Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

duh.. Kulikoni hawajasema hilo.. tatizo ni kuwa mimi nikizungumza na watu wa TRA peke yake watetezi wa ukabila watasema niko biased kwa vile msimamo wangu unajulikana wazi. Ndio maana nataka wao ndio washindane kwa hoja na watu hao wa TRA. Nitahakikisha kuwa identity zao zinalindwa.
MKJJ!
Ukweli ni kwamba wale ambao walikuwa wakileta data za ukabila wamegoma kuzisimamia data hizo hilo limesimama dhahiri kwa kukataa kwao kushiriki kwenye huo mjadala.Naomba zile zile Data tulizonazo awali ambazo zililetwa hapa JF na zikazusha mtafaruku zitumie kuwauliza maswali atakayesema Uko Biased wakati yeye ambaye hangekuwa biase hakutokea atakuwa hana hoja na ataeleweka hivyo na wote.Tafadhali andaa hayo mahojiano na hili swala liweze kuzikwa au kuwa hai...............Kama linastahili uhai huo...................kitu ambacho ninakidauti..!
 
Hili swala mnalifanya rahisi sana. Kama lingekuwa rahisi hivyo lingeweza kutatuliwa zamani, kuna misingi mingi ambayo ni lazima ifuatwe kama tunataka kutatua jambo, sio mikurupuko kama hii ambayo baadhi ya members wanafikiri ifanyike jinsi wao wanavyotaka. Hao TRA hata mkiwapa ushahidi namna gabi hawawezi kukubali kwamba kuna ukabila. Je wale ambao wanatuhumiwa watakuwepo kwenye upande wa TRA?

JE NI MWIZI YUPI ALIKUBALI KWAMBA YEYE NI MWIZI? BAADA YA HAYA MAHOJIANO NINI KITAFUATA?
 
Dua,
At least watatupa msimamo wao, angalau kutoka jikoni, as it were. Kwa hiyo naamini hili wazo la mahojiano na Mwkjj ni wazo zuri. Tukipanga maswali yetu vizuri itasaida kuonyesha kwa kiasi undani wa TRA. Don't you think so?
 
Dua!
sasa unashauri vipi? Hiyo misingi inayotakiwa ifuatwe ni ipi?Kwanini awali mwanakijiji aliposema kwamba kwasababu ktk pande mbili zinazofautina juu ya hili kila mmoja anaamini hicho anachokiamini hata kama akifanya mahojiano na TRA Bado haitaondoa dhana iliyojengeka?Je kwa kauli yako hapo juu unaamini kwamba aliyosema mwanakijiji hapo awali yana Ukweli juu ya kutokuwa na mantiki ya kuitisha mahojiano na watu wa TRA?
 
Waliokubali kuhojiwa TRA sio ambao wanatakiwa kuhojiwa.
 
Dua,
Hata kama si wao lakini tunaweza kuwauliza maswali juu ya wahusika. Au?
 
Kama ni hivyo tunaweza kumuuliza mtu yeyote akasema vile anavyoamini au sivyo? Tunafahamu Mwanakijiji mawazo yake hapa tulikuwa ni lazima tuweke strategy ya kufanya sio kuuliza every Tom, Dick and Harry.
 
of course.. you don't!! wale mnaotaka kuhojiwa wako tayari...! mimi ndio naonekana zugazuga hapa baana ya kuzungumza nao. Leo napigiwa simu Katibu Muhtasi wa mmoja wao na kuniuliza nimefikia wapi, nimebakia kujiuma meno.. baadhi yao wanasafiri kwenda nje ya nchi in a week or so...! I had two weeks to pull this thing off..
 
of course.. KNKCU.. hilo ndilo nitakalofanya.. ila tukiweka hapa.. watetezi waukabila watakuja "mbona hukuuliza hivi au kile.. oh.. wewe mwanakijiji unafaidika na TRA ndio maana hukuuliza hili wala lile"... this is lose lose situation..
 
Nilitegemea kupata hayo majina kwenye PM lakini sikupewa bali niliambiwa watakuwa etc etc. na kadhalika.
 
Nilitegemea kupata hayo majina kwenye PM lakini sikupewa bali niliambiwa watakuwa etc etc. na kadhalika.
wewe ulipendelea kina nani wahojiwe?Naomba upendekeze na ukizingatia uwezo wa vyombo husika vya kufanyia mahojiano Vina uwezo kuwa HEWANI na watu kama sita pamoja na mtangazaji akiwemo NA makundi yote husika kwenye mada.Tafadhali zingatia uwiano unapopendekeza majina na ueleze!
 
Mwanakjj.
nimekwambia niko tayari hukunipa muda wa interview wala nini? nadhani umekuwa na agenda ya siri. kwani mwanzo uliunda tume na mimi utaniweka kwenye tume kama mwenyekiti. hatujamaliz kazi umeleta mahojiano na nikakupa contact za watu wa kuwahoji pamoja na mimi. ukaingia mitini. umekuja na mpya nyingine. vipi? hueleweki mzee angalia usipoteze jina lako kwa mkate wa siku moja tu.
 
Mwanakjj.
nimekwambia niko tayari hukunipa muda wa interview wala nini? nadhani umekuwa na agenda ya siri. kwani mwanzo uliunda tume na mimi utaniweka kwenye tume kama mwenyekiti. hatujamaliz kazi umeleta mahojiano na nikakupa contact za watu wa kuwahoji pamoja na mimi. ukaingia mitini. umekuja na mpya nyingine. vipi? hueleweki mzee angalia usipoteze jina lako kwa mkate wa siku moja tu.
MKJJ!
Hili nalo unalitolea maelezo ya aina gani?
 
Mswahili!
Kwenye hili MKJJ alishasema amekubali kuwahoji na kikwazo ni wewe na wengine ambao mna data za ukabila pale TRA,Sasa kwasababu uwezo wa mwanakijiji kuhosti watu kwenye KLH NEWS ni mtu sita kwa wakati mmoja kama nilisikia vizuri huko nyuma,
Naomba nipendekeze washiriki wafuatao:
1.Mswahili}KWA UPANDE WANAOTETEA HOJA YA UKABILA TRA
2.Dua }KWA UPANDE WANAOTETEA HOJA YA UKABILA TRA.
3.Chagueni watu wawili toka TRA Ambao nyinyi mngependa wahojiwe.
4.Mwanakijiji
5.Mwanakijiji na wewe naomba uchague mtu mmoja toka TRA,Ambaye unaona anaweza kuwa chanzo kizuri cha information na kuzungumzia swala hili na kujibu maswali kuhusu Ukabila na maswali mengineyo yatakayotolewa. na ufafanuzi utakaohitajika.
Hapo tayari tutakuwa na Idadi ya watu sita.
Pangeni muda wa mahojiano na Yatakayozungumzwa na hao watu wapande mbili tofauti kutoka TRA Kuhusu kuwepo kwa ukabila au laah,(Nikimaanisha upande uliotafutwa na mwanakijiji na upande uliotafutwa na mswahili)Ndiyo liwe jibu la swali letu na hapo ndiyo iwe mwisho wa mjadala huu kwa TRA na tuendelee kwengineko. Sijui MKJJ,DUA ,MSWAHILI NA WANABODI MNALIONAJE PENDEKEZO HILI?
 
Unajua tangia mwanzoni nilisema watu waache kutumia sababu binafsi kujengea "Nadharia za matatizo hata kama hayo matatizo hayapo"
Ni kawaida ya watanzania kutengeneza mazingira ya chuki, wivu, pale kwa watu au kundi la watu tusiowapenda au tulioshindwa kufikia kiwango chao.
Mifano ni mingi hapa JF na hata nje ya hapa.

Mfano tangia kule BCS na hata hapa JF watu wamekuwa wakisema Reginald Mengi anakwepa kodi na anadaiwa zaidi ya bilioni 5 kwa kodi ambayo hajalipa na kesi tayari imeshapelekwa Mahakama ya Biashara. Watu tulipouliza tuliambia kuna ushahid mwingi tu na tukaee mkao wa kula kwani kesi itaanza kunguruma, lakini cha kushangaza ni karibia miaka mitatu sasa hatujaona huo ushahidi siyo hapa tu hata mahakamani. Watu wanabakia kusema anatumia jina la Walemavu kuingiza mali zake binafsi, mara kaangiza benzi kwa kuzingizia ni la walemavu. Mtu mwenye akili timamu hawezi kusema kitu kama hicho, jamani tangia lini Mlemavu akaendesha Benzi sembuse baiskeli ya kusukuma.

Hata serikali hutumia nadharia pale inapoona mambo ya wapinzania ni bora kuliko yao. Chukulia mfano, serikali ya CCM inavyowaambia wananchi kuwa tuchagueni kwani wapinzani hawapendi au hawawezi kuleta maendeleo na hata hudhiriki kusema angalieni sehemu zinazoongozwa na madiwani na wabunge wa vyama vya upinzani yalivyo nyuma kimaendeleo, lakini wakibanwa hawana mfano.

Kuna wakati kuna mtu aliwahi pia kulalamika mbona madaktari na Manesi wengi waliosajiliwa ni kutoka Mikoa ya Kaskazini, nadhani aliyekuwa waziri wa Afya kipindi hicho aliwaambia katembelee huo mkoa utaona wana college ngapi za kusomea unesi kwani kila hospitali ina kituo cha kufundishia, na madaktari wengi tulio nao ni wale waliosomea kwenye vituo kama hivi na kuwa medical officer na baadaye kwenda kuongeza elimu hadi kupata hadhi ya Daktari kamili.

Binafsi siungi mkono upande wo wote ule kwa sasa ila ninataka watu wakilete kero basi wawe tayari kutetea kero zao mpaka mwisho na siyo maswala ya kuishia njiani.

Inawezekana haya yakawa ni mapambano yaleyae ya siku zote; MANJI, QUALITY Group na udini versus MENGI, IPPmedia Group na Uchaga na TRA. Iwapo hata shekhe mzima ananunuliwa kusukuma ajenda, sembuse akina yakhe! Yote Yanawezekana!
 
Back
Top Bottom