mtukwao,
maneno mazito hayo... ndugu zetu humu hawataki kukubali kuwa wanaongozwa na ukabila. Wakati wanadai kuna ukabila TRA , ukabila wao wenyewe unawekwa hadharani. Wanapopandikiza mbegu za kuwachukia wachagga, wakati huo huo wanarutubisha chuki ya kikabila ndani yao wenyewe. Leo hii tukisikia kiongozi mchagga amepewa nafasi basi tunajiuliza "kwanini Mchagga?"
Dhambi hii ya ukabila haikomi! Imeanzia kwa wachagga itaenda kwa Wahaya, Wanyakyusa, Wangoni (wa kunyumba) na ni kama mtu kula nyama ya binadamu! Ni mwiko mkubwa ambao ukishauvunja ni vigumu kujikomesha. Ndugu zetu hapa wanajifanya wanasukumwa na uzalendo! kumbe kinachowasukuma ni wivu usio na msingi na chuki isiyokaribishwa! Hawa ndugu tukiwapa nafasi wachague watu kwenye nafasi fulani, la kwanza watakalojiambia ni "wachagga, wahaya, wanyakyusa" hapana!! Wakiona jina la makabila hayo watayakwepa!
Bado tunaendelea kuwapinga, kuwakosoa, na kuwaonesha makosa yao! ili hatimaye wajirudi!