Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Mtupori.

Karibu ndugu yetu jamvini umejiunga kuja ku defend uchaga?

imekuwaje wenyeviti wote wa vyama vya siasa kuwa hawana elimu ya kutosha tena wametoka mikoa yenye historia ya elimu?

Mbatia james ni mwenyekiti Nccr elimu yake kidato cha sita tu, Ulotu ni mwenyekiti wa taifa NRA elimu yake darasa la saba, Mrema ni mwenyekiti wa taifa Tlp elimu yake mwalimu wa shule ya msingi hadi uwaziri aliopewa na ruksa alikuwa waziri pekee mwenye elimu duni ndani ya baraza lile la mawaziri na mtu huyo huyo alikuwa Mbunge wa Kilimanjaro huo usomi ulikuwa wapi?

Anna Senkoro nae hana digrii.

Wanabodi.

wakati tunasubiri interview ya redio ya mwanakijiji juu ya ukabila TRA mimi nimeanza kupiga tochi Wizara ya ujenzi na kujua kwanini mabarabara ya Kilimanjaro yalipewa kipaumbele sana kwa bajeti nyingi tu.

ukifuatilia vizuri utaona project cordinator wa mradi wa IPR-INTERGRATED ROAD PROJECT mradi huu ulikuwa chini ya world bank alikuwa mchagga aliyejulikana kwa jina la WILLY LYATUU.

na Kamishina wa Barabara alikuwa mchagga mwingine KIMAMBO

ILIPOKUJA kuanzishwa TANROADS huyo huyo WILLY Lyatuu akawa mkubwa wa mradi na akachagua wachaga kwenye kitengo cha uhasibu alimuweka Mushi, materu na msuya

na idara ya mipango ya wizara ya ujenzi mkuu wake ni mchagga.
world bank walikuwa wakitoa incentives nyingi lakini waliokuwa wakipewa ni wachaga tu.

Lyatuu alikuwa na masecretary wawili Rukia Mohamed Abood(mtoto wa mhasibu mkuu wa serikali mstaafu) na Madeline huyo Rukia alikuwa hapati incentives allowance hadi wafagiaji wa kichagga walikuwa wakipata. lakini madeline alikuwa akipewa.

Lyatuu alikuwa akipeleka masomoni wachaga wenzake tu mfano Mushi alipelekwa Leeds Metropolitan university kwa kozi ya miezi sita na akawa anashikiria mfuko wa Road Fund.

kwa utaratibu huo barabara ya Lindi mtwara hawezi kuisha haraka.
na watu hawa hawa hawawezi kuona aibu kutenga billion 17 kujenga barabara ya Mramba na kuisahau ya Nzega. ukabila ni sumu ya maendeleo na tutazidi kuumulika kila kona.
 
Tusitafute majibu rahisi kwa maswali magumu. Mimi natokea Mbeya, lakini nimekaa sana Tanga, Pwani (Rufiji), Kilimanjaro, Morogoro na nimesoma iringa na Dar. Kwa hiyo angalau nina picha kidogo ya tofauti ya elimu za mikoa hii. Maendeleo ya shule ya mikoa ya K'njaro, Mbeya na Kagera yanatokana na historia, kwamba wamisionari waliwahi kujenga shule maeneo hayo, kwa hiyo sio rahisi sana kulinganisha mikoa na kuwapaka ukabila pasipo sababu. Mpaka kesho, idadi ya shule za K'njaro haiwezi kufanana na ile ya mkoani Rukwa ama Pwani, wala ile ya Mbeya haiwezi kufanana na Lindi au hata jirani zao Singida. Huu ndio ukweli na si kukimbilia kulaumu ukabila,
Mzee Mwanakijiji pokea tano za chap chap, pia mpe Samvula chole hicho kitabu cha Mwalimu Nyerere asome.


Ni kweli shule nyingi zilijengwa wakati wa wakoloni huko Kilimanjaro(Moshi).

Je ni kwa nini hadi sasa hivi mkoa huo bado unapendelewa hadi sasa?

Fedha nyingi sana toka wizara ya Elimu, ( Kuna mchanga Boss wa mfuko wa shule za sekondary) bado zinaenda Moshi kujenga sekondary na Lindi je amewekwa hapo kwa ajili ya Tanzania nzima au kilimanjaro?


Ok, sasa unadhani ni kwa nini serikali imeshindwa kuondoa hizo tofauti za shule TOKA UHURU????

jawabu ni rahisi tu!! wachagga wanajitahidi sana kuhakikisha wanaendelea kuweka gap kubwa!!!!


bye for now.
 
Mkira hebu tutajie angalau shule kumi (10) tu ambazo zimejengwa na Serikali mkoani Kilimanjaro tangi 1995. Halafu linganisha na shule za watu binafsi na makanisa.

Baada ya hapo tupe idadi ya shule za Serikali kwa uwiano na shule za watu binafsi na madhehebu ya dini.

Kuna kitu ambacho mnashindwa kuelewa hapa Tanzania kwa sasa ina shule za Sekondari 2011 (as of June 2006). Katika shule hizi shule 222 ni za Mkoa wa Kilimanjaro. Mikoa inayofuatia ni Mbeya 176, Mwanza 169, Mara 128, Shinyanga 121....

Utaona kuwa mikoa hii ndiko wanakotoka wale wanaosemwa kuwa wanaendekeza Ukabila (Wachagga - Wasukuma - Wanyamwezi)

Swala la kujiuliza (hii inaweza kuwa Thesis ya Mtu): Je kuna uwiano gani kati ya idadi ya Shule na ukabila kwenya kazi za Serikalini, Au kuna uhusiano gani kati ya idadi ya shule na elimu kwa kabila ilipo shule.
 
Aljazeera

Wanaosoma kwenye shule i.e za Kilimanjaro sio wachaga peke yao, Mwanza sio wasukuma peke yao, Mbeya sio wanyakyusa peke yao. mbona unataka kuchanganya mambo hapa.
 
Mkira,
unazungumzia UPENDELEO ktk wizara ya Elimu ya Taifa, au Mamlaka ya Elimu Tanzania[Tanzania Education Authority]?

Tanzania Education Authority wana website yao hii hapa:
http://www.tea.or.tz/index.htm

Board of Directors ya Tanzania Education Authority:
http://www.tea.or.tz/board.htm

Management Team ya Tanzania Education Authority:
http://www.tea.or.tz/management.htm

Hapa kuna habari nyingi, ikiwemo allocation of funds. Bodi ya Wakurugenzi ndiyo inayoidhinisha fedha ziende wapi.
http://www.tea.or.tz/news.htm
 
Aljazeera

Wanaosoma kwenye shule i.e za Kilimanjaro sio wachaga peke yao, Mwanza sio wasukuma peke yao, Mbeya sio wanyakyusa peke yao. mbona unataka kuchanganya mambo hapa.

Ni kweli kwenye shule hizo wanasoma pia watoto wa kutoka nje ya sehemu hizo, lakini bado ni kielelezo muhimu kinachoonyesha umuhimu watu wa sehemu hizo wanaouweka kwenye elimu.
 
Mtukwao,
Bado utakuta asilimia kubwa wanaosoma katika shule hizo ni wakazi wa maeneo hayo, hata kama kuna makabila mengine.
 
Hata jamaa wa Ghana walikuja TRA kujifunza!!

Na jamaa wa nchi kibao za Afrika washakuja kwenye Bima ya Afya ya Tanzania kujifunza licha ya kwamba huko kuna Wanyamulenge kibao!
 
While you are still at it guys, listen to the voice of Mrema!


2007-03-27 09:50:21
Na Abdul Mitumba


Dalili za kukua kwa sekta ya elimu katika mikoa ya Kagera, Kilimanjaro, Mbeya na Arusha zilikuwepo hata kabla ya uhuru na hadi sasa inazidi kusonga mbele kielimu, huku mikoa mingine kama Lindi, Mtwara, Singida, Kigoma na Rukwa ikizidi kuyumba.

Moja kati ya sababu zilizotajwa ni mifumo ya utawala isiyozingatia uwiano. Nini kifanyike kuweka uwiano huo. Mwenyekiti wa TLP, Bw.Augustine Mrema anashauri katika makala hii ya Mwandishi Abdul Mitumba.


Huku shule za sekondari za taasisi binafsi zikiendelea kufanya vizuri kitaaluma, hali si ya kuridhisha kwa upande wa shule za sekondari za serikali.Baadhi yake hazina walimu wa kutosha kulinganisha mahitaji.

Tatizo hilo limesababishwa na uamuzi wa baadhi ya walimu kutafuta maslahi bora katika shule binafsi na kuziacha shule za serikali zikiwa hazina walimu wenye sifa.

Wataalam wa mafunzo kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na wanasiasa wanasema hali hiyo ndio iliyochangia kwa kiasi kikubwa wanafunzi wengi kushindwa kupata alama za kuwawezesha kujiunga na elimu ya juu katika vyuo vikuu vya ndani na nje.

Miongoni mwa wanasiasa waliotoa maoni yao juu ya kuzorota kwa elimu ni Bw. Augustine Mrema, Mwenyekiti wa TLP ambaye anasema ana wasiwasi juu ya tatizo hilo akisema kama serikali haitachukua hatua kutafuta ufumbuzi mapema, mikoa itaendelea kuwa na uwiano mbaya katika maendeleo ya sekta ya elimu.

``Tutaendelea kuwa na wasomi kutoka mikoa michache tu yenye watu wanaopenda au waliowezeshwa kuwekeza katika sekta ya elimu,`` anasema Bw Mrema.
Akaongeza kuwa kwa mikoa ya Mbeya, Kagera, Kilimanjaro na Arusha kuongoza kuwa na watu wengi walioendelea kielimu ni dalili tosha kwamba maeneo mengi yataendelea kuwa na uwiano mbaya katika maendeleo ya elimu.

Anasema wakati mikoa mingi haina shule za sekondari za kutosha, mikoa
hiyo ina shule nyingi za binafsi na walimu wengi wenye viwango vya juu vya elimu`.

``Mtu anapokuwa na kiwango bora cha taaluma ni wazi atakuwa katika nafasi ya kufundisha vizuri, japokuwa shule hizo zinatoa elimu kwa gharama kubwa.

``Gharama katika shule hizo ni za juu na wazazi wachache tu ndio wanaomudu kulipa ada. Lakini hata sekondari za serikali zilizomo katika mikoa hiyo zina walimu wengi na wenye viwango vizuri vya taaluma…watoto wanaosoma huko ndio wanaopata nafasi ya kusoma vyuo vikuu,`` anasema Bw.Mrema.

Anasema uwiano mzuri wa elimu miongoni mwa maeneo utapatikana kwa kila eneo kuwa na shule nyingi za sekondari pamoja na za watu binafsi zinazoendeshwa kwa ufanisi na kujali maslahi ya walimu.

Akasema kwa sasa ni shule za watu binafsi tu ndizo zinazojali maslahi ya walimu, hali ambayo inasababisha walimu wengi kuzikimbia shule za serikali.

``Katika hilo ni wazi wengine wananunuliwa kwa fedha nyingi na shule binafsi zikiwemo zinazomilikiwa na taasisi za dini kama misheni.``
Nini kifanyike wakati huu:
Ili kurekebisha hali hiyo Bw. Mrema anaishauri serikali kuweka vivutio kwa walimu wanaokubali kwenda kufundisha katika sekondari za serikali zilizoko wilayani na katika kata ili kuwajengea ari mpya, nguvu na kasi mpya kama falsafa ya serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete inavyosema.

Anasema vivutio vinaweza kupatikana kwa kuwaongeza maslahi walimu walioko katika mikoa ya pembezoni mwa nchi ambayo iliachwa nyuma kimaendeleo.

Kwa hali hiyo, Mrema anasema walimu watapenda mazingira ya vijijini, tofauti na sasa ambapo wengi wao wanakimbilia kufundisha zaidi mijini.

``Lindi, Mtwara, Singida, Rukwa na Kigoma ni baadhi ya mikoa ya mfano inayotakiwa kupewa kipaumbele ili iweze kusogea kwa haraka mbele kimaendeleo kama mikoa mingine,`` anasema Bw. Mrema.

Akaongeza kuwa kwa sasa, hata kama mikoa hiyo imeitikia wito wa serikali kwa wananchi kujenga shule za sekondari katika kila kata, hatua hiyo haitakuwa na maana endapo shule hizo zitakosa walimu wenye viwango vizuri vya taaluma.

Bw. Mrema anasema ingawa uwiano baina ya mkoa na mkoa, kielimu hauwezi kupatikana kirahisi, lakini ni vizuri kwa serikali kuwa na mikakati ya muda mrefu ya utekelezaji.

Zipo njia kadhaa za kuchukua ili kuwashawishi walimu kwenda na kufundisha katika sekondari za wilaya na kata,
Baadhi ya njia hizo ni kuwahakikishia kuwa mishahara yao italipwa kwa wakati na kuwafikishia mahali walipo na kuwawezesha kukopa fedha kwa ajili ya kuanzisha miradi ya maendeleo ili kuongeza vipato vyao.

Kadhalika, kuwajengea nyumba bora za kuishi, kuwakopesha vifaa vya usafiri kama vile baiskeli na pikipiki ili iwe rahisi kwao kusafiri kutoka kijiji kimoja hadi kingine.

Bw.Mrema anaamini kwa kufanya haya, mikoa iliyo nyuma na ile iliyopembezoni mwa nchi itapata walimu wazuri hatimaye wananchi wake kupata elimu na kuchangia katika maendeleo ya taifa lao.

Kauli ya Bw. Mrema imekuja wakati utekelezaji wa ahadi ya Rais Jakaya Kikwete ya kutoa kipaumbele kwa mikoa hiyo ukiwa umeanza.

Moja ya maeneo hayo ni kuanza kwa ujenzi wa shule za sekondari katika maeneo ya jamii ya wafugaji mkaoni Arusha, ambao kwa muda mrefu wamekuwa hawasomi kutokana na mazingira kuwabana.

SOURCE: Nipashe
 
wana jamboForums,

Wakala wa Barabara Tanzania, Tanroads:

1.nimesoma taarifa za tanroads nimekuta kuna miradi michache sana ya barabara ktk mkoa wa kilimanjaro. sikuona dalili za upendeleo.

2.pia taarifa za tanroads zinathibitisha yale yaliyokuwa kwenye bajeti aliyosoma Basil Mramba wakati akiwa waziri wa miundombinu.

3.Management ya tanroads iko diversified. sikuona kama wachaga wamejaa humo. sifahamu kuhusu watumishi wa ngazi za kati, na chini, lakini management nimeona iko vizuri.

Mamlaka ya Elimu Tanzania:

1.Mamlaka ya Elimu nayo nimesoma taarifa yao ya June2006 nikakuta wamesaidia shule kama nne hivi toka kilimanjaro. nikasoma zaidi nikakuta mamlaka pia imesaidia shule 3, na Kigoma shule 4. Kwa kuangalia haraka, nadhani Arusha ndiyo wamesaidiwa zaidi.

2.kuhusu bodi yao ya wakurugenzi, naamini wengi wanaingia humo kutokana na nyadhifa zao serikalini. sikuona wachaga wengi.

3.Management ya Mamlaka ya Elimu nayo haikusheheni wachaga.

naelewa Tanzania tuna matatizo mengi, lakini inaogopesha tunapojaribu kulaumu sehemu ya jamii yetu kama chanzo cha matatizo yetu. mfano mdogo, ni kitendo cha kulaumu wachaga kwa kuzorota kwa ujenzi wa barabara za maeneo mbalimbali tanzania.
 
nafikiri wangewakatalia hao wachagga, wanyakyusa, na wahaya ili kutoa uwiano kidogo..!! Ambao wangestahili kupewa zawadi ni wale ambao makabila yao hayana wasomi wengi ili kuwatia moyo watu wa makabila hayo.
 
nafikiri wangewakatalia hao wachagga, wanyakyusa, na wahaya ili kutoa uwiano kidogo..!! Ambao wangestahili kupewa zawadi ni wale ambao makabila yao hayana wasomi wengi ili kuwatia moyo watu wa makabila hayo.

Unaunalolitafuta.....................................Msubiri Mhusika ..............I was around....................!
 
Kama hakuna au wapo mmoja mmoja wa makabila yaliyotajwa which is fine to me, yakujiuliza ni;
1. Inakuwaje huko TRA predominantly ni wachaga ? is it a coincidence or an accident? or combination of the two?

2. Je suala la kihistoria mbona halipo hapo? kama lipo basi wachaga wangekuwa wengi!
 
Kama hakuna au wapo mmoja mmoja wa makabila yaliyotajwa which is fine to me, yakujiuliza ni;
1. Inakuwaje huko TRA predominantly ni wachaga ? is it a coincidence or an accident? or combination of the two?

2. Je suala la kihistoria mbona halipo hapo? kama lipo basi wachaga wangekuwa wengi!

Unajua mimi nimeona waliofaulu vizuri wametoa picha ya utaifa kwa kiasi fulani .Sasa naona MKJJ anawasha moto aliozoea kuwashiana na Mswahili kwa kuendeleza yale yale kila mmoja analoliamini Ndiyo maana nikasema ,I was around............................. !kwenye hili wataelewana na Mzee wa Data Mswahili!
 
KNKCU.
Nipo mkuu huyo mwanakjj hana kitu nimeweka shule na watoto waliofanya vizuri hakuna shule toka Kilimanjaro hiyo historia iko TRA tu? ilitakiwa wanafunzi wote watoke Kilimanjaro.

mimi sina ugomvi na watu wa Mbeya ndio maana nalia na Benny Lusege kijana wa Mbeya aliyekabwa kwa ukabila tra.
tumeambiwa kuna interview hadi sasa kimya. tunasubiri kwa hamu kuwaumbua kina Kittlya na kundi lake.
 
Written by Ester Bulaya
Saturday, 31 March 2007
Asema Mungu ndiye ajuaye ukweli, kulambwa bakora 12

JUSTINE Kasusura (48) jana alipigwa na butwaa baada ya kuhukumiwa miaka 30 jela na viboko 12, huku akishuhudia wenzake wanne wakiachiwa huru na kumuacha pekee yake kwenye kizimba cha mahakama.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Kasusura alipelekwa gerezani akiwa chini ya ulinzi mkali ambapo alipakizwa kwenye gari lenye king'ora akiwa amezungukwa na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) huku akisindikizwa na Defender lililojaa polisi.
Kasusura aliyekuwa akikabiliwa na mashitaka ya wizi wa kutumia silaha na kuiba dola za Marekani milioni mbili, alihukumiwa kifungo hicho na Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi Sivangilwa Mwangesi wa Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam.
Hukumu hiyo ilianza kusomwa saa 5.50 asubuhi ambapo Kasusura alipanda kizimbani huku akiwa amevalia suruali nyeusi na shati la kitenge na alionekana ni mtu mwenye furaha na kujiamini.
Lakini alibadilika sura pale alipobaki mwenyewe kizimbani na kumsikia hakimu akitamka kwamba ametiwa hatiani katika makosa ya wizi na wizi wa kutumia silaha.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mwangesi alisema hakuna ubishi kwamba siku ya tukio Agosti 2, mwaka 2001, Kasusura akiwa na shahidi wa kwanza wa upande wa mashitaka, Saidi Mussa, walitumwa kwenda uwanja wa ndege kuchukua mzigo ambao juu uliandikwa kuwa ni pesa.
Mwangesi alisema kulingana na ushahidi, mahakama imeridhika kuwa siku hiyo Kasusura alikuwa na silaha aina ya bastola.
Alisema maelezo ya mashahidi wa upande wa mashitaka kuhusu mtu aliyekwendakuchukua fedha hizo, yanaungana na maelezo ya onyo aliyoyatoa Kasusura, kwamba ni kweli alitumwa na bosi wake na kweli alikuwa amezichukua fedha hizo yeye mwenyewe.
"Kulingana na ushahidi wa shahidi wa kwanza na 14, ambao unaelezea Kasusura ndiye aliyechukua fedha hizo na kwamba alikuwa na silaha aina ya bastola, huku shahidi wa kwanza Mussa alidai alitishiwa bastola na Kasusura akimlazimisha kusimamisha gari na kumweleza kuwa mkataba wangu na wako umekwisha wewe nenda zako.
"Ushahidi huo umeungwa mkono na maelezo ya onyo aliyotoa Kasusura mwenyewe, maelezo hayo yalitolewa kama kielelezo na upande wa mashitaka, Kasusura alieleza kuwa baada ya kuchukua fedha alimtishia kwa bastola Mussa ambaye walikuwa naye kwenye gari na kumuamuru asimamishe gari huku akimueleza kuwa hawajuani. Kutokana na kuungwa mkono na maelezo hayo, mahakama inasema Kasusura aliiba fedha na alitumia silaha," alisema Hakimu Mwangesi.
Aliongeza kuwa: "Mahakama imethibitisha kuwa, wewe ndiye ulichukua fedha na mwenyewe ulikiri kwani ndiye uliyetumwa na bosi wako, ingawa ulileta maelezo uliyodai baada ya kuchukua fedha hizo, ulimkabidhi bosi wako ambaye alikufuata huko uwanja wa ndege, kisha akakupa kazi nyingine na kusafiri kwenda Mbeya, kushika nafasi ya mfanyakazi mwenzako wa Knight Support aliyekuwa akienda likizo."
"...maelezo yako haya hayaungwi mkono na maelezo mengine na hayana uzito ukilinganisha na hoja za mashahidi wa upande wa mashitaka ambao hata wewe uliyaeleza. Mahakama inaona wewe ndiye ulichukua fedha hizo ingawa idadi yake haikufahamika na hakuna shahidi aliyekuja kuthibitisha kuwa zilikuwa dola milioni mbili, hivyo fedha hizo wewe ndiye ulichukua na ulijua ulikozipeleka, kwani hukupeleka kule ulikotakiwa kama bosi wako alivyokuagiza," alisisitiza Mwangesi
Hakimu Mwangesi alisema, kulingana na ushahidi huo, Kasusura anayo hatia ya makosa hayo.
"Mahakama inaona una hatia na umefanya wizi huo, hilo halina ubishi kwa kuwa nimefungwa pingu kwa mujibu wa sheria, natoa adhabu kama ifuatavyo; kosa la wizi una hukumiwa miaka mitano gerezani, kosa la wizi wa kutumia silaha ni miaka 30 haipungui wala haiongezeki kama sheria inavyoagiza, utatumikia kifungo cha miaka 30 kwani adhabu zitaenda sambamba, lakini pia utachapwa viboko 12, sita wakati wa kutoka na sita wakati wa kuingia," alisema.
Hakimu Mwangesi alipokuwa akiwaachia huru washitakiwa Leornad Urasa, Wyclif Urasa, Lucy Urasa na Libert Lukondwa, alisema kwa upande wa Wyclif na Leornad, upande wa mashitaka ulishindwa kuthibitisha kwamba washitakiwa hao ni kweli walishiriki kufanya wizi huo na Kasusura.
Alisema katika shitaka la kula njama linalowakabili washitakiwa hao, hakuna ushahidi ulioeleza kuwa ni kweli washitakiwa hao walikula njama ya kutenda kosa, ambapo shahidi wa tatu aliyekuwepo karibu na eneo la tukio na kulishuhudia, alidai mahakamani aliwaona watu wengine wakiingia kwenye gari haraka haraka, lakini alishindwa kuwatambua kama ndiyo washitakiwa.
Hakimu Mwangesi alisema pia katika maelezo ya onyo aliyoyatoa Kasusura, alidai kabla ya kufanya tukio hilo alipanga na akina Urasa kwamba akitumwa kuchukua fedha atawajulisha, lakini maelezo hayo hayaungwi mkono na ushahidi wa upande wa mashitaka hivyo washitakiwa hawa hawana hatia.
"Kwani kuna akina Urasa wengi na katika kesi hii wapo watatu ni Urasa gani? Sikupewa jibu hilo," alisema hakimu.
Hakimu Mwangesi alisema kwa upande wa washitakiwa Lucy na Lukondwa, hakuna ushahidi ulioithibitishia mahakama kuwa walipokea fedha za wizi, ambapo kwa upande wa Lucy kutokana na maelezo ya polisi, Kasusura alidai kuwa fedha hizo dola milioni mbili baada ya kuiba walimkabidhi Lucy ambaye ni mke wa Leornad.
Kwa upande mwingine, Hakimu Mwangesi alisema Lucy aliunganishwa katika kesi hiyo kimakosa, kwani polisi walidhani ni mke wa Kasusura.
Kwa upande wa Lukondwa, Hakimu Mwangesi alisema anamuachia huru kwa kuwa hakuna ushahidi wa kumtia hatiani.
Kasusura aliyekuwa akibadilika badilika kwa mshangao na kutoamini macho yake kwani kuna muda mwingine alikuwa akitabasabu, akicheka, akiongea pekee yake na hata kukunja sura na kuzubaa, alipokuwa kizimbani pekee yake. Kasusura alijifuta jasho zaidi ya mara 16 huku akitetemeka midomo.
Baada ya hukumu hiyo kutolewa, ndugu wa Kasusura walikuwa wakilia kwa uchungu huku mwenyewe akiondoka kizimbani akicheka kama ishara ya kukubali kilichotokea.
Kasusura aliondoka chini ya ulinzi mkali huku akipunga mikono na kuwaambia waandishi kuwa hukumu hiyo imetolewa kwa shinikizo, lakini ukweli ni kwamba hakuhusika na wizi wa fedha hizo na kusisitiza kuwa hakuwa na silaha.
Kasusura aliongeza kuwa Mungu ndiye aliyepanga kupata adhabu hiyo na hakimu ameshahitimisha hivyo hana la kufanya.
Wakili aliyekuwa akimtetea Kasusura, Majura Magafu, alisema kulingana na sheria ya adhabu ya makosa ya wizi wa kutumia silaha, hana cha kusema bali anaiachia mahakama kwani adhabu yake ni moja tu haipungui wala kuongezeka.
Mashahidi 14 wa upande wa mashitaka na vielelezo 27 ndiyo vilivyoithibitishia mahakama kuwa kweli Kasusura aliiba fedha hizo.
Kasusura amekaa rumande kwa zaidi ya miaka sita wakati akiendelea na kesi hiyo ya wizi wa kutumia silaha na kupora dola Milioni mbili mali ya City Benki.
Tukio hilo lilitokea Agosti 2, mwaka 2001 saa tatu asubuhi katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere ambapo kwa kipindi hicho, Kasusura alikuwa dereva wa kampuni ya ulinzi ya Knight Support.
 
Mwanakjj na Phillimon mikael.
naona kina Urassa wamemtosa Kasusura nadhani sababu ya historia imefanya kazi yake na Dpp angekuwa Shayo au Munisi mnaowalilia kungekuwa hakutoshi.
 
Back
Top Bottom