, katika hotuba hiyo mimi nilitoa maelezo kuhusu
mfanyakazi wa TRA aliyefukuzwa kazi kule Mbeya. Mfanyakazi huyo alifukuzwa kwa
sababu alitoa msamaha wa kodi kwa mabati yaliyonunuliwa na Kanisa, Mbeya,
akaonekana cheo chake ni kidogo kutoa msamaha akafukuzwa kazi. Huyo alikwenda
kwenye Baraza la Usuluhishi la Mkoa wa Mbeya, Mkoa wa Mbeya ulitafuta ushahidi
mbalimbali ukapatikana kwamba haikuwa mara ya kwanza kwa huyo mtu kutoa
msamaha kwa sababu mkubwa wake wa Idara alikuwa mgonjwa.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, wakasema adhabu aliyopewa ni kubwa mno
asamehewe, arudi kazini ila apewe onyo. Mkubwa wake wa kazi kwenye kikao hicho
akasema yeye hawezi kukubali kushindwa na mwanamke. Sasa huyo mwanamke akawa
amepata ushindi wa Baraza la Usuluhishi la Mkoa Mbeya. TRA hawakuridhika kwa
kushindwa na mwanamke, wakaomba rufaa kwa Waziri. Mheshimiwa Profesa Juma
Kapuya, akakaa nadhani Wizara ya Kazi na Maendeleo ya Vijana na Michezo inajua sheria za kazi, wakatoa uamuzi kwamba kwanza tuhuma walizomtuhumu hazikuthibitika.
Kwa hiyo, arudishwe kazini. Mtu huyo hakurudishwa kazini.

Mimi nimekuwa nawasiliana na Mheshimiwa Waziri wa Fedha na watu wa TRA
hata tumezungumza hapa Bungeni na Commissioner Mkuu wa TRA akaniambia
atalipeleka kwenye Bodi na kwamba ana kesi za namna hiyo saba za watu waliopitishwa
na Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana na Michezo kurudishwa kazini, lakini
hawajarudi kazini. Mimi nikaona ahaa, basi niache na nikamweleza wazi kwamba mimi
na Mheshimiwa Basil Mramba tumefanya kazi SIDO kwa muda wa miaka 10 wala sina
haja ya kukabiliana naye Mheshimiwa Basil Mramba, ni mkubwa wangu tumefanya naye
kazi vizuri sana. Sasa nikaona hakuna kinachoendelea na ndiyo nikasema kwenye hotuba
ya Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana na Michezo, athibitishe kwamba alimwona
na hatia huyo au hapana. Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana na Michezo kwa
kujibu hoja yangu Bungeni, Hansard imetoka ya tarehe 29 Julai, 2004. Mheshimiwa
Waziri anasema: "Mheshimiwa Stephen Kahumbi, alizungumzia kuhusu mtumishi wa
TRA, nataka nimhakikishe Mheshimiwa Mbunge kwamba tutajitahidi kulifanyia kazi hilo
tatizo la huyo mfanyakazi kwa sababu mimi naamini Serikali ni moja na Waziri wa Kazi
anapoamua anaamua kwa niaba ya Serikali ile ile."

Kwa hiyo, nadhani Mawaziri wengine vile vile wanajua kwamba lazima tuheshimiane. Waziri wa Kazi, Maendeleo ya Vijana na Michezo anasema na akakazia kwamba, atarudi kazini ikilazimika atakaza hukumu, imeandikwa kwenye Hansard ya tarehe 29 Julai, 2004.
Mheshimiwa Spika, cha kushangaza watu wa TRA wanaona kama mimi ninaconfrontation nao. Leo wameniletea barua kwa EMS ambayo haina ukweli wowote.
Ninasikitika ninayo hapa yaani baada ya kusikia tunazungumza humu Bungeni wakakaa
kule Dar es Salaam kupinga Bunge. Imeandikwa tarehe 2 Agosti, 2004 mimi
nilizungumza tarehe 29 Julai, 2004. "Hii ni kukujulisha kuwa msimamo wa Mamlaka ya
Mapato ya Tanzania ni kuwa haikubaliani na maamuzi yaliyotolewa na Baraza la
Usuluhishi Mbeya kupitia karatasi namba 5 yenye kumbukumbu namba hiyo ya tarehe 12
Desemba, 2001. Mamlaka ya Mapato ilipokea uamuzi uliotolewa na Mheshimiwa
Waziri wa Kazi, Maendeleo ya Vijana na Michezo kupitia karatasi namba 8 yenye
kumbukumbu namba hiyo ya tarehe 17 Desemba, 2002." Hasemi sasa wanaifanyaje hiyo
barua ya Mheshimiwa Waziri. Lakini anaruka anasema: "Tunapenda ufahamu kuwa
Sheria iliyotumika katika kulishughulikia suala lako ni Sheria ya Usalama ya Kazini
namba 62 ya mwaka 1964 kama ilivyorekebishwa na kitendo namba 1/195 inamruhusu
mwajiri kukurudisha kazini au kutokurudisha kazini." Sheria hii inamruhusu private employer siyo employer wa Serikali. Huyu mtumishi hakuwa mtumishi wa Commissioner, alikuwa ni mtumishi wa Serikali. Mwajiri binafsi anaruhusiwa kwamba mimi unaniambia huyu mtumishi wangu hana kosa, nakubali hana kosa, lakini simtaki. Kwa hiyo, nampa mshahara wa miezi mitatu, off. Huyo mtumishi hakuwa mtumishi wa mtu alikuwa ni mtumishi wa Serikali kama Commissioner mwenyewe. Kuna provision yake na provision yake imehukumiwa na 45 Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana na Michezo, anadharauliwa Commissioner wa Kazi maana yake nini? Tuna Serikali ngapi hapa? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa madhumuni ya kuomba niseme hapa, nilitaka kusema
mambo mawili, matatu. La kwanza, mimi sina chuki na watu wa TRA wala huyo
mtumishi wao, mimi Mbeya sijafika. Sina chuki nao lakini si mwoga kutetea haki ya
mtu. Kuna Waheshimiwa Wabunge wenzangu wameniambia Stephen Kahumbi, acha tu
kwani nani, mimi huwa nimezoea kufanya confrontation ikilazimika. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, huwezi ukaacha mtu anaonewa kwa kuvunja sheria. Kwa
sababu mtu hajui sheria kwamba hii inayosemwa ni ya nani? Kuna sheria mbili,
mfanyakazi wa Serikali huwezi ukamhukumu kwa sheria ya wafanyakazi wa ofisi za
watu binafsi, kama unamchukia ondoka wewe. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, mimi nikiwa mfanyakazi niliomba uhamisho kutoka shule
fulani kwenda shule fulani kupitia kwa DC. DC akaniambia wewe unaomba uhamisho
kwa kumkimbia Headmaster, je, ukipelekwa Sumbawanga naye kesho akahamishwa
kwenda Sumbawanga utamkimbia tena? Kaa naye mpambane naye hapa hapa
tukapambana mpaka tukaachanishwa yeye kaenda Tabora na mimi nikaenda
Sumbawanga. Sasa huu uamuzi wa chuki binafsi, hii ni chuki au ubaguzi, ukabila,
mwanamke. Ni kosa kuwa mwanamke? (Makofi)

Naomba hilo wafahamu kwamba mimi sina chuki nao. Hawa watu wa TRA kama
walikuwa wanataka kumfukuza kazi wangempelekea Waziri wa Kazi na Maendeleo ya
Vijana na Michezo. Hawakumpelekea Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana na
Michezo barua hii aliyesema atakaza hukumu siyo mimi. Sasa kwa nini
hawakumpelekea Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana na Michezo wananiletea
mimi, mimi ni nani, mimi ni Mbunge nilikuwa nawashauri tu. Sasa naomba ieleweke
kwamba Waziri wa Fedha hawa watu wake kama anawaunga mkono waungane mkono.
Ila mimi nakuomba kwa suala hili uitume Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi,
ichunguze ukweli wa hili jambo. Hatuwezi kuvumilia watu wanaonewa kwa sababu ya
ubaguzi sijui ukabila au nini haiwezekani. (Makofi)

Mimi nimekaa hapa Bungeni tangu mwaka 1985 mlishanisikia nikisema habari ya
mtu hapa hata siku moja lakini they are knowing. Naomba aidha, Waziri wa Fedha
amuunge mkono Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana na Michezo kwamba huyo
mtumishi anarudishwa kazini au basi kwa sababu ni Bunge limedharauliwa na mimi
sikusema nje huko kwenye Kantini nilisema hapa hapa Bungeni. Kwa nini kuruhusu
Bunge lidharauliwe kiasi hiki? Nilikuwa naomba wakati Waziri wa Fedha rafiki yangu
Mheshimiwa Basil Mramba ana-wind up anieleza anamwambia huyo amrudisha kazini.
Maana Mheshimiwa Profesa Juma Kapuya, aliyesema, sisemi Mheshimiwa Profesa
Juma Kapuya kwa sababu anatoka Tabora. Nilisema hapa Bungeni kwamba ni halali na
ni vizuri zaidi, kuchinja kuku wako utalaumiwa na mimi nikasema nakuchinja wewe
Mheshimiwa Profesa Juma Kapuya, kwa sababu Mheshimiwa Profesa Juma Kapuya,
unatoka Tabora kwa hiyo, nikikutolea shilingi wewe ndiyo vizuri. (Makofi)

Sasa na hapa simtetei Mheshimiwa Profesa Juma Kapuya, kwa sababu anatoka
Tabora naitetea Serikali, Mheshimiwa Profesa Juma Kapuya, ni Waziri wa Serikali,
anachosema ni amri watu wa TRA lazima wafahamu.Waziri yeyote anaposema ni amri
siyo anakubembeleza tutakuwa na Serikali ngapi. Naomba nielezwe kwamba huyo mtu
atarudishwa kazini aidha Commissioner anampenda au hampendi mimi sijui. Kama sivyo
hivyo nina heshima sana nakuomba uitume Kamati ya Fedha na Uchumi, ichunguze
ukweli wa kufukuzwa kazi kwa huyo mtu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. (Makof)


Je Bunge lilizungumzia Ukabila TRA jibu ni HAPANA! Siyo Mbunge Kahumbi wala Mbunge mwingine aliyezungumzia "Ukabila" TRA kama Dua unavyotaka watu tuamini. Maneno "Ukabila" yanaonekana mara tatu na mara zote hayako peke yake.
Mara ya kwanza:

Sasa huu uamuzi wa chuki binafsi, hii ni chuki au ubaguzi, ukabila, mwanamke. Ni kosa kuwa mwanamke?

Mara ya pili:

Hatuwezi kuvumilia watu wanaonewa kwa sababu ya ubaguzi sijui ukabila au nini haiwezekani.

Mara ya tatu wakati Mramba anajibu hoja

hakuna mtu aliye na nia mbaya wala husuda wala ukabila wala uovyo ovyo tu kufanya kazi bila kutafakari.


Hivyo, ni lazima tukubali kuwa "ukabila TRA" haukuzungumzwa!! Katika hoja ya Kihembu alikuwa anashangaa ni kitu gani kinaweza kusababishwa mtu kutorudishwa kazi na akajaribu kujenga nadharia za kuhisi kuwa yawezekena ni chuki, ubaguzi, ukabila au nini, HAKUWA anathibitisha kuwa kuna ukabila TRA!!

Wakati Mramba anajibu hizo hoja alisema wazi kuwa 'HAKUNA' ubaguzi au ukabila huo!!! Kama Waziri mwingine alitoa amri na sisi tunatakiwa kuyapokea maneno ya waziri huo kama sheria, kwanini tusikubali maneno ya Waziri mwingine kuwa Hakuna ukabila TRA? Of course, jibu lenu liko wazi kwa vile aliyesema ni waziri Mchagga!!!

jokaKuu

1.) Kwa hiyo unakubali kwamba swala hili lilizungumziwa bungeni kuhusu ukabila pale TRA. Je unaweza kufuta usemi wako kwangu, Mswahili na wengineo wa maneno yako haya:

wrong never happened!!

Hili swala ambalo limezungumzwa kwa kirefu katika bunge la Tanzania haliwezi kuwa sawa na maneno uliyoandika hapo juu kwa wanabodi.

wrong again! never happened.. not kwa kirefu not hata kwa kifupi!

2.) Je kama TRA hawakuwa na makosa ni kwa nini walilipa 'compensation'?

si kwa sababu walikuwa na makosa, ni kwa sababu hawakutaka kumrudisha kazini!!

3.) Je wewe ni kati ya wale wanaofaidi na uendekezaji wa ukabila pale TRA?

Hakuna ukabila TRA na wala hakuna uendekezaji wa kitu ambacho hakipo!!

Only in Tanzania maamuzi ya waziri yanaweza kupuuzwa na viongozi wa ngazi ya chini yake, iko siku tutapata wasafishaji wa hii system iliyooza.

You got that right.. only in Tanzania ambapo maneno ya waziri hayawezi kukosolewa na amri za mawaziri ni sheria!! lakini Mawaziri na wenyewe wanabanwa na sheria hizo hizo!! Kwa vile Waziri kaweka sahihi haina maana lazima ikubaliwe hasa kama ni kuvunja sheria!!

Dua kama kweli unafuatilia haya mambo utaona kuwa mhe. Kihembu alikuwa anazungumzia ubaguzi mwingine kabisa kama anavyosema hapa:

Mkubwa wake wa kazi kwenye kikao hicho akasema yeye hawezi kukubali kushindwa na mwanamke. Sasa huyo mwanamke akawa amepata ushindi wa Baraza la Usuluhishi la Mkoa Mbeya. TRA hawakuridhika kwa kushindwa na mwanamke,

Je unaweza kufikiri ni ubaguzi gani aliokuwa anaufikiria Mheshimiwa Kihembu?
 
Mzee Mwanakijiji,
Nakuaminia kwa jinsi unavyopangua mashambulizi hayo. Hii ni kali ya mwaka maana katika yote neno ukabila kuonekana tayari inaonyesha kuna ukabila. Mweee!
 
Nakumbuka kuna mbunge wa kutoka mkoa wa Mara-nadhani Ibrahim Marwa (Musoma Mjini, CCM) aliwahi kuzungumzia madai/shaka/tuhuma/shutuma za ukabila hasa katika Wizara ya Fedha na asasi zilizo chini yake, zikiwemo Benki Kuu, TRA, IFM na DSAs (Dar, Singida etc). Kama sikosei ilikuwa kwenye moja ya vikao vya 2005.Nikipata fursa nitapitia hansard kuona kwa uhakika alisema nini.
 
Kweli kabisa Mwanagenzi huyu Mbunge aliweka wazi jambo hilo la ukabila TRA. wanaobisha wawahoji Maboss wa TRA KAMA waliwahi kufikishwa bungeni kwa tuhuma za ukabila tena uchagga.

Mwanakjiji.

umeunda tume kabla hatujafanya kazi umekuja na hoja nyingine ya kuwahoji TRA. jee kazi za TUME YA MWANAKIJIJI zimekamilika? au tunazidi kulikoroga humo humo?

kwenye mahojiano apatikane na phillimon mikael, Joka kuu. mtu kwao.

na mabosi wa TRA usikose kumuoji Lauwo kwa kumuweka mdogo wake na kuwa ndio mpitishaji wa mizigo michafu. halafu uliza uhalali wa Kittilya kwenda kufanya harambee za kusaidia jimbo la mramba nyumbani kwa mramba na kuwashinikiza wafanya biashara watoe pesa kwa nguvu. kulifanyika mikutano zaidi ya 20 na yote Mramba anaanza kuhutubia halafu anaonesha picha za miradi ya jamii jimboni kwake halafu unasimamishwa mfanyabiashara mmoja mmoja unaambiwa ujifunge kitanzi. huku Kittlya akikukodolea mimacho.

Wafanyabiashara wote wakubwa wamekumbwa na rungu la Mramba na kittlya hapo nyumbani kwa Mramba.

ulisikia kisa na sababu ya kumfukuza kazi Benny Lusege tena cha ajabu aliporudi tu masomoni akiwa na masters badala ya kupandishwa cheo au kubaki alipokuwepo mwanzo akashushwa na kuwa examination officer toka kwenye Officer incharge.na ilikuwaje akarudishwa kazini.
Foyi aliyekuwa RRO alimfanyia nini benny lusege?

Imekuwaje kituo cha ushuru kikawekwa Holili kwa Mramba huku akiwa waziri wa wizara husika(Fedha) na iweje kituo hiki kitumike kukwepa ushuru na serikali imeipa amri TRA kuweka T-SCAN hapo, hadi sasa zaidi ya mwaka hakuna jibu LOLOTE.
 
Mahojiano hayo mimi yananitia wasiwasi kama yatakuwa fair, coz mtu aliyeyaanda hayo mahojiano hakubaliani na kuwepo kwa huo unaoitwa ukabila, kweli haki itatendeka hapa???
 
MKJJ et al....................

Unaweza kuandika vizuri kama hadithi ili kuonekana kama kuna ukweli lakini unapotosha wale ambao hawasomi na kuelewa kinachoongelewa kwa kimazingaombwe.

Hoja niliyotoa kutokana na kilichojadiliwa bungeni ni hii hapa: http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=1867&page=71
Rejea kikao cha Bunge (Majadiliano ya Bunge mkutano wa 16 kikao cha 41 August 2004) Mhe Stephen M Kahumbi alipotoa hoja ya TRA kukataa kumrudisha kazini mfanyakazi kule Mbeya ingawa alifuata taratibu zote kwenye Baraza la usuluhishi la Mkoa Mbeya. TRA hawakuridhika kushindwa na kukata rufaa kwa Waziri.

Lakini na huko walishindwa na kwa ajili ya kuendeleza ukabila waligoma kumrudisha kazini. Hawa wanakiburi hata kupinga amri ya waziri. S.Kahumbi alisema Waziri wa kazi anapoamua anaamua kwa niaba ya Serikali ile ile, lakini huyo Commissioner ambaye naye ameajiriwa na Serikali ameifanya TRA kama kampuni yake binafsi.

http://www.parliament.go.tz/Polis/PA...16-41-2004.pdf


MKJJ Je Bunge lilizungumzia Ukabila TRA jibu ni HAPANA! Siyo Mbunge Kahumbi wala Mbunge mwingine aliyezungumzia "Ukabila" TRA kama Dua unavyotaka watu tuamini. Maneno "Ukabila" yanaonekana mara tatu na mara zote hayako peke yake.
Mara ya kwanza:
Sasa huu uamuzi wa chuki binafsi, hii ni chuki au ubaguzi, ukabila, mwanamke. Ni kosa kuwa mwanamke?
Mara ya pili:
Hatuwezi kuvumilia watu wanaonewa kwa sababu ya ubaguzi sijui ukabila au nini haiwezekani.
Mara ya tatu wakati Mramba anajibu hoja
hakuna mtu aliye na nia mbaya wala husuda wala ukabila wala uovyo ovyo tu kufanya kazi bila kutafakari.
Hivyo, ni lazima tukubali kuwa "ukabila TRA" haukuzungumzwa!! Katika hoja ya Kihembu alikuwa anashangaa ni kitu gani kinaweza kusababishwa mtu kutorudishwa kazi na akajaribu kujenga nadharia za kuhisi kuwa yawezekena ni chuki, ubaguzi, ukabila au nini, HAKUWA anathibitisha kuwa kuna ukabila TRA!!

Sasa wewe ulitaka mbunge aongelee ukabila kwa tafsiri yako. Hapa umenoa Mzee kwa sababu hata kama angetaja ukabila mara moja tayari amekwisha liongelea hilo na hivyo kuihusisha TRA moja kwa moja. Kwa nini mathalani asiongelee ukabila na kutaja Dodoma au Dar Es salaam? hapa naona unataka kutuletea mazingaombwe ambayo tayari Tabasamu anachekelea. Mtu anafungwa kwenda jela kwa sentesi au neno moja na kama hufahamu panapofuka moshi pana moto.

Wakati Mramba anajibu hizo hoja alisema wazi kuwa 'HAKUNA' ubaguzi au ukabila huo!!! Kama Waziri mwingine alitoa amri na sisi tunatakiwa kuyapokea maneno ya waziri huo kama sheria, kwanini tusikubali maneno ya Waziri mwingine kuwa Hakuna ukabila TRA? Of course, jibu lenu liko wazi kwa vile aliyesema ni waziri Mchagga!!!
Ulitegemea waziri aseme nini? Yeye kama ni mchaga na anashiriki katika kuendeleza ufisadi pale TRA, mifano mingi tumekupa kuhusu huyu waziri lakini kwa sababu moja au nyingine unalifumbia macho, je ni miradi mingapi amepeleka jimboni kwake? Je kuna bandari Rombo? Rudia hoja zilizotolewa mwanzo na uje na majibu muafaka - huwezi kuleta mazingaombwe yako hapa jaribu mahali pengine.

jokaKuu

1.) Kwa hiyo unakubali kwamba swala hili lilizungumziwa bungeni kuhusu ukabila pale TRA. Je unaweza kufuta usemi wako kwangu, Mswahili na wengineo wa maneno yako haya:

wrong never happened!!
It happened as mentioned above on your own words three times, Why do you think it was mentioned? To please you and your clan? NO
Hili swala ambalo limezungumzwa kwa kirefu katika bunge la Tanzania haliwezi kuwa sawa na maneno uliyoandika hapo juu kwa wanabodi. wrong again! never happened.. not kwa kirefu not hata kwa kifupi!
Utaendelea kubisha kama vile tulivyokupa tafsiri ya DENY kwani hilo ndio ujualo.

2.) Je kama TRA hawakuwa na makosa ni kwa nini walilipa 'compensation'? si kwa sababu walikuwa na makosa, ni kwa sababu hawakutaka kumrudisha kazini!!
''Sheria ya usalama ya kazini namba 62 ya mwaka 1964 kama ilivyorekebishwa na kitendo namba 1/195 inamruhusu mwajiri kukurudisha kazini au kutokurudisha kazini'' Sheria hii inamruhusu private employer siyo employer wa serikali. Huyu mtumishi hakuwa mtumishi wa Commissioner, alikuwa mtumishi wa serikali Mwajiri binafsi anaruhusiwa kwamba mimi unaniambia huyu mtumishi wangu hana kosa, nakubali hana kosa lakini simtaki. Kwa hiyo nampa mshahara wa miezi mitatu off.. Kukataa kumrudisha kazini maana yake ni nini? Uliona wapi mtu analipwa fidia wakati hakuna aliyekosea. Another mazingaombwe kutoka kwa Mwana kijiji. Bali angekuwa Mchaga ungemtetea mpaka kufa.

3.) Je wewe ni kati ya wale wanaofaidi na uendekezaji wa ukabila pale TRA? Hakuna ukabila TRA na wala hakuna uendekezaji wa kitu ambacho hakipo!!
Kwa mawazo yako ni sahihi kwa sababu uchungu wa kulitumikia taifa ni kwa wachaga kwa hiyo sio ajabu.

Only in Tanzania maamuzi ya waziri yanaweza kupuuzwa na viongozi wa ngazi ya chini yake, iko siku tutapata wasafishaji wa hii system iliyooza. You got that right. only in Tanzania ambapo maneno ya waziri hayawezi kukosolewa na amri za mawaziri ni sheria!! lakini Mawaziri na wenyewe wanabanwa na sheria hizo hizo!! Kwa vile Waziri kaweka sahihi haina maana lazima ikubaliwe hasa kama ni kuvunja sheria!!

Dua kama kweli unafuatilia haya mambo utaona kuwa mhe. Kihembu alikuwa anazungumzia ubaguzi mwingine kabisa kama anavyosema hapa:

Mkubwa wake wa kazi kwenye kikao hicho akasema yeye hawezi kukubali kushindwa na mwanamke. Sasa huyo mwanamke akawa amepata ushindi wa Baraza la Usuluhishi la Mkoa Mbeya. TRA hawakuridhika kwa kushindwa na mwanamke,

Je unaweza kufikiri ni ubaguzi gani aliokuwa anaufikiria Mheshimiwa Kihembu?

Bado unaendeleza mazingaombwe kwani issue iliyonifanya niweke hii artical ipo hapo juu na si kweli kwamba ni taboo kuongelea ukabila unaoendeshwa na wachaga pale TRA. Hatuwezi kubadili neno hilo ili kukufurahisha wewe au wale ambao wanaendeleza ukabila.
 
Kitendo cha kuutaja ukabila mara tatu kwenye mazungumzo ya Mbunge ni dalili tosha anasisitiza kitu gani.

mbona hakusema neno udini? neno ukabila limetajwa sana likiambatana na ubaguzi. huo ni ushahidi wa wazi labda mtu awe makengeza.

hakuna neno lililosisitizwa kama ukabila.

kabla ya uchaguzi mkuu REDET walisema kikwete ni chaguo la watu wengi kwani anatajika sana, wakaja watu kama mwanakjj wakabisha hapana, ikaja BBC-SWAHILI wakasema jina la JK limetajwa sana kwa kitendo cha kutajwa anaweza kuwa ndio mwenye mvuto kati ya wagombea wa ccm akaja Mwandosya na wengine wakapinga sio kweli. lakini ukweli ukaja kudhihiri kuwa kweli anakubali na watu kuliko wagombea wengine hata siku alipotajwa Dodoma kuwa ni mshindi-Dar hakukalika kwa shangwe.

mfano huu ni kuwasaidia watu kuwa ukabila umejirudia sana ktk hoja ya mbunge Kahumbi. hiyo ni dalili tosha TRA kuna moto unawaka wa ukabila.

Mwanakijiji.

tunaomba mahojiano haya umpate na MHANGA WA UKABILA TRA bwana Benny Lusege atupe yaliyomsibu nitakutumia number yake kwenye PM.
NA kina mzee ngairi ambao tuliambiwa ni ma examination officer,

jitahidi umpate na charles huyu nae kamaliza masters na ana uzoefu mzuri lakini kwa vile hatoki Kilimanjaro amekuwa akiwekewa usiku tu. yupo ukaguzi wa viwandani.

nitakutumia orodha ndefu ya wahanga wengine kwenye pm humu tutaharibu ushahidi na inawezekana wakaanza kuandamwa na kina Lauwo, msoffe, mmanda na baba lao kittlya.
 
angalieni neno mwanamke linatokea mara ngapi na neno ukabila linatokea mara ngapi.. ubishi mwingine hata hauna ubishi!
 
Hoja niliyotoa kutokana na kilichojadiliwa bungeni ni hii hapa:

http://www.jamboforums.com/showthrea...t=1867&page=71

So what is the issue then. Imekamilika kama ilivyo.

Hebu tuangalie kile ndugu Dua alichokisema halafu tuone kina ukweli kiasi gani.

Rejea kikao cha Bunge (Majadiliano ya Bunge mkutano wa 16 kikao cha 41 August 2004) Mhe Stephen M Kahumbi alipotoa hoja ya TRA kukataa kumrudisha kazini mfanyakazi kule Mbeya ingawa alifuata taratibu zote kwenye Baraza la usuluhishi la Mkoa Mbeya. TRA hawakuridhika kushindwa na kukata rufaa kwa Waziri.

Lakini na huko walishindwa na kwa ajili ya kuendeleza ukabila waligoma kumrudisha kazini. Hawa wanakiburi hata kupinga amri ya waziri. S.Kahumbi alisema Waziri wa kazi anapoamua anaamua kwa niaba ya Serikali ile ile, lakini huyo Commissioner ambaye naye ameajiriwa na Serikali ameifanya TRA kama kampuni yake binafsi.

maneno "kuendeleza ukabila" ni maneno yako na hayana ushahidi katika mazungumzo ya Bunge! Kahumbi alikuwa anazungumzia bosi kutamba kuwa hawezi kushindwa na "mwanamke" na Mbunge kwa uhalali alihoji jambo hilo kuwa haiwezekani mtu asirudishwe kazini kwa sababu ni mwanamke, au chuki binafsi, au husuda, ubaguzi au ukabila!! Hakusema hata mahala pamoja kuwa huyo mdada hakurudishwa TRA sababu ya Ukabila hayo ni maneno yako yasiyo na msingi hata chembe!! kwanini usichague husuda, chuki, ubaguzi na umeng'ang'ania ukabila?

Kwa vile hukutaka kujibu ni mara ngapi neno "mwanamke" linatokea kwenye mazungumzo ya Bunge nitakusaidia.... inatokea mara tano, five, (5)! kuliko neno ukabila!!!!! Uniambie wewe Mbunge alitaka kusisitiza ukabila au jinsia?

ukasema hivi:

It happened as mentioned above on your own words three times, Why do you think it was mentioned? To please you and your clan? NO

This one is personally offensive! if you can't argue without attacking one's person (ad hominem) don't argue at all, it is immature, uncalled for, and indeed unpallatable! Kama unataka kunitukana just go ahead na mtukane mamangu, if that will make your arguments a little bit stronger!
 
MKJJ
This one is personally offensive! if you can't argue without attacking one's person (ad hominem) don't argue at all, it is immature, uncalled for, and indeed unpallatable! Kama unataka kunitukana just go ahead na mtukane mamangu, if that will make your arguments a little bit stronger!

Umeona hilo ni tusi siyo?
As I told you before, umeamua kuja na mazingaombwe yako. Deny to the end of the world but the truth will remain the same and people will continue to suffer because of few individuls who think its their own right to continue with their tribalism. But let me assure you it will end very soon with you agreeing or not.
 
MKJJ,

kwa nini ulichukua dataz za mswahili na kuwapelekea maboss wa TRA kwa nini usisubiri mpaka hiyo siku ya mahojiano uwaulize na sisi sote tusikie majibu yao????
 
duh! sasa niwaulize kitu wasichokijua.. kama data za mswahili ziko sahihi itabadilisha kitu gani? Na mswahili bado nasubiri jibu lake na contacts zake...hadi hivi sasa ni Dua tu aliyetayari kushiriki majadiliano hayo. Na si mahojiano, ni mazungumzo kati ya Watanzania. Wale wanaofikiri kuwa lengo ni kutafuta uadui, au ni mazugumzo ya maadui hawanielewi vizuri. Kuna baadhi ya ndugu zetu Watanzania ambao wanaona kuwa ndugu zao Watanzania wenzao ni wakabila. Sasa tunataka kuwapa nafasi ya kuzungumza pamoja siyo kutegana na kuumbuana.

Pili siwezi kuwashikirisha watu wote kwenye mahojiano hayo nahitaji watu si zaidi ya sita. Hadi hivi sasa mimi (moderator - sina upande), maafisa wawili wa TRA (wanaodai hakuna ukabila) na wajumbe wawili (Dua, Mswahili???, Mkandara??? - wanaodai ukabila upo) na tunaweza kuongeza mtu mmoja au wawili... otherwise hautakuwa mjadala wa watu wenye akili!!
 
Dua,

OK, ngoja nijibu maswali yako ili mjadala huu usonge mbele.

Dua wrote: Kwa hiyo unakubali kwamba swala hili lilizungumziwa bungeni kuhusu ukabila pale TRA. Je unaweza kufuta usemi wako kwangu, Mswahili na wengineo wa maneno yako haya:


Ni kweli kwamba Mheshimiwa Kahumbi alidai bungeni kwamba yuko mtumishi wa tra aliyefukuzwa kwa uonevu na akadai uonevu huo unaweza kuwa wa kikabila.

Madai hayo yalikuja kuwa refuted with FACTS na waziri wa Fedha. Mbunge aliridhika kwamba madai yake hayakuwa na msingi wowote ule.

Binafsi nilikuomba u-quote kauli ya Mbunge pamoja na ile ya waziri wa Fedha ili kuonyesha kama uko FAIR katika suala hili. Wewe uliendelea na msimamo wako wa ku-quote maelezo ya Mbunge peke yake.

Maelezo ya Waziri wa Fedha yalidhihirisha kwamba Mbunge Kahumbi hakuwa ameyafanyia utafiti madai yake. Mbunge mwenyewe alikubaliana maelezo na ushahidi aliotoa waziri wa fedha.

Mimi naamini ulikuwa na NIA MBAYA ulipo-quote madai ya Mbunge ambaye amekiri kwamba hakuwa ameyafanyia utafiti. Maelezo kwamba ulitoa link ya mjadala mzima hayana uzito hapa. Binafsi ningekuelewa kama ungetoa link ya mjadala bila ku-quote maneno ya kichonganishi na chuki ya Mbunge Kahumbi.

Dua wrote: Je kama TRA hawakuwa na makosa ni kwa nini walilipa 'compensation'?


Huyo Mama aliyefukuzwa kazi hakupewa "compensation." Hapa naona unazidi kujaribu kuwapotosha wana jamboforum. Kama TRA wangekuwa na makosa kama unavyodai, basi remedy ingekuwa kumrudisha huyo mama kazini, na kumlipa mishahara yake kwa kipindi chote alichokuwa nje ya kazi.


Vilevile ni katika mazingira yapi chombo chenye mamlaka ya kukusanya kodi kikawa na makosa kwa kumuachisha kazi mtumishi anayewasaidia wafanyabiashara kukwepa kodi?

TRA wametumia kipengele cha sheria kinachowaruhusu kumlipa mfanyakazi mtovu wa nidhamu mshahara wa mwaka mmoja na "kumuachisha" kazi.



Dua wrote: Je wewe ni kati ya wale wanaofaidi na uendekezaji wa ukabila pale TRA?
Hakuna kitu kama ukabila TRA. Hata kama ungekuwepo nisingefaidika kwa namna yoyote ile. Pamoja na hayo, Watanzania wote tunafaidika na uchapakazi na ufanisi wa watumishi wa TRA, bila kujali makabila,dini, ua jinsia zao.

Dua wrote:Only in Tanzania maamuzi ya waziri yanaweza kupuuzwa na viongozi wa ngazi ya chini yake, iko siku tutapata wasafishaji wa hii system iliyooza.


YES, only in tanzania waziri na wanasiasa wanaweza kutetea watumishi wa umma wanaogushi na kushiriki kuikosesha na kuiibia serikali kodi.
 
Mwalimu alituasa kuwa tusiendekeze ukabila na mambo ya kujuana makabila yawe na maana sana, labda, kwenye matambiko na utani...

Kulikuwa na mzee mmoja aliyeitwa Mushi ambaye alipata ajali mbaya sana ya gari na kiasi cha kufikishwa chumba cha mahututi akiwa hajitambui. Kwa kudra za Mwenyezi Mungu, baada ya siku kadhaa alizinduka, na baada ya kupata fahamu akawaita wauguzi wamweleze nini kilichomsibu. Mmoja wa wauguzi akaanza kumwelezea jinsi alivyopata ajali.

Mzee Mushi akamaka, “Ajali ya gari! Lile Benzi langu la mbei mbaya? Limeharibika eeh?”

Muuguzi akamtuliza, “Mzee ilikuwa ajali mbaya sana na gari liliharibika vibaya sana…nasikitika kukuambia kuwa mkono wako wa kushoto ulivunjika kabisa na tumeshindwa kuuunga.”

Mzee Mushi akauliza, “Nimepoteza mkono? Na saa yangu ya Rolex aliyoniletea mwanangu Godlove wa Marekani iko wapi?”


Muuguzi akajitahidi kumfariji Mzee Mushi akimwambia asijali sana maana Mungu akipenda atapata nyingine. Akamwambia, ”Tena familia yako iko hapa, wamekuja kukuona."

Basi Mzee Mushi akaagiza wapite ndani. Walipokuwa wameingia ndani ya chumba alichokuwa na wakiwa wamezunguka kitanda chake, akaanza kuwaita majina mmoja mmoja.

"Mama Manka, uko hapa?"

"Ndiyo mume wangu, siwezi kukuacha," mkewe akajibu.

"Manka, na wewe uko hapa?", mzee akauliza.

"Ndiyo baba, na mimi siwezi kukuacha, pole sana", binti akajibu kwa huzuni.

Mzee Mushi akaendelea, "Aikaeli, uko hapa pia?"

Kama wenzie, Aikaeli naye akajibu, "Ndiyo baba, siwei kukuacha."

"Elibariki mwanangu, na wewe uko hapa?" Mzee Mushi akauliza.

Elibariki, mtoto wa kiume wa Mzee Mushi, akajibu kwa kujiamini, "Ndiyo baba, siwezi kukuacha kamwe."

Baada ya kimya cha sekunde kadhaa, Mzee Mushi akasema,"Ninyi wapumbafu sana…kama Manka, Aikaeli, Elibariki na wewe mama yao wote mko hapa duka nani yuko dukani?”

Whats the moral of the story?

Maana umeiacha ina-hang bila kuleleza huu utani (au ukweli) unatoa picha gani kwa huyo Mushi!
 
mtukwao.. ni prejudice hii inayowasukuma kuona ukabila... wachagga=pesa, TRA ina pesa hivyo wachagga+TRA = ?
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji Nimewawekea ripoti nyingi ya:

a. Autonomy, Incentives, and Patronage - A study of Corruption in the Tanzanian and Ugandan Revenue Authorities.

Katika ripoti hiyo yenye kurasa 102 hakuna mahala hata pamoja ambapo Ukabila unatajwa isipokuwa kuhusu Uganda. Na huu ni uchunguzi huru, kama waliweza kujua kuna ukabila kwenye taasisi kama hiyo Uganda bila ya shaka wangesema hivyo kama wangenusa harufu yake TRA!!


Je maneno haya ni kweli? Au tunaona mazingaombwe mengine. Kama nilivyosema huko nyuma katika report hiyo neno ukabila limetumiwa sio zaidi ya mara moja. {Mwanakijiji anasema uchunguzi huru} - NORAD walifanya huu uchunguzi sio kwa swala la ukabila bali kwa malengo yao, ili waweze kupata ajira kwa ma-exparts wake kwenye nchi zetu hilo ndio lilikuwa muhimu kwao. Kwa Mawanakijiji hilo ni sahihi kwake lakini neno ukabila linapotumiwa katika Bunge la Tanzania mara tatu kama alivyotuhesabia sio kweli kwamba kuna harufu ya ukabila hapo TRA.

Yeye tu ndiye anayeweza kunusa harufu ya ukabila.

Maneno yaliyoandikwa kwenye ripoti hiyo haya hapa: In Uganda, it has also led to accusations of biased recruitment based on 'secterism' and 'tribalism'. Na licha ya hivyo hizo ni allegations tu.

HARUFU ITAPATIKANA TU TOKA NORWAY {WAKISEMA} SIO DUA, MKANDARA AU MSWAHILI. JE NI LINI TUTAKOMBOKA NA MAWAZO POTOFU?

JK alipokuwa Norway na kusema hatuna wataalam kila mtu alikuja juu, lakini ripoti inapoandikwa na hao hao Norway Mwanakijiji anaikumbatia kuwa ndio ukweli wenyewe, wamewazuga wengi itakuwa Mwanakijiji, tabia yao ni kukutawala kimawazo na hii ni ishara ya kinyonga.

Anasema ingawaje neno hili lipo mara hizo alizohesabu ni vizuri tuanze kuliangalia neno mwanamke, what a joke? Mwanamke = Ukabila ???? Je neno makofi linatokea mara ngapi katika vikao vya bunge? Sasa mbishi ni nani? Aliyeleta document na link ya Norwegian report au ile ya Bunge letu. Uchaguzi ni wako.

jokaKuu

Huyu mbunge aliisha anza kusakamwa kwa EMS na mengine ambayo hakuweza kusema, je unafikiri alikubali kwa hiari yake? Hivi uliona wapi ulimwenguni mtu anapewa compensation wakati hakuna hatia? Tupe mfano naona wengi watajumuika kupata hizo pesa za bure.

Mimi sijaandika waziri na wanasiasa hayo ni maneno yako. Wanasiasa hawakusemwa kwenye kile kifungu cha sheria, ni Waziri tu ambaye anazarauliwa na Commissioner wa TRA.
 
Back
Top Bottom